Andiko lako refu, ambalo baadae umelifanya kuwa kama maandiko ya Mwashamba na ho wengine limekosa hitimisho.No offence hii ni perception ya jamii ya watanzania kuanzia mama yetu shuka chini hadi kwa machawa wa level za chini kbs kama hapa nilipo cholesamvula.
Kwa hiyo jaribu sasa kukamilisha huo utafiti wako na ueleze inakuwaje "Dude" hilo, ambalo ni CHADEMA; bado halitafua dafu mbele za hao mahasimu wao wakuu.
Weka ushabiki pembeni, wewe eleza tu kwa maoni yako kwa nini "dude" hili linaendelea kuminywa. Achana na hizo habari za mapolisi, kwani hakuna polisi anayemzidi polisi mkuu, ambaye ni hao watu ulio wazungumzia kwenye hilo andiko lako.
Kwa nini CHADEMA hafurukuti, na dalili tayari zimeanza kujionyesha kuwa anaanza kulazwa chali hata kabla ya kipenga.