Ushauri: Anza hata na chumba na sebule. Nyumba kubwa inatesa

Kasema 8-9m ukikiremba sana ndio 15m. Ni kweli ukinogewa kuweka vitu vya gharama unaweza kutumia gharama kubwa kujenga hadi watu wakakushangaa. Kumbuka chumba na sebule mtu anaweka na jiko pia sio chumba na sebule kama police post.
Hata hiyo bado sana sijui wenzangu mnajengaje lakini kwa uhalisia mill9 ni nyingi sana kujenga chumba na sebure tu ni kuchezea pesa

Nimejenga room 3 na kuzunguusha na fensi na geti la kisasa kabisa bajeti nmetumia mil13 japo sijaweka vioo bado nimeweka nyavu kwanza
 
Kabla hujawaza kujenga huwa hujiulizi maswali je nyumba inagharimu kiasi gani?
Una 20m unaanza ujenzi wa nyumba mpaka inaisha inakugharimu 70m sasa ya nini kuhangaika kama sio wehu
Hesabu zinatakiwa na kujipanga kama una 70m anza mpaka kuisha huna napo fuata ushauri huu wa mleta mada
 
Aisee, nilikuwa najiona bingwa wa ujenzi nafuu, ila wewe umenizidi.
 
📖MHADHARA WA 16:
Baada ya kununua kiwanja......
Ukibahatika tena kupata vihela kidogo ni bora kuanza kujenga CHUMBA + SEBULE + CHOO. Kama hela zako ni za msimu au hela za kulenga kwa manati usijenge nyumba kubwa, kwasababu inaweza kukutesa kwenye harakati za kuimaliza. Wabongo wana msemo wao wanasema; "Ujenzi wa nyumba unaanza kutesa wakati wa kuanza matumizi ya lugha ya kiingereza" - Yaani wanamaanisha kuanza harakati za kupaua hadi kumaliza.

Wengi wanateswa sana na ujenzi wa nyumba kubwa unakuta pesa inakatika katikati ya ujenzi, hatimaye jengo linabaki kuwa pagala kwa zaidi ya miaka 5 hadi 10. Ujenzi wa nyumba kubwa unatesa hasa kwa wale wanaotumia mikopo ya benki kwa ajili ya kujenga. Ujenzi wa "kuvuta pumzi" ni mgumu sana kwasababu kila pumzi unayovuta ukiipata inakutana na ada za watoto, ugonjwa, kodi ya nyumba, huduma za ndani, n.k.

Baadhi ya mafundi wa nyumba ambao wanayajua maisha ya kubangaiza huwa wanawashauri watu kuanza kujenga nyumba ya nyuma (CHUMBA + SEBULE + CHOO) - Ni nadra sana kukutana na mafundi watakaokushauri hivyo. Ukizingatia ushauri wao utafanikiwa kuhamia kwako mapema, nyumba ya mbele (nyumba kubwa) utaijenga taratibu ukiwa papo hapo kwako.

RIGHT MARKER,
Dar es salaam,
24/09/2024.
Uko sahihi kwa mtazamo wa mtu asiye na familia na asiye na fanicha nyingi
 
Kabla hujawaza kujenga huwa hujiulizi maswali je nyumba inagharimu kiasi gani?
Una 20m unaanza ujenzi wa nyumba mpaka inaisha inakugharimu 70m sasa ya nini kuhangaika kama sio wehu
Hesabu zinatakiwa na kujipanga kama una 70m anza mpaka kuisha huna napo fuata ushauri huu wa mleta mada
Mkuu Bongo sio UK. Huku unaweza kujenga nyumba ya 50m bila account kufikisha 10m mwaka mzima. Unajenga kwa kudunduliza. Ukipata 1m unaenda site,ukipata 500k unaenda site hadi nyumba inaisha hata ikichukua miaka mitano.
 
