Wadau mi ni mtu mzima wa miaka 29,
Kuna binti nilikuwa na mahusiano nae mpaka tukaanza kuishi pamoja.
Kabla ya kuishi pamoja nilimpa ujauzito kwao wakaja kujua, binti alifokewa na kwao walimkataa asiende baada ya kumaliza chuo, Nilimhudumia ujauzito Lakini Mungu akasaidia kwao wakarudisha moyo nyuma anapokaribia kujifungua ikabidi aende kwao (ukweni) kila kitu nilitoa mpaka anajifungua.
Alipojifungua zikapita wiki mbili, nashangaa napigiwa simu na baba yangu mzazi nyumbani kuna tatizo ikabidi niende. Nafika nyumbani mzee ananiuliza kuna binti nilimpa ujauzito? nikamjibu ndio bila kufahamu amejuaje.
Nilipokubali kwa mzee hapo hapo akasema subiri, akapiga simu kumbe anaempigia ni baba mkwe, Wakaombana msamaha yani kumbe baba mkwe alimpigia simu mzee kumpa taarifa, mzee aliposema hafahamu ngoja nimulize kijana wangu baba mkwe alikasirika wakakosana mana hata mzee wangu nae ni mtata.
Sasa baba mkwe alipomaliza kuongea na mzee wangu akaomba aongee na mimi. Alichoniuliza ni kuwa naenda lini kumuona mtoto, nikamwambia ngoja nijipange nitakuja.
Akamind akasema sitaki chochote kutoka kwako kesho nakuchinjia jogoo uje umuone mwanao kama hauna nauli nakutumia. Nikamwambia basi nakuja kesho akakazia sana kesho nakuandalia jogoo njoo umwone mwanao sitaki chochote toka kwako nikasema sawa.
Kesho yake nikaenda na mzee mmoja mtu mzima, nilipokelewa vizuri nikamwona mwanangu na hatimae nikaaga nikarudi.
Ikapita wiki moja baba mkwe akanipigia simu akasema nikamchukue mtoto na mke wangu hataki kuishi nao wakati mimi nipo, nikasema sawa akanielekeza na utaratibu utakaofuata ndugu wakikaa wapange mahari. Ndugu walikaa nakupanga mahari, na nikatumiwa pdf ya mahari pamoja na faini ya kumpa binti yao mimba bila ruhusa yao.
Nikamwambia mzee basi ngoja nijipange mana bado najitafuta, ukapita mwezi wa pili sijaend kuto mahari, nikapigiwa tena simu nikamchukue mtoto na mke wangu, ikabidi niende wakanikabidhi na kutupa baraka hivyo tukaanza maisha ya ndoa.
Tumeishi miaka mitatu, changamoto tunapitia nakuzikabili, tulikuwa tunakoseana kiukweli lakini mambo madogo madogo sio ya usaliti.
lakini mwishoni ukatokea ugomvi mimi na mke wangu tatizo lilianzia kwenye simu, Mana kwenye simu yake kuna mtu alikuwa akichati nae mpaka wanakaribishana chakula usiku wakati mi nipo nae simu anacheza mtoto magemu kwahiyo nasoma sms halafu nakaa kimya.
Kuna siku nikashika simu yake nikarudi kwenye zile chat nakuta kafuta, nikambana akasema bahati mbaya, nikasema sawa akasema yule huwa ananua mzigo kwake ni huwaga wanataniana.
Mara ya mwisho sasa narudi nyumbani namkuta kalala na hajapika, nikamwambia naomba simu yako akakataa na sio kawaida nikajua kuna kitu anaficha, nikaforce anipe hadi akanipiga na simu mdomoni nikapasuka kwa ndani.
Ilibidi nimchape makofi, tukalala usiku tumedinyana fresh asubuhi akaondoka nikajua anaenda kwenye biashara ambayo nilimpa mtaji mwenyewe, baada ya kuona kazi aliyoajiriwa haina maslahi na inabidi redioni aende vipindi hadi vya usiku.
Sasa baadae mida yake ya kurudi nakuta hajarudi toka kazini kwake, nilipiga simu zaidi ya mara 50 hakupokea ila kuna muda ilikuwa busy nikajua ni makusudi.
Kumbe kaenda nyumbani kwetu sio kwao, na wakati huo napigiwa simu na ndugu zangu wakilalamika mimi kumpiga mke wangu wanataka nimuombe msamaha nikawa nimekaza siwezi jishusha kwa kiasi hicho, kwasabu japo nilimpiga pia alikuwa na makosa, na sio scale yakupiga kama napiga kweli bali nikumkumbusha kurudi kwenye mstari.
Nikapigiwa simu na shangazi yangu, kumbe mke wangu bwana siku ya ugomvi ambapo naforce anipe simu, alikuwa katunza screenshot zangu ambazo nilikuwa nawasiliana na eX wangu instagram na huyo X yupo sehemu ambayo siku sio nyingi inabidi niende kikazi na hata txt hazikuwa mbaya kiasi hicho na mambo niliyokuwa nachat nae ni kuhusu kazi.
Sasa wife alikuwa hataki kunipa simu akijua nitafuta ushahidi wa kuwapa ndugu zangu wakati mi nawaza yeye ananificha alichokuwa anachat na nani anaechati nae, Wife aliscreenshot txt ambazo huyo x tumechat hata kabla ya mimi na yeye wife kuwa na mahusiano hakuangalia tarehe, na kuwaonyesha ndugu zangu.
Ikabidi nimpigie simu mama yake kuwa huku kilitokea hivi na hivi alinisema sana kwakuwa nilimpiga wife lakini akasisitiza tuyamalize.
Niliwaelekeza ndugu zangu kwasabu hata account yangu ya instagram sikulogout kwenye simu yake na hata eX nilikuwa nawasiliana nae Mambo ya biashara kwasabu anaconnection ninakoenda, na ningesema nilogout angeona ndio sababu zaidi.
Lakini hii leo narudi kwangu kwasababu funguo anajua napoweka nakuta wife kabeba kila kitu kasepa, alishindwa beba sofa tu na kitanda. Hajaacha hata glass ya kunywea maji hivi nanywea kwenye ndoo.
Ikabidi nichukue Mmbwa wangu (Malinois) nifwatilie alimopita wakati anasomba vitu, nimekuja kuta kapanga chumba sio mbali na ninapoishi, ikabidi nirudi na Malinois mpaka kwangu.
Nimejaribu kupiga simu hapokei, nilipomtumia sms nataka niongee na mwanangu kanipigia nimeongea na mwanangu.
Nashindwa kuelewa chakufanya nahitaji ushauri wenu, na mwanangu ni wakiume siwezi kubali alelewe na mama yake mana kuna tabia huwa naona hawezi mshape bila mimi na kama mnavyoelewa watoto wakiume kulea ni kazi kuliko wa kike kwa dunia hii ya sasa.
Na sijapiga simu kwao kabisa mpaka sasa ila ndugu zangu nimewaambia.
Ushauri please