Ushahi wa Mabilioni ya Ford kwa Maria Sarungi kuchochea migogoro.

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
Pamoja na juhudi na nia njema za Serikali, kumekuwepo na makundi mbalimbali yanayopokea fedha kutoka nje ili kufitinisha Wamasai na wananchi dhidi ya serikali.

Mfano wa hili ni taasisi ya Mwanzo inayoongozwa na Maria Sarungi, ambayo imepokea zaidi ya dola za Kimarekani 400,000, sawa na zaidi ya shilingi bilioni moja, kwa ajili ya kuendesha kampeni ya kuhamasisha Wamasai wasihame na pia kuichafua serikali.

Swali la kujiuliza ni kwa nini mashirika ya kimataifa yanawekeza mabilioni kuyafadhili mashirika kama yale ya Maria Sarungi na mengineyo kwa lengo la kuleta mgongano kati ya serikali na wananchi wake?

Hali ilivyo Sasa

Kwa sasa, mchakato wa uhamisho unaendelea, huku idadi kubwa ya familia za Wamasai zikiwa zimehamia maeneo mapya kwa hiari.

Serikali inaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu, ikitoa msaada unaohitajika kwa wale waliohamia na kudumisha njia za wazi za mawasiliano na wale waliobaki.

Changamoto zilizopo Ngorongoro ni ishara ya masuala mapana yanayokabili jitihada za uhifadhi barani Afrika.

Mbinu ya serikali ya Tanzania inaonyesha sera yenye uwajibikaji na maono inayoleta usawa kati ya uhifadhi wa mazingira na watu walioishi kwa amani na mazingira hayo kwa karne nyingi.

Hitimisho

Uhamisho wa Wamasai kutoka Ngorongoro ni ushahidi wa kujitolea kwa serikali ya Tanzania kwa maendeleo endelevu.

Kwa kuweka kipaumbele uhifadhi na ustawi wa Wamasai, serikali inafanya kazi kuhakikisha kuwa Eneo la Hifadhi la Ngorongoro linabaki kuwa urithi wa dunia unaotambulika, huku pia ikiunda mustakabali mzuri kwa watu wa jamii ya Wamasai.

Suala hili tata linahitaji uelewa na msaada kutoka kwa pande zote zinazohusika. Hatua za serikali ni kielelezo cha kujitolea kwake kufanya yaliyo bora kwa mazingira na watu wake, sasa na katika siku zijazo.
 
Attachments

  • 9bfd899e-ddfd-4416-8a6b-93b11f498a45.jpeg
    9bfd899e-ddfd-4416-8a6b-93b11f498a45.jpeg
    342.4 KB · Views: 8
  • 9cc3a3c9-6466-4b6e-be5b-eb47689b5fe2.jpeg
    9cc3a3c9-6466-4b6e-be5b-eb47689b5fe2.jpeg
    316.2 KB · Views: 9
  • 11369ad1-84d3-4a7d-874d-ae7d67883362.jpeg
    11369ad1-84d3-4a7d-874d-ae7d67883362.jpeg
    97.5 KB · Views: 9
“Hatua ya kufuta vijiji na vitongoji ni hatua inayoenda mbali sana. Maana yake ni kwamba wananchi wahusika hawatakuwa na serikali zao za mitaa vijijini na vitongojini. Hii ni kinyume cha ibara ya 145 na 146 ya Katiba ambayo inazungumzia Madaraka ya Umma na kuweka Serikali za Mitaa. Kuwa na madaraka ngazi ya vijiji ni mosi, kuimarisha demokrasia ngazi za chini; pili kuwezesha wananchi waishio vijijini kushiriki katika utawala ambayo ni haki yao kwa mujibu wa ibara 21(1); na tatu, waishio katika eneo hilo kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika Halmashauri zao kama wananchi wenzao waishio katika maeneo mengine. Kwa kuwa vijiji vimefutwa wananchi hao watakosa haki hizo. Kwa maneno mengine wamekuwa disenfranchised (Kuporwa haki). Jamani tunaelekea wapi? Nini lengo la kufanya hivyo? Je tuelewe vipi? Tuambiwe waziwazi kama jamii ya Kimaasai waishio Ngorongoro ni wananchi au wakimbizi wa ndani? Prof. Shivji

Maneno ya Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Profesa wa Sheria Profesa Issa Shivji kupitia mtandao wake wa X.
20240820_162254.jpg
 