Sina muda mkuu na wala sikubishii kwamba haiwezekani. Ujenzi una ambo mengi kila mtu ana style yake na malipo yake.
Ndio maana nikasema hesabu za humu ni kubwa sana ukizifuata unaweza usianze hata msingi

Mfano tu mtu anaweza kusema msingi tu katumia mil4-7 wakati msingi wa kawaida eneo lililo flat hata 1mil haiiishi

But ni mawazo tu hatubishani mkuu
 
Za kuambiwa changanya na zako usifuate yote ya humu mkuu
 
📖MHADHARA WA 16:
Baada ya kununua kiwanja......
Ukibahatika tena kupata vihela kidogo ni bora kuanza kujenga CHUMBA + SEBULE + CHOO. Kama hela zako ni za msimu au hela za kulenga kwa manati usijenge nyumba kubwa, kwasababu inaweza kukutesa kwenye harakati za kuimaliza. Wabongo wana msemo wao wanasema; "Ujenzi wa nyumba unaanza kutesa wakati wa kuanza matumizi ya lugha ya kiingereza" - Yaani wanamaanisha kuanza harakati za kupaua hadi kumaliza.

Wengi wanateswa sana na ujenzi wa nyumba kubwa unakuta pesa inakatika katikati ya ujenzi, hatimaye jengo linabaki kuwa pagala kwa zaidi ya miaka 5 hadi 10. Ujenzi wa nyumba kubwa unatesa hasa kwa wale wanaotumia mikopo ya benki kwa ajili ya kujenga. Ujenzi wa "kuvuta pumzi" ni mgumu sana kwasababu kila pumzi unayovuta ukiipata inakutana na ada za watoto, ugonjwa, kodi ya nyumba, huduma za ndani, n.k.

Baadhi ya mafundi wa nyumba ambao wanayajua maisha ya kubangaiza huwa wanawashauri watu kuanza kujenga nyumba ya nyuma (CHUMBA + SEBULE + CHOO) - Ni nadra sana kukutana na mafundi watakaokushauri hivyo. Ukizingatia ushauri wao utafanikiwa kuhamia kwako mapema, nyumba ya mbele (nyumba kubwa) utaijenga taratibu ukiwa papo hapo kwako.

RIGHT MARKER,
Dar es salaam,
24/09/2024.
Andiko zuri sana kwa wenye mazingatio, basi wafate ushauri 👆👆👆:EZclap::EZclap::EZclap:
 
Bahati mbaya mtu akisema ajenge hiyo ya uwani kwanza then aje kujenga nyumba ya ndoto zake mpaka anakuja kuzeeka atakachokuwa amefanikiwa ni kununua tofali anazipanga nje kwake zikinyeshewa mvua na kubadilika rangi lakini hakuna cha kuanza ujenzi tena wala nini.

Hili lieleweke tu kwamba kila mtu atamiliki alichopangiwa wewe anza ujenzi kama ni nyumba kubwa au ndogo utakapoishia ni hapo hapo muhimu anza ujenzi lakini kama unapumua na bado unapambana utaishi kwenye nyumba uliyoitaka.
Wazo lakinidhamu kabisa ili

Kunywa soda apo
 
Kama mtu fedha anayo kwanini aanze na chumba na sebule? Ujenzi ni plan ya mjengaji kutegemea ana malengo gani, hayo mambo ya kutishana sio mazuri kabisa
 
Ndio maana nikasema hesabu za humu ni kubwa sana ukizifuata unaweza usianze hata msingi

Mfano tu mtu anaweza kusema msingi tu katumia mil4-7 wakati msingi wa kawaida eneo lililo flat hata 1mil haiiishi

But ni mawazo tu hatubishani mkuu
Shukran mkuu kwa mchango wako. Pia km una uzoefu naomba unipe rough estimation gharama za msingi wa nyumba yenye sebule 10*10ft bedroom 8*8ft kijiko simple 5*3ft, choo 3*5ft. Nashkuru 🙏
 
Msingi unategemea na slope ya eneo either flat au muinuko

Kingine jenga vitatu mkuu gharama hazitofautiani sana na hiyo unayotaka kuanza nayo utajikuta umetumia pesa nyingi kwa kajumba kadogo wakati ungeweza kuongeza kidogo ukajenga ya vyumba vitatu ni ushauri tu
 
Back
Top Bottom