Angekuwa Mzungu ndiyo anajibu huyo ujumbe basi angeandika kwa kiswahili au hata angetafuta Mkalimani lakini kamwe asingeweza kuchanganya lugha kama ulivyofanya, Ushahidi mwingine wa kuwa na akili ndogo!
Sasa ni kwanini wazungu wanaojua Kiswahili kama Mapadri huwa hawachanganyi Lugha yaani Kiswahili na Kiingereza? Lakini Padri wa Kiafrika Mweusi atachanganya Lugha Kiswahili na Kiingereza?
Nani kakuambia mapdri wazungu wanajua kiingereza??
Kuchanganya lugha ni kipimo cha IQ ya mtu???? Inabidi nikubaliane na wewe kwa kuwa ndio mtazamo wako na uelewa wako unapoishia. Ungejikita kwenye content ungenufaika zaidi
Haya ni maonyesho yaliyoandaliwa na Wazungu (Umoja Wa Mataifa) kuhusu kile kilichotokea huko Ulaya wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia! Maonyesho hayo yalihusu hasa mauaji ya Wayahudi huko Ulaya!
Kilichonigusa hasa na kunifanya mpaka niandike hapa ni jinsi Wazungu walivyofanya haya maandalizi, kwanza aina ya wanafunzi waliokuja ni wa kutoka Shule za kawaida kabisa za Serikali za kata yaani Mtz wa kikawaida, lkn kama hii shughuli ingeandaliwa na Serikali yetu (sisi Watz weusi) basi Wanafunzi ambao wangepata fursa hii wangetoka Shule za binafsi kama Al Muntazir, International school, St Marys n.k yaani shule za Watoto wa kidosi!
Pili kilichonivutia zaidi kuhusu haya maandalizi yaliyofanywa ni Wazungu ni Lugha iliyotumika, Wazungu wameamua kutumia Lugha ya Kiswahili lkn kama hii ingefanywa na Mtz Mdiaspora kama John Mashaka basi lazima wangeandika kwa Kiingereza ingawaje mlengwa ni Mtz wa kawaida!
Hii imenifundisha moja ya kwamba Wazungu ni kweli kabisa wana akili sana kuliko sisi!
I don't get your point at all!
Ni rahisi kwa wao sababu wanajifunza kiswahili ukubwani, waafika (Tz) tunatoka na huo mfumo toka udogoni!!
Pia binafsi sioni tatizo la kuchanganya lugha wakati wa kuongea.
Pia lugha yetu bado haijitoshelezi baadhi ya maneno, hivyo tunaazima maneno mengi kuongeza msisitizo!
Hata mimi nilikuwa naamini hivyo siku zote lakini pia kuna UKWELI ambao sasa nashindwa kuulezea kwa mfano hili la Lugha, ni kwa nini Mtz anayetaka kufikisha Ujumbe kwa Watz wenzake anatumia lugha ya Kiingereza wakati Mzungu, Mchina, Muhindi wakitaka kufikisha Ujumbe kwa Watz hutumia Lugha ya Kiswahili?
Kwa hali ya kawaida ungetegemea ya kwamba huyu Mtz aweze kutumia Kiswahili zaidi kwa maana anaelewa ya kwamba watu wake wengi wanaelewa Kiswahili zaidi kuliko Kiingereza sasa hiyo tofauti ndiyo nashindwa kuilezea kwa ni sijawahi kuona Mzungu, Mchina Muirani, Mwarabu akifanya hivi isipokuwa sisi tu, tena Waafrika weusi hata Waafrika wenzetu wa Kaskazini hawafanyi hivi, sasa ni kwa nini?
Ni mazingira tu Je ni kwanini sisi hapa kwenye mtandao tunafikiria tofauti na viongozi wetu ni mazingira sio rangi wala nini. Hapa Marekani unajua kwamba Native African ni most educated group na wenye degree ni zaidi ya 60% kuzidi hata Asian! hivyo ni mazingira. Wengi wetu tumekuja nchi za watu bila kitu sasa kama tungekuwa wajinga mbona tunaajiri wazungu sasa wakati tumekuja na mabegi tu kwenye nchi yao!!