Ushauri: Anataka akafanye kazi za ndani (house girl) Uturuki

Ushauri: Anataka akafanye kazi za ndani (house girl) Uturuki

Mdau jf

Senior Member
Joined
Sep 10, 2020
Posts
182
Reaction score
313
Wasalaam Wana jf

Kuna binamu yangu mkoa X ameniomba ushauri, kwamba amepata mchongo wa kwenda nchini UTURUKI kufanya kazi za ndani.

Nami kwakua sina experience na mambo hayo nikaona ni Bora nilete kwenu mnaweza Kua na ABC's za kumuambia, ili nimfikishie na iwe hiari kwake kwenda ama kutokwenda kutokana na maoni mbalimbali mtayo toa hapa

NAWASILISHA
 
Kazi yyte ambayo elimu sio kigezo cha kupata kazi hio basi itakuwa ya mateso na udhalilishaji kwa nchi za watu,kama hana elimu anaki Bongo apambne ,ila kama amejitoa sadaka, in sha Allah.
 
Kutegemea na bosi atakaempata, hata hapa bongo wwengine safi, wengine mabosi vichefu chefu, kuna binti mmoja alienda uturuki lakini kule wakurdishi wanapojitenga, yeye alibahatika kupata bosi fresh, kaenda karudi freeeeesh.
 
Mwambie ahakikishe serikali inajua ikiwemo balozi yetu iliyopo inajua kuwa yupo nchini humo kwa shughuli gani ili iwe rahisi kusaidiwa ikiwa mambo yatakwenda mrama
 
1. Ahakikishe anaenda kihalali, awe na connection ya ubalozi wa nchi yake.

2. Atumie Agency za ndani ya nchi yetu zilizosajiliwa kuwa kama wasimamizi wake.

3. Asome Kwa makini mkataba wa kazi kabla hajafika huko

4. Asilete uswahili wake kwenye nchi za watu.
Maana huku bongo Wafanyakazi wanawaonea Maboss Kwa kutofuata makubaliano ya Mkataba. Jambo Hilo ndilo hufanya wananyang'anywa passport wawapo huko Nchi za watu.

5. Asiwe mdekaji na tabia za kitoto za uvivu uvivu
 
Mimi Na dada angu yupo uturuki kama house girl mpaka sasa ana nyumba nane Na gari tisa ziko Nyumba ziko dar pia anatarajia kununua ndege yake waache kukutisha mkuu
 
1. Ahakikishe anaenda kihalali, awe na connection ya ubalozi wa nchi yake.

2. Atumie Agency za ndani ya nchi yetu zilizosajiliwa kuwa kama wasimamizi wake.

3. Asome Kwa makini mkataba wa kazi kabla hajafika huko

4. Asilete uswahili wake kwenye nchi za watu.
Maana huku bongo Wafanyakazi wanawaonea Maboss Kwa kutofuata makubaliano ya Mkataba. Jambo Hilo ndilo hufanya wananyang'anywa passport wawapo huko Nchi za watu.

5. Asiwe mdekaji na tabia za kitoto za uvivu uvivu
dah jamiiforum kweli kiboko,, nna manzi yangu soon anaenda oman kikaz sasa alinambia nimpatie ushauri ,,,nmekaa nkafiikiri kuwaza na kuwazua nkaamua njitose JF kwakweli baada ya kuona haya madini nmefurahis sana wacha nkamshauri
 
Back
Top Bottom