Ushauri: Amejifungua lakini hataki niwaone watoto wangu. Nimshtaki?

Ww jamaa,,,, unatia hasira ? Mbona unakuwa bwege ? Una uhakika hao watoto ni wako ? Eti kajifungua wiki iliyopita, watoto wanafanana na watu wa kwenu,,,, huyo mjanja,,,watoto sio wako, na kuna njemba inampa huduma kutoka ujauzito mpaka leba na hatimae uzazi! Kaa mbali nae kabisa,,,,, !
 
Kaka yangu, kwanza pole sana kwa hali unayopitia. Najua inavyoweza kuwa ngumu, hasa kama unaamini kabisa kwamba hao watoto ni wako na unataka kuwajua na kuwapa majina.

Kwanza, ni muhimu utulize akili na usichukue maamuzi kwa hasira au maumivu. Kama kweli unataka kujua ukweli kuhusu watoto hao, basi njia bora ni kupendekeza kufanya DNA test ili kuthibitisha kama kweli ni wako. Hii itakusaidia kuwa na uhakika kabisa badala ya kuhisi tu kutokana na kufanana.

Kuhusu kutotaka kukuonyesha watoto au kukupa nafasi ya kuwajua, inawezekana kuna mambo yanayomfanya asione hilo kama jambo sahihi kwa sasa—labda hasira, maumivu, au hata ushawishi wa familia yake. Hata hivyo, kama wewe ni baba wa watoto hao, una haki ya kuwajua na kuwa sehemu ya maisha yao.

Njia bora ni kutafuta mjomba, shangazi, au mtu wa kati kutoka upande wake ambaye unaweza kuzungumza naye ili kusaidia kusuluhisha hili bila ugomvi. Kama hakuna mwafaka, unaweza pia kutumia njia za kisheria kama unajua anapoishi, ili kudai haki yako kama mzazi.

Pia, hakikisha unafikiria kwa mapana—je, uko tayari kuchukua majukumu ya kuwa baba kwao? Kama jibu ni ndiyo, basi fanya kila linalowezekana kwa njia ya busara na hekima ili kuhakikisha unakuwa sehemu ya maisha yao.

Mwishowe, usikubali hasira au maumivu ya zamani yakuzuie kufanya kilicho sahihi. Kama kweli unajali watoto hao, tafuta njia za kuwajua, lakini kwa amani na busara. Nakutakia kila la heri kat
ika hili.
 
Bro umeongea points sana kiukweli nashukuru sana kwa ushauri huu bingwa sana

Mungu akuzidishie sana
 
Hao watoto siyo wako mkuu... Kipindi ana mimba alikuwa anat**bwa na jamaa mwingine, Alafu kiurahisi rahisi tu useme watoto ni wako..????

Acha uzezeta kijana
 
Yaani dalili zote huzioni kwa kile kinachoendelea!! Juzijuzi hapo kuna mwenzio kajiondoa uhai huko Iringa kwa michezomichezo ya mapenzi na kuleta viumbe duniani kwa style ya mkanganyiko kama huyo mwenzako, yeye alikuwa anahudumia kabisa, kilichomtokea hakuweza kuhimili nafsini mwake!
 
Amekudanganya huyo na anajua anachotaka kukifanyia ila wewe umepagawa kisa umesikia mapacha
 
Kwanini alituma picha kwa mwanamme asitemtambuwa kuwa baba watoto wake?, tena hawala yake wa zamani?
 
Hapo umrpigwa kaka kaa kimya tafuta watoto wasiokupa stress kunamtego hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…