Je, tuko tayari kumuomba Mungu atufundisha jinsi ya kuwa na upendo kama ule wake kwa sababu tukipenda kama vile Mungu anavyopenda tutawapenda wengine hata kama hatupati faida yoyote.
Sasa basi kuna msichana tulimaliza wote o-level miaka ya nyuma kidogo nilikuwa namkubali sana ila alinipiga chini, sasa amerudi na ana mtoto anadai ananipenda!
Naomba ushauri wakuu.
Kama wewe ni kijana haujaoa na haujawahi kuoa, hilo swali haukustahili hata kulileta humu, kwa sababu nyuzi na mifano mingi sana ilikwishakutolewa na members humu kuwa kijana 'fresh' kama wewe haustahili kujibebesha misalaba isiyokuhusu.
Kimapenzi, wanawake huja kuwagawa wanaume magrupu matatu katika uhai wao wa kimapenzi na huwa'rank' kutokana na magrupu hayo.
1: ni mwanaume aliyemtoa bikira yake: huyo ndiyo mwanaume boss kwenu nyote mtakaofuatia, yeye hana maneno ya kutongozea, kama mfano wa nyumba kujenga alishaijenga kuanzia kufyeka uwanja na kujenga msingi, muda wowote akitaka anaingia ama kutoka, hahojiwi na mtu, ni yake.
2: ni mwanaume aliyezaa naye mtoto ama watoto:
Huyu ni mwanaume ambaye hukimbiwa akikosa kauli thabiti mdomoni mwake pamoja na matunzo kwa ajili ya ulofa.
Lakini pamoja na kukimbiwa na mwanamke huyo akapata neno la kubembeleza, nikuhakikishie siku yoyote atapashiwa kiporo na kula hata kama wewe umemuoa kwa gharama gani ya mahari, utake usitake.
Visingizio vya kuona watoto kipumbaf pumbaf ama mbinu nyinginezo hutumika kama passport ya kufanyia unyambilisi huo.
3: mlishi: huyo sasa ni wewe: mwanaume mwenye heshima zake aliyekubali kuyabeba majukumu ya kumuoa mwanamke huyo na kumtunza na kumheshimisha katika jamii.
Umempenda na kasoro zake, aidha za kuzaa akiwa kwao ama unawafahamu dhahiri ma hawara zake, lakini kwa upendo wa dhati, umeamua kuipindua meza, leo kawa mkeo.
Wewe hautazingatiwa kimapenzi kama hao ma senior zako #1 pamoja na #2, maana wakimtaka akiwa katika himaya yako, watampata tu kwa sababu nao ni mke wao pia.
Kijana mifano ni mingi ya kukutolea kama darasa, lakini itoshe kusema tu kuwa mapenzi hayana darasa kwa sababu yanahusisha moyo na siyo akili.
Moyo ukishapenda, akili hujikuta imeshindwa nguvu zake za kupinga.
Sisi wazee tunapinga kwa nguvu zetu zote kabisa kuruhusu vijana kuzianza ndoa zao mpya kwa najukumu yasiyowahusu.
Hivyo tunashauri: tafuteni wasichana wa rika zenu wenye maadili mema katika jamii zenu muoe, kuanza maisha na msichana wa rika lako asiye na mawaa huwa ni faraja kubwa sana kuliko kuanza maisha na mwanamke aliyekuzidi sana mitazamo hasa ya kimapenzi.
'Maadili mema' tunayoyaongelea ni pamoja na kuangalia dosari nilizozitaja hapo juu pamoja na mambo mengineyo mengi yanayohusu nasaba yake pamoja na makuzi na malezi.