Ushauri: Baada ya ugomvi Mke Wangu kabeba kila kitu ndani, kaondoka na Mwanangu wa Miaka 2.5

Ukweni nimeongea nao leo nao walikuwa hawajui, ila wameniambia itakuwa ni hasira zikiisha atarudi, japo mtoto ndio ananiumiza sana akili.
 
Ok mkuu thanks ila Note ya mwisho sijaelewa yani anipe ABC kivipi mana sidhani kama ndio ninachofikiria.
 
Ni kweli dogo kukaa na mama yake pekee utampoteza, pia kama ukimchukua ukamleta home badae ukao mwanamke mwingine utampoteza pia, kazi ni kwako kusuka au kunyoa...
 
Kama ME mwenzio nakushauri kwamba kwa mambo yalivyo sasa, wewe tulia tu. Zingatia zaidi afya na usalama wako na wa mwanao. Mtafute na ongea naye kimkakati - ili mradi akuwezeshe kuwasiliana na kumhudumia mwanao. Kama anaonekana yupo tayari kwa maridhiano, na bado unampenda, basi jaribu kupatana naye muendeleze ndoa yenu isiyo rasmi. Kama ni dhahiri hataki. Usimbembeleze. Endelea na maisha yako.
 
Watoto wa kiume mara nyingi huwa tunaigi kwa wazee wetu kama mzee wako ni mtata it means hayumbishwi na maza kwanini wewe usiwe mtata hata kwa kiasi tu?
Mkuu utata wa mzee sijawahi ona kafokeana au kampiga maza.

Ila huyu mke wangu kumpiga ilikuwa ni lazma ili nimuweke sawa.
Mzee ni mtata kwenye misingi huwa hayumbishwi.

Ila mtoto wangu akibaki nae ataharibika, siwezi kabisa kusema abaki nae.
 
Mkuu utata wa mzee sijawahi ona kafokeana au kampiga maza.

Ila huyu mke wangu kumpiga ilikuwa ni lazma ili nimuweke sawa.
Mzee ni mtata kwenye misingi huwa hayumbishwi.

Ila mtoto wangu akibaki nae ataharibika, siwezi kabisa kusema abaki nae.
Kumpiga mke hakumuweki sawa bali kutamfanya awe sugu na atakudharau maana hatahisi unampenda. Tafuta adhabu nyingine lakini sio kumpiga, acha huo ubabe wa kizamani, haufanyi kazi kwenye kizazi hiki cha sasa hivi.
Na ukizoea kumpiga ipo siku mtoto atashuhudia and trust me atakuchukia.

Kwasasa mtoto bado ni mdogo, miaka miwili huwezi kukaa nae mwache kwa mama yake hadi akifikisha miaka 4 au mitano ndo uanze mchakato wa kukaa nae.
Kwasasa hivi kung'ang'ania mtoto ni kama vile unamng'ang'ania huyo mama yake.
Kama humtaki piga kimya utulie lakini usiache kumuona mtoto na kumuhudumia kwa mahitaji ya msingi.
 
Wewe na huyo mkeo wote mna akili za kitoto,

Kuna mambo umejaribu kuyaficha hapa,ila mkeo anakucheat na wewe unamcheat,kifupi mmekutana Pipa na Mfuniko,

Mkeo kapangishiwa na mchepuko wake na ndiye anayempa kiburi,na wewe endelea na huyo ex wako,

Namuhurumia sana mtoto wenu kupata wazazi wa aina yako na huyo mkeo.
 
Mlete mkeo naye aelezee hatutoi ushauri bila kusikiliza upande wa pili
 
Mkuu mimi sina mahusiano nnje ya ndoa, na sina vita na ma eX.
 
Oa at your own risk. Kama hivyo yaani😃
Dah sahihi mkuu.

Nimewaza mengi sana kwa sasa naona nibadili dini, nijitenge kabisa na maisha niliyo yazoea, nijiweke karibu na mwenyezi mungu.

Kiufupi niwe mtu wa tofauti kabisa na kawaida.
 
Kaka we kausha kimya kwanza focus na mambo mengine usipige simu tulia kimya uone itakuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…