Mzee Mgaya: Kimsingi huwezi kufuta Kijiji, Kata wala Tarafa kwa Sababu hao ni Watu

Mipaka ya kiserikali kwa ajili ya Utawala huwakuta Watu katika maeneo yao na unapowaondoa ni lazima uwalipe fedha za Kuishi hadi watakapokufa

My take; Mzee Mgaya ana pweinti 😄
Mikoa huanzishwa na kufutwa
 
Mzee Mgaya: Kimsingi huwezi kufuta Kijiji, Kata wala Tarafa kwa Sababu hao ni Watu

Mipaka ya kiserikali kwa ajili ya Utawala huwakuta Watu katika maeneo yao na unapowaondoa ni lazima uwalipe fedha za Kuishi hadi watakapokufa

My take; Mzee Mgaya ana pweinti 😄
Mikoa huanzishwa na
 
“Hatua ya kufuta vijiji na vitongoji ni hatua inayoenda mbali sana. Maana yake ni kwamba wananchi wahusika hawatakuwa na serikali zao za mitaa vijijini na vitongojini. Hii ni kinyume cha ibara ya 145 na 146 ya Katiba ambayo inazungumzia Madaraka ya Umma na kuweka Serikali za Mitaa. Kuwa na madaraka ngazi ya vijiji ni mosi, kuimarisha demokrasia ngazi za chini; pili kuwezesha wananchi waishio vijijini kushiriki katika utawala ambayo ni haki yao kwa mujibu wa ibara 21(1); na tatu, waishio katika eneo hilo kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika Halmashauri zao kama wananchi wenzao waishio katika maeneo mengine. Kwa kuwa vijiji vimefutwa wananchi hao watakosa haki hizo. Kwa maneno mengine wamekuwa disenfranchised (Kuporwa haki). Jamani tunaelekea wapi? Nini lengo la kufanya hivyo? Je tuelewe vipi? Tuambiwe waziwazi kama jamii ya Kimaasai waishio Ngorongoro ni wananchi au wakimbizi wa ndani? Prof. Shivji

Maneno ya Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Profesa wa Sheria Profesa Issa Shivji kupitia mtandao wake wa X.View attachment 3074949
Ameifuta kwenye mtandao wake wa x sijui kwanini
 
Ila mimi bado sikubali kwamba serikali inaweza kudhulumu wananchi wake kwa sababu Rais hana nguvu za kipekee , kuna watu wanasapot tena kutoka sehemu tofauti kufanya maamuzi hususani katika uteuzi na miradi .

Kesi kama hiyo ni mbaya sana kweny mahakama ya dunia sio rahisi kufanya maamuzi bila ya kujua faida yake...Ifike mahali tuongee ukweli sio kufuata wanasiasa mbona ishu ya bnadari ilifanikiwa , CCM wa ovyo ila hawawezi kufanya maamuzi ya namna hiyo .

Sehemu hiyo ni miongoni mwa foreign investment kama moja ya matakwa ya WB&IFM.
 
mnaib*ka katiba & serikali inatesa wananchi wake, unategemea wasaidiwe na nani? Hizo western-sceptic ideologies hazitawaokoa this time, alikua anaweza Magu tu kuaminisha waTZ kuwa wazungu hawana jema. Nyie, not so much
 
Ila mimi bado sikubali kwamba serikali inaweza kudhulumu wananchi wake kwa sababu Rais hana nguvu za kipekee , kuna watu wanasapot tena kutoka sehemu tofauti kufanya maamuzi hususani katika uteuzi na miradi .

Kesi kama hiyo ni mbaya sana kweny mahakama ya dunia sio rahisi kufanya maamuzi bila ya kujua faida yake...Ifike mahali tuongee ukweli sio kufuata wanasiasa mbona ishu ya bnadari ilifanikiwa , CCM wa ovyo ila hawawezi kufanya maamuzi ya namna hiyo .

Sehemu hiyo ni miongoni mwa foreign investment kama moja ya matakwa ya WB&IFM.
ask the Chinese (Mao zeDong), Cambodians(Pol Pot), North Koreans(ukoo wa Kim), Venezuelans(Maduro), Americans(Biden,Obama FDR n.k), British(under Starmer) etc. Serikali zote duniani as long as zinaongozwa na wanadamu zina asili ya udhalimu dhidi ya raia wanaowatawala.
 
