Ushauri: Anataka nimuoe kwa lazima

Ushauri: Anataka nimuoe kwa lazima

Van Pauser

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2017
Posts
417
Reaction score
420
Habari za asubuhi wapendwa,

Natumaini ni Jumatatu nyingine ambapo kila mmoja anajiandaa kwenda katika majukumu ya ujenzi wa taifa basi na Mungu awe pamoja nanyi.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni kwamba nina mpenzi wangu ambaye nipo nae katika mahusiano si kwa kipind kirefu sana lakini tangu nimekaa nae kwa kipindi hiki kifupi nimegundua mambo mengi sana ambayo yananipa wakati mgumu sana halafu pia anataka nimuoe kwa lazima.

Kwanza; huyu mwanamke ni muongo ambapo amenidanganya vitu vingi ambavyo nimegundua kuwa sio kweli amenidanganya ana dada yake Zanzibar kumbe sio dada yake wa kuzaliwa nae kumbe yule dada alikuwa ni mfanyakazi wa ndani.

Pili; huyu mwanamke ni 'single mother' nimekuja kugundua kuwa ni 'single mother' baada ya kuambiwa na yule boss wake alipokuwa akifanya kazi Zanzibar halafu kwangu anapretend kuwa hana mtoto.

Tatu; huyu mwanamke ana majini.Iko hivi mimi sio mnywaji pombe ila jana wakati natoka kazini nilimkuta yupo na dada mmoja amenitambulisha kuwa ni dada yake lakini mimi sijaamini kwa sababu ameshakuwa ni mwongo sasa baada kuona vile nikaenda kwenye grosary moja jirani nikachukua kinywaji chenye kilevi basi nikarudi nyumbani ile nafika tuu hamwezi kuamini alipandisha majini.

Nne; amekaa kwangu almost week tatu sasa amekuja kwangu binafsi mimi ni msela, sjaoa na nilikuwa sina mpango wa kuoa sasa hataki kuondoka na ananitishia kuniloga, nimemwambia kuwa akafanye anachotaka.

Ushauri wako ni muhimu sana kwangu maana nipo katika wakati mgumu, tafadhalini sana sihitaji matusi wala kebehi.

Asanteni sana na Mungu awatangulie katika njia zenu.
 
Apite kushoto hyo asikutishe kukuloga sasa kumbe ni mchaw huoni kashaweka sifa yke mbya mezani hao mm ndo nawatakaga hao anakula mabanzi na ataondka apnde aspende kudadadeki pole sana
 
Mkwara kuhusu kukuloga ila kwa uchunguzi wako Wa awali na ww umeisha kuwa mwanaume Fanya maamuzi ya kiume
 
Usimuogope wewe mtimue. Na Mimi kuna manzi alikua ananilazimisha kumuoa kwa vitisho. Nikamtimua huu mwaka wa 5 hamna chochote.
 
Pole mkuu lakin inaonyesha huyo hafai hata kuwa jiran wewe mweleze uliyoyaona kwake pamoja na uongo wake halafu kila mtu afanye yake kwan ukiendelea nae ipo siku atakuletea bwanake mwengine atakwambia Kakake
 
Mrudie Mungu wako, huyo ni wa kumuondoa kwa maombi si kwa njia nyingine.

Mlivyosex naye na mengine yote mliyofanya pamoja yameshawaunganisha kiroho.
 
Nahisi mwanamke atakuwa mmanyema na wewe ni wa pwani hujazoea mikwara,
Mwite mjumbe mwambie huyu mwanamke amekuvamia kwako na unataka aondoke,
Kumbuka akushika mimba huyo ndio itakuwa tiketi ya kukaa kabisa.
 
Mtelekeze!
Ongea na Mwenye Nyumba mpe hadithi nzima halafu mwambie inakubidi uondoke! Nenda kapange sehemu ya mbali asoijua!
Ila kuna somo la kujifunza hapo, Tubu halafu utulie hadi utakapooa!
 
Pole sana mkuu huyo sio mtu mzuri na inaonekana yupo kimaslahi zaidi cha msingi achana nae. Kama anakutishia maisha na hataki kuondoka wewe funga nyumba yako ondoka, kakae hata kwa washkaji siku kadhaa, ataondoka mwenyewe
 
Kuoa ni hiari na kuridhiana, huyo anavyokulazimisha na kukutishia ni hatari kwa afya na maisha yako.

