nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 12,106
- 12,916
Hii kitu inafichwa sana sijui kwa faida ya nani. Binadamu ameumbwa ili kuishi milele. Ukifa unazaliwa tena.
1. Kuna ushahidi India mwanafunzi aliyekufa kwa ajali ya pikipiki kazaliwa tena ana kumbukumbu ya sehemu aliyoishi.
2. Kuna mcheza sinema wa marekani pia ameshangaza ulimwengu kwa kuwa na kumbukumbu sahihi za maisha yake yaliyopita.
Ndugu msomaji hata mie kumbukumbu hizo ninazo bila shaka kabisa.
Funga kazi ni Anthony Cicoria Huyu bwana alipigwa na radi, na alipoteza uhai wake kwa muda. kwamba aliuona mwili wake ''live'' ukiwa umelala chini na yeye katika hali ya mwili mwingine usio onekana anajiona kasimama pembeni. Baada ya muda aliamua kujaribu kurudi tena katika mwili wake na akafanikiwa. Baada ya siku mbili akasikia sauti ya piano music laini ukamvutia na kuamsha kitu fulani ndani yake kilichopelekea kutafuta piano na kuanza kupiga bila hata ya kufundishwa na mtu yeyote.
Ndugu msomaji zingatia hakuna kifaa kigumu cha muziki kushinda piano. Bwana Tony haya mambo yalimsibu akiwa na umri wa miaka 42. Katika kufanya utafiti wanasayansi wanazidi kugundua vitu vya kuogofya kwamba huyu jamaa kabla ya kuja kwenye ulimwengu huu alikuwa ni mtaalam mzuri wa Piano ndio sababu kwa sasa anaweza kupiga na kuandika note vizuri kiasi kwamba anafanya maonyesho makubwa makubwa.
Cha ajabu zaidi ni uwezo wa kuandika note kila anapolala usiku huamka na kuanza kuandika note zinazomjia kichwani.
Je? wewe hii unaionaje?