Van Pauser
JF-Expert Member
- Mar 21, 2017
- 417
- 420
Habari za asubuhi wapendwa,
Natumaini ni Jumatatu nyingine ambapo kila mmoja anajiandaa kwenda katika majukumu ya ujenzi wa taifa basi na Mungu awe pamoja nanyi.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni kwamba nina mpenzi wangu ambaye nipo nae katika mahusiano si kwa kipind kirefu sana lakini tangu nimekaa nae kwa kipindi hiki kifupi nimegundua mambo mengi sana ambayo yananipa wakati mgumu sana halafu pia anataka nimuoe kwa lazima.
Kwanza; huyu mwanamke ni muongo ambapo amenidanganya vitu vingi ambavyo nimegundua kuwa sio kweli amenidanganya ana dada yake Zanzibar kumbe sio dada yake wa kuzaliwa nae kumbe yule dada alikuwa ni mfanyakazi wa ndani.
Pili; huyu mwanamke ni 'single mother' nimekuja kugundua kuwa ni 'single mother' baada ya kuambiwa na yule boss wake alipokuwa akifanya kazi Zanzibar halafu kwangu anapretend kuwa hana mtoto.
Tatu; huyu mwanamke ana majini.Iko hivi mimi sio mnywaji pombe ila jana wakati natoka kazini nilimkuta yupo na dada mmoja amenitambulisha kuwa ni dada yake lakini mimi sijaamini kwa sababu ameshakuwa ni mwongo sasa baada kuona vile nikaenda kwenye grosary moja jirani nikachukua kinywaji chenye kilevi basi nikarudi nyumbani ile nafika tuu hamwezi kuamini alipandisha majini.
Nne; amekaa kwangu almost week tatu sasa amekuja kwangu binafsi mimi ni msela, sjaoa na nilikuwa sina mpango wa kuoa sasa hataki kuondoka na ananitishia kuniloga, nimemwambia kuwa akafanye anachotaka.
Ushauri wako ni muhimu sana kwangu maana nipo katika wakati mgumu, tafadhalini sana sihitaji matusi wala kebehi.
Asanteni sana na Mungu awatangulie katika njia zenu.