Unavyomchelewesha hapo kwako ndivyo anazidi kuwa mwenyeji.

Atakwambia nina mimba yako, maana najua wiki tatu zote kama ulitumia kinga ni siku moja tu.
 
Pole sana mkuu huyo sio mtu mzuri na inaonekana yupo kimaslahi zaidi cha msingi achana nae. Kama anakutishia maisha na hataki kuondoka wewe funga nyumba yako ondoka, kakae hata kwa washkaji siku kadhaa, ataondoka mwenyewe
Hello Beingsingle,

Ila akimwacha akaenda kwa washkaji, siku akirudi afanye mpango ahame kabisa. Nyumba weza kuwa imetegwa mabomu ya asili au ya mzungu hiyo. Silaha ni Biblia tu.
 
Hello Beingsingle,

Ila akimwacha akaenda kwa washkaji, siku akirudi afanye mpango ahame kabisa. Nyumba weza kuwa imetegwa mabomu ya asili au ya mzungu hiyo. Silaha ni Biblia tu.
Kweli kabisa yaani akirudi ahame mazima maana huyo manzi anaweza kuja kumfanyia kitu kibaya
 
Asanteni sana na Mungu awatangulie katika njia zenu.
neno hili la baraka unatupa wakati unajua fika uko na mtu ambaye sio mkeo mnagegedana bila ruhusa ya mwenyezi Mungu ahaha umenifurahisha hapa. Haya huyo mchukue tu hamna jinsi hataki kuondoka tuseme ni wako tu.
 
Habari za asubuhi wapendwa..!! Natumaini ni jumatatu nyingine ambapo kila mmoja anajiandaa kwenda katika majukumu ya ujenzi wa taifa basi na Mungu awe pamoja nanyi.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni kwamba nina mpenzi wangu ambaye nipo nae katika mahusiano si kwa kipind kirefu sana lkn tangu nimekaa nae kwa kipind hiki kifupi nmegundua mambo mengi sana ambayo yananipa wkt mgumu sana halafu pia anataka nimwoe kwa lazima..

Kwanza;Huyu mwanamke ni muongo ambapo amenidanganya vitu vingi ambavyo nmegundua kuwa sio kweli amenidanganya ana dada yake Zanzibar kumbe sio dada yake wa kuzaliwa nae kumbe yule Dada alikuwa ni mfanyakazi wa ndani...

Pili;Huyu mwanamke ni single mother nmekuja kugundua kuwa ni single mother baada ya kuambiwa na yule boss wake alipokuwa akifanya kazi Zanzibar halafu kwangu anapretend kuwa hana mtoto...

Tatu;Huyu mwanamke ana majini.. Iko hv mm sio mnywaji pombe ila jana wakati natoka kazini nlimkuta yupo na dada mmoja amenitambulisha kuwa ni dada yake lkn mm cjaamin kwa sabab ameshakuwa ni mwongo ss baada kuona vile nikaenda kwenye grosary moja jirani nikachukua kinywaji chenye kilevi bac nikarudi nyumbani ile nafika tuu hamwezi kuamin alipandisha majini...

Nne;Amekaa kwangu almost week tatu sasa amekuja kwangu binafsi mm ni msela cjaoa na nlikuwa cna mpango wa kuoa ss hataki kuondoka na ananitishia kuniloga nmemwambia kuwa akafanye anachotaka..

Ushauri wako ni muhim sana kwangu maana npo katika wakati mgumu tafadhalini sana sihitaji matusi wala kebehi..!!! Asanteni sana na Mungu awatangulie katika njia zenu.
Simama Imara ahache kumloga aliye mzalisha akuloge wewe ? [emoji1] [emoji1]
HII AWAMU YA TANO TUTAVURUGWA SANA
 
Pole sana mkuu,ila ww ni mwanaume..kwa nini huyo mtoto akutoe jasho????
fanya maamuzi ya kumtoa tuu coz wapo wengi
 
Apite kushoto hyo asikutishe kukuloga sasa kumbe ni mchaw huoni kashaweka sifa yke mbya mezani hao mm ndo nawatakaga hao anakula mabanzi na ataondka apnde aspende kudadadeki pole sana
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom