Ushauri: Ana division four ya 29, akasomee nini?

Wakuu habarini.

Nina mdogo wangu kamaliza form four mwaka jana, amepata div four 29

Naombeni ushauri anaweza kwenda vyuo vya kati vinavyotoa certificate?
Au ni chuo gani kitaendana na ufaulu wake

Ana Hist D, kiswah D, Bio D, Chem D, Geo D, Phy F, Engl F, Math F

Jinsia ni wakike

Ahsanteni
Nafikiri tufikirie kufanyika kazi ushauri wa mtunga sera fulani,kuwa boda au mafunzo ya wizi ili kutengeneza ajira iwe sehemu rasmi ya sera na mafunzo ili kuendana na ushindani wa kileo,watu wanavuna hela kwa ajili ya mataifa yao kidigitali.Ni mawazo tu jamani sijakuwa na nia mbaya kwa mleta mada wala yeyote.Naomba nieleweke kwa mtazamo huo tu na sii vinginevyo.
 
Upo sahihi, ila malengo yake bado hajachoka anataka aendelee kusoma
Kwa umri wake anaweza akawa anaona kama kusoma ndio option pekee iliyopo hasa kwasababu anaona wenzie wote nao wanasoma. Ila nyie mnaweza kumsaidia kumuonyesha kuwa kuna option zingine nzuri tuu
 
Nafikiri tufikirie kufanyika kazi ushauri wa mtunga sera fulani,kuwa boda au mafunzo ya wizi ili kutengeneza ajira iwe sehemu rasmi ya sera na mafunzo ili kuendana na ushindani wa kileo,watu wanavuna hela kwa ajili ya mataifa yao kidigitali.Ni mawazo tu jamani sijakuwa na nia mbaya kwa mleta mada wala yeyote.Naomba nieleweke kwa mtazamo huo tu na sii vinginevyo.
Kwamba akawe mwizi wa mtandaoni kama hushpapy?
 
Kwa umri wake anaweza akawa anaona kama kusoma ndio option pekee iliyopo hasa kwasababu anaona wenzie wote nao wanasoma. Ila nyie mnaweza kumsaidia kumuonyesha kuwa kuna option zingine nzuri tuu
Mkuu ni sahihi
Ila acha tufuate mawazo yake.
 
Kwamba akawe mwizi wa mtandaoni kama hushpapy?
Ajira imekuwa majanga,hivyo zitengenezwe fursa tunazoziweza kwa mazingira yetu na watunga sera tulionao kwa wakati wa sasa,tunatambalia ilipo fursa.
 
Japo ajira imekua majanga, ila kwa hili wazo lako big No.
 
Back
Top Bottom