Ushauri: Anasema nimezidisha usela, niachane naye?

Ushauri: Anasema nimezidisha usela, niachane naye?

Kiparamoto

Senior Member
Joined
Oct 1, 2015
Posts
100
Reaction score
100
Wakuu,

Mimi ni kijana wa makamo, on my early 30s, sina familia (mke & mtoto), vipaumbele vyangu kwenye maisha ni kujitoa kwenye dimbwi la umasikini uliokithiri kwenye familia zetu hizi za kiswahili, ukijumlisha nilishawahi kupigwa matukio huko nyuma na wachumba kwa kukosa vijisenti hata vya mboga basi focus yangu kubwa kwa mda mrefu imekuwa ni kufanya kazi kwa bidii na kutafuta financial freedom.

It's been a while, over 5+ years sijakuwa kwenye mahusiano serious, hata mabinti ninaokutana nao huwa nawaambia toka mwanzo kuwa sina mpango wa kufanya mahusiano nao ya serious, just having some fun na kuzagamuana tu, wengi wamekuwa wakielewa hilo.

Hivi karibuni nimejikuta kwenye penzi zito na mtoto wa "kiburushi" toka kusini (anaishi dar) nimekuwa nae kwa kipindi Cha miezi kadhaa naona anakila sifa za kumfanya awe wife, shida inakuja moja, huyu binti amekuwa akilalamika mno kuwa nimezidisha Usela sana kwake, hata ninavyomtreat ni kama msela mwenzangu, kuanzia kumtext, na hata mazungumzo yetu, anadai anataka ajifeel kama mtoto wa kike/mpenzi na si vinginevyo, anasema sipo romantic kwake kitu ambacho mimi kinanipa wakati mgumu coz ninavyoishi ndio maisha yangu huko kuwa romantic anavyotaka yeye mimi najionea shida, nampa mahitaji yake yote, namfanya rafiki lakini changamoto ndio hiyo binti anataka mapenzi ya kwenye sinema na luninga mimi sijazoea ukizingatia nina mda mrefu sipo kwenye mahusiano.

Mnisaidie ndugu zangu msela Mimi nisimpoteze mrembo huyu.
 
Huenda umezidisha usela kweli.
Si ajabu hata majina ya kimahaba humuiti, zaidi ya oya, niaje, vp apo, inakuaje mzee, kama kawa nk...

Ni kitu kidogo ila kwa wanawake ni kikubwa.
Kama utaendelea na hiyo tabia, wazee wa kimasihara wapo kwa ajili ya kusolve matatizo madogo madogo kama hayo.
 
Jiandae kwa yoyote. Umeisha kisela sela sana ndomaana unaona kama ndo ulivyo.
Legeza kwa mpenzi wako😂😂 vinginevyo utakuja na Uzi mwingine wanawake hawaridhiki na bla blaaa..Niko pale nakusubiri.
Not usela kivile ni vile sisi wengine tumezoea kuwa straight forward on each and everything sasa hawa wenzetu wanataka diplomasia na drama kwenye kila kitu.
 
Huenda umezidisha usela kweli.
Si ajabu hata majina ya kimahaba humuiti, zaidi ya oya, niaje, vp apo, inakuaje mzee, kama kawa nk...

Ni kitu kidogo ila kwa wanawake ni kikubwa.
Kama utaendelea na hiyo tabia, wazee wa kimasihara wapo kwa ajili ya kusolve matatizo madogo madogo kama hayo.
😀😀 Kwenye hili ni kweli amekuwa akilalamika mara nyingi nikiongea nae lazima nimuite "mwanangu", which I thought it's normal and friendly way ila nimekuja kugundua kuna mda ananuna kabisa, for really?
 
We endelea kua na masela la sivyo huyo manzi atakua anabanduliwa kwa sababu uchwara kama hizo.

Ni mpenzi wako, why umtreat kama msela wako??
Ni sawa na dem wako awe anakuita "shost" sijui udugu na zile sauti zao za kimbeambea kama mwanamke mwenzie, haipendezi na bila shaka hutopenda.

Naamini hilo liko ndani ya uwezo wako ila hupendi, unahisi utajishusha.
 
Kwahiyo mkuu

Unataka usiachwe
Unataka kubadilisha lifestyle yako .

Anayemuhitaji mwenzake ndo anabidi kubadilika ili kuendana na mwenzanke
Well, kwanza I found it very weird mtu kununa kwa kigezo kuwa simtreat in a romantic way, sikuwahi kufikiria mtu mzima anaweza kuraise such a matter ukizingatia nafanya vile a man anapaswa kumfanyia mpenzi wake Sasa hayo anayoyataka yeye mimi naona it's strange, but may it's true I need sometimes kujiadjust anavyotaka yeye.
 
We endelea kua na masela la sivyo huyo manzi atakua anabanduliwa kwa sababu uchwara kama hizo.

Ni mpenzi wako, why umtreat kama msela wako??
Ni sawa na dem wako awe anakuita "shost" sijui udugu na zile sauti zao za kimbeambea kama mwanamke mwenzie, haipendezi na bila shaka hutopenda.

Naamini hilo liko ndani ya uwezo wako ila hupendi, unahisi utajishusha.
Daaah sawa mkuu nimekusoma 😀😀
 
Back
Top Bottom