sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,406
- 19,375
Ni maada kwa dini zote wakristo na waislamu na wala sitegemei wachangiaji kuanzisha malumbano
Hakika Mungu anatupenda, Mungu baba wa mababa, mfalme wa wafalme, mungu wa miungu, alfa na omega, mwenye ufalme, utakatifu na nguvu milele na kokote ulimwenguni.
Nina miaka 28, kwa kipindi kilichopita niliitwa tu fulani ni muumini dini flani kwa maneno tu lakini mimi sikuwa na muda kabisa na Mungu mwenye nguvu.
Nilienda kwenye nyumba za mungu kumuabudu ili tu basi nionekane kwamba ni muumini au baada ya kusutwa sana sijaenda siku nyingi.
Nililala kama gunia, wala sikumuomba mungu na pale nilipoomba basi tu ni kwa sababu tu nilitaka pasipo kujua nilichoomba wala kujua niliyemuomba maana sikuwa na muda kumjua Mungu kupitia vitabu vyake.
Nilipotea sana, nilifanya vitu kwankufata mkumbo pasipo kujua ni dhambi, Nilitekeleza matamanio ya mwili ili nifurahi kama kula sana chakula nilipokipenda hasa nyama, kulala sana weekend, kuustarehesha mwili wangu kupitia ngono kwa wanawake wasio wangu katika ndoa, n.k.
Nilikuwa mtu wa visasi niliamini ya kwamba ni ubwege kumuacha aliekukosea, Uongo ulipoweza kunikamilishia nachotaka ulitumika, Kumtusi mtu hata nilioma kawaida tu, Kuna rafiki zangu wa kike wameolewa ila bado nlikuwa nikiwatamani wanistareheshe, Pesa ilinipofua nlifanya vingi vyenye chembe chembe za dhambi ili niipate, Kusaidia watu kwakweli nlikua naona upuuzi, nk
Nilijikuta bila kujijua nikifanya yaliyompendeza shatani zaidi kuliko Mungu, Nilidhani dunia hii inanizungukia mimi katika maisha yanayonihusu pasipo kumwabudu Mungu.
Lakini sasa baada ya kupatwa na matatizo mazit, hakika nilianza kujaribu kuyatatua kwa njia za wanadamu kwa tiba asili hizi lakini bado yaliendelea.
Ndipo ilipobidi nijikabidhi kwa Mungu maana Mungu ni Mwema sana yupo kwajili yetu wote, haijalishi umechelewa kwa muda gani lakini yeye atakupokea tu, yeye ni kama Bwana mwenye shamba huwalipa sawa wafanyakazi wote walioanza kufanya kazi asubuhi na walioanza kufanya kazi jioni, wote atawalipa malipo ya siku nzima kwasababu ya wema wake.
Nikaanza kuwa karibu na asieshindwa lolote na hakika matatizo yangu haya yameacha na kukoma kuniandama.
Muhimu kuliko yote nina kiu ya ajabu sana kumjua Mungu kupitia vitabu vyake, Matatizo yameisha ila sijaacha kuwa na Mungu.
Masaa mawili ya kila siku nayatumia kumjua, kumsifu, kumtukuza na kumwabudu Baba wa mababa wote, sijilazimishi maana nimekuta napenda sana kufanya hivi, imekua kama kucheki comedy za joti.
Kwa hakika nilipotea na nikawa uchi kwenye dunia hii yenye baadhi ya watu waovu wanaoweza kukuletea matatizo mengi endapo huna kinga, Kinga zipo nyingi tu lakini kinga hii ya bwana haina janja janja kama upande mwengine ambako kumesheheni wanaojinadi kutatua matatizo na ukaangukia kwa matapeli, Mungu hana masharti ya kuweza kukudhuru kwamba kinga yake usile maini, usikalie kinu, n.k Kinga ya bwana ni bure kabisa na masharti yake hayatakuharibia maisha bali kukupa utukufu zaidi.
Hakika nilipotea ila kwa upendo wa mungu, hata kondoo wake moja niliepotea nina thamani na hivyo kaniokoa.
Nakushukuru sana Mungu wangu,