Pamoja na juhudi na nia njema za Serikali, kumekuwepo na makundi mbalimbali yanayopokea fedha kutoka nje ili kufitinisha Wamasai na wananchi dhidi ya serikali.

Mfano wa hili ni taasisi ya Mwanzo inayoongozwa na Maria Sarungi, ambayo imepokea zaidi ya dola za Kimarekani 400,000, sawa na zaidi ya shilingi bilioni moja, kwa ajili ya kuendesha kampeni ya kuhamasisha Wamasai wasihame na pia kuichafua serikali.

Swali la kujiuliza ni kwa nini mashirika ya kimataifa yanawekeza mabilioni kuyafadhili mashirika kama yale ya Maria Sarungi na mengineyo kwa lengo la kuleta mgongano kati ya serikali na wananchi wake?

Hali ilivyo Sasa

Kwa sasa, mchakato wa uhamisho unaendelea, huku idadi kubwa ya familia za Wamasai zikiwa zimehamia maeneo mapya kwa hiari.

Serikali inaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu, ikitoa msaada unaohitajika kwa wale waliohamia na kudumisha njia za wazi za mawasiliano na wale waliobaki.

Changamoto zilizopo Ngorongoro ni ishara ya masuala mapana yanayokabili jitihada za uhifadhi barani Afrika.

Mbinu ya serikali ya Tanzania inaonyesha sera yenye uwajibikaji na maono inayoleta usawa kati ya uhifadhi wa mazingira na watu walioishi kwa amani na mazingira hayo kwa karne nyingi.

Hitimisho

Uhamisho wa Wamasai kutoka Ngorongoro ni ushahidi wa kujitolea kwa serikali ya Tanzania kwa maendeleo endelevu.

Kwa kuweka kipaumbele uhifadhi na ustawi wa Wamasai, serikali inafanya kazi kuhakikisha kuwa Eneo la Hifadhi la Ngorongoro linabaki kuwa urithi wa dunia unaotambulika, huku pia ikiunda mustakabali mzuri kwa watu wa jamii ya Wamasai.

Suala hili tata linahitaji uelewa na msaada kutoka kwa pande zote zinazohusika. Hatua za serikali ni kielelezo cha kujitolea kwake kufanya yaliyo bora kwa mazingira na watu wake, sasa na katika siku zijazo.
Petty issues kama kawaida. Nani anayewalipa machawa wanaozunguka kila sehemu bila kazi maalumu? Hela zinatoka wapi?
Kama sisi wote tunataka kupinga watu wa aina hiyo, tujifunze kuwa safi na waadilifu. Vinginevyo, ni kuonea wivu nani ana chanzo kizuri cha mapato, katika kuitafuna fursa yetu. Inasikitisha sana maana hakuna aliye na afadhali
 
ask the Chinese (Mao zeDong), Cambodians(Pol Pot), North Koreans(ukoo wa Kim), Venezuelans(Maduro), Americans(Biden,Obama FDR n.k), British(under Starmer) etc. Serikali zote duniani as long as zinaongozwa na wanadamu zina asili ya udhalimu dhidi ya raia wanaowatawala.
Sio rahisi mzee kufanya uhuni tena nchi ndogo kama hii , kesho tu kikwazo kama laki .
 
The West has a functioning brain, wanaangalia na historia ya nchi, na pia wanaangalia na vitu vya ku-react vile vile. Unafikiri hawaoni ya kina Kagame, Paul Biya, ya huko Sudani Kusini , huko Nigeria + na huko Chad yanayoendelea.

Kuna mitafaruku mengine wont bring good PR to them, wakijiingiza. Huu wameuona unawafaa
 
“Hatua ya kufuta vijiji na vitongoji ni hatua inayoenda mbali sana. Maana yake ni kwamba wananchi wahusika hawatakuwa na serikali zao za mitaa vijijini na vitongojini. Hii ni kinyume cha ibara ya 145 na 146 ya Katiba ambayo inazungumzia Madaraka ya Umma na kuweka Serikali za Mitaa. Kuwa na madaraka ngazi ya vijiji ni mosi, kuimarisha demokrasia ngazi za chini; pili kuwezesha wananchi waishio vijijini kushiriki katika utawala ambayo ni haki yao kwa mujibu wa ibara 21(1); na tatu, waishio katika eneo hilo kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika Halmashauri zao kama wananchi wenzao waishio katika maeneo mengine. Kwa kuwa vijiji vimefutwa wananchi hao watakosa haki hizo. Kwa maneno mengine wamekuwa disenfranchised (Kuporwa haki). Jamani tunaelekea wapi? Nini lengo la kufanya hivyo? Je tuelewe vipi? Tuambiwe waziwazi kama jamii ya Kimaasai waishio Ngorongoro ni wananchi au wakimbizi wa ndani? Prof. Shivji

Maneno ya Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Profesa wa Sheria Profesa Issa Shivji kupitia mtandao wake wa X.View attachment 3074949
Mbona Prof Shivji kaifuta hii ilikuwaje….?
 
Pamoja na juhudi na nia njema za Serikali, kumekuwepo na makundi mbalimbali yanayopokea fedha kutoka nje ili kufitinisha Wamasai na wananchi dhidi ya serikali.

Mfano wa hili ni taasisi ya Mwanzo inayoongozwa na Maria Sarungi, ambayo imepokea zaidi ya dola za Kimarekani 400,000, sawa na zaidi ya shilingi bilioni moja, kwa ajili ya kuendesha kampeni ya kuhamasisha Wamasai wasihame na pia kuichafua serikali.

Swali la kujiuliza ni kwa nini mashirika ya kimataifa yanawekeza mabilioni kuyafadhili mashirika kama yale ya Maria Sarungi na mengineyo kwa lengo la kuleta mgongano kati ya serikali na wananchi wake?

Hali ilivyo Sasa

Kwa sasa, mchakato wa uhamisho unaendelea, huku idadi kubwa ya familia za Wamasai zikiwa zimehamia maeneo mapya kwa hiari.

Serikali inaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu, ikitoa msaada unaohitajika kwa wale waliohamia na kudumisha njia za wazi za mawasiliano na wale waliobaki.

Changamoto zilizopo Ngorongoro ni ishara ya masuala mapana yanayokabili jitihada za uhifadhi barani Afrika.

Mbinu ya serikali ya Tanzania inaonyesha sera yenye uwajibikaji na maono inayoleta usawa kati ya uhifadhi wa mazingira na watu walioishi kwa amani na mazingira hayo kwa karne nyingi.

Hitimisho

Uhamisho wa Wamasai kutoka Ngorongoro ni ushahidi wa kujitolea kwa serikali ya Tanzania kwa maendeleo endelevu.

Kwa kuweka kipaumbele uhifadhi na ustawi wa Wamasai, serikali inafanya kazi kuhakikisha kuwa Eneo la Hifadhi la Ngorongoro linabaki kuwa urithi wa dunia unaotambulika, huku pia ikiunda mustakabali mzuri kwa watu wa jamii ya Wamasai.

Suala hili tata linahitaji uelewa na msaada kutoka kwa pande zote zinazohusika. Hatua za serikali ni kielelezo cha kujitolea kwake kufanya yaliyo bora kwa mazingira na watu wake, sasa na katika siku zijazo.
Kumbe ni mgogoro kati ya serikali vs wananchi..

Mimi nilikuwa nadhani utasema anaipinga nchi na taifa, lakini kumbe ni dhidi ya serikali..?

Sasa wewe huelewi nini hapo maana serikali zote popote duniani huwa zinapingwa zinaposhindwa kukidhi matarajio ya watu...

Sera, mipango na mikakati ya serikali kutekeleza sera au mpango fulani huungwa mkono na wananchi au kama ni mbaya, basi, hupingwa na kukosolewa big time kwa nguvu na kwa mbinu zozote na wananchi. Hili siyo kosa la jinai hata kidogo..!

Na ndiyo maana serikali huja na kuondoka..

Serikali hii sera na mipango yake ikikataliwa, basi serikali hiyo hufurushwa na wananchi na kuondolewa Ili kuruhusu serikali bora zaidi kuja kwa kufuata utaratibu na njia zilizowekwa kikatiba..

Nchi na taifa lenyewe hubaki na kudumu siku zote lakini huondoka..

Serikali hii ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan haifai, imeshimdwa na inastahili kukosolewa na kupingwa kwa nguvu zote kitaifa na kimataifa mpaka iondoke yenyewe..

Kwa hiyo, hakuna kosa kwa watu akiwemo Maria Sarungi kupinga na kukosoa sera na mipango ya serikali ya Rais Samia kwa njia zozote halali..!
 
Back
Top Bottom