Ushauri: Baba mkwe katupa kiwanja nijenge na mwanaye wa kike. Ninasita, nikubali au niache sababu naingia mtegoni?

Ushauri: Baba mkwe katupa kiwanja nijenge na mwanaye wa kike. Ninasita, nikubali au niache sababu naingia mtegoni?

Wakuu habarini,

Hivi karbuni nimebahatika kufunga ndoa na mke wangu, wakati huo nishampatia mimba.

Hivi karibuni baba mkwe nilimwambia anitaftie kiwanja cha million 1.5 -2, cha kushangaza mzee wa watu akatupa kiwanja cha Bure tujenge mimi na mwanae wa kike, ili hiyo pesa niliyotaka kununulia kiwanja tuweke kwenye ujenzi.

Mpaka sasa hivi nimesita kwanza kujenga hicho kiwanja, ninahofia siku tukikosana au kuachana na mtoto wake itakuwaje na nishajenga nyumba pale?

Wakuu naombeni mnishauri, nijenge au niache kiwanja? Maana kipo katikakati ya mji na amesema tukijenge.

Kuhusu maisha ya baba mkwe yeye yupo vizuri kwani ni msitaafu, hana shida kabisa. Watoto wake karibu wote wapo serikalini.

Ushauri wenu wa muhimu sana, karbuni.
Ukijenga hapo, jiandae kwa masimango pindi mkikorofisha na mkeo..!!!
 
Usikatae ila usiache kununua kingine ukajenga. Jipe challange kuwa unasehemu mbili za kujenga, Priority iwe kwenye ulichonunua wewe, hicho cha mzee nenda nacho taratibu.

UACHE KIHEREHERE NA KUTAFUTA SIFA KWA WAKWE, BABA MKWE WAKO NI DALALI KUMUAMBIA AKUTAFUTIE KIWANJA?
 
Mwenyewe imenishangaza sana, kwamba imekuwaje mambo yake binafsi anamshirikisha baba mkwe?

Ndio maana mzee wa watu akaona isiwe tabu, dogo bado hajakomaa ngoja niwape cha bure.
Kama hii simulizi yake ni kweli, basi kajifedhehesha yeye na ukoo wake wote.

Kaonesha 'utegemezi' kwenye familia ya mke. Ni kama yeye nd'o kaolewa.

Kitendo cha kuoa bila kuwa na kiwanja ni aibu, kwako mwanaume na familia yenu iliyoshindwa kukupatia. Angelijua hilo, angenunua kiwanja kimyakimya kwa heshima yake.
 
Mdogo wangu chukua huu uchauri......mimi ni mmoja kati ya wale tuliowahi kupewa zawadi ya kiwanja na mashamba,tulichokifanya kwanza tuliwashukuru familia kwa upendo wao kwetu na pili tulikuja na azimio la pamoja yaani mimi na mkewangu kwenda kwa wakwe kwamba tumeazimia kuhamisha eneo na mashamba kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine hivyo tuliomba baraka zao na walikubali hivyo tuliuza maeneo hayo na kwenda kununua sehemu nyingine na sasa tumebahatika kujenga na tunaishi na mashamba ni kweli tulinunua sehemu nyingine na tunalima kila msimu.
 
Ulikosa watu wa kuwashirikisha kukutafutia kiwanja mpaka umchore Bamkwe, ona ulivyochoreka sasa.
Usikikatae ila jenga kajumba ka ajabu hapo hata ka buku kisha endelea na mchakato wako wa kutafuta kiwanja chako na kukijenga.
 
Yaani wewe ungeanza kufikiia kuachana mapema hivi?ni hatari sana kwa mustakabali wa ndoa.Ni sawa na kumuhusu Mtu wako wa jaribu kuwa ni Mchawi,hutokaa umuaminina kila atakachofanya utahisi anakuloga.Ushauri wangu ni uache mawazo hayo na onesha kujali zawadi uliyopewa kea roho safi na anza ujenzi mara moja,suala la ndoa kuvunjika ni kama akali tu ndio maana hatuachi kupanda Ndege kwa sababu ikianguka tunakufa.Labda kama kuna viashiria ambayo umeshaviona mapema hii.
 
Mtagini jamaa kwwnye ule uzi wa yule jamaa aliyepewa zawadi ya kiwanja na baba mkwe wake then akajenga nyumba baadae yule mke wake akafariki
 
Kuna namna napata wasiwasi na mleta mada,
Sawa wewe umeshindwa kutafuta, kwanini usimwambie baba yako badala yake unamwambia baba mkwe?.
Kuna namna nimegundua aidha unapenda kitonga, maana uliona ukweni wana maeneo mengi na wewe ulitaka kitonga kwa gia ya akusaidie kutafute eneo.
Mbili mwanamke ana mamlaka kuliko wewe na ndio aliyekupa wazo la kumwambia baba yake. Soon naona familia ya mke ikikutawala.
Wewe ni dhaifu sana
 
Shida ilianzia wewe kuanza kumshirikisha mipango yako baba mkwe... hukuona madalali uwape io kazi
 
Wakuu habarini,

Hivi karbuni nimebahatika kufunga ndoa na mke wangu, wakati huo nishampatia mimba.

Hivi karibuni baba mkwe nilimwambia anitaftie kiwanja cha million 1.5 -2, cha kushangaza mzee wa watu akatupa kiwanja cha Bure tujenge mimi na mwanae wa kike, ili hiyo pesa niliyotaka kununulia kiwanja tuweke kwenye ujenzi.

Mpaka sasa hivi nimesita kwanza kujenga hicho kiwanja, ninahofia siku tukikosana au kuachana na mtoto wake itakuwaje na nishajenga nyumba pale?

Wakuu naombeni mnishauri, nijenge au niache kiwanja? Maana kipo katikakati ya mji na amesema tukijenge.

Kuhusu maisha ya baba mkwe yeye yupo vizuri kwani ni msitaafu, hana shida kabisa. Watoto wake karibu wote wapo serikalini.

Ushauri wenu wa muhimu sana, karbuni.

Jenga mkuu. Ukimaliza Ujenzi tafuta kiwanja kingine tena, huko nako ukajenge.
 
Kwamba mashem karibia wote wako serikalini umepata unafuu kwakweli 🤣🤣🤣🤣, hiyo hela nunua kiwanja chako pembeni master ukiendeleze na hicho
 
Tafuta cha kwako ujenge,ukijenga kwenye hicho kiwanja hautakuwa huru kwenye hiyo nyumba.
 
Utabiri wangu utakuwa umeoa ukweni kwangu huku kasikazini,nami yalinikuta nikachomoa.
 
Wakuu habarini,

Hivi karbuni nimebahatika kufunga ndoa na mke wangu, wakati huo nishampatia mimba.

Hivi karibuni baba mkwe nilimwambia anitaftie kiwanja cha million 1.5 -2, cha kushangaza mzee wa watu akatupa kiwanja cha Bure tujenge mimi na mwanae wa kike, ili hiyo pesa niliyotaka kununulia kiwanja tuweke kwenye ujenzi.

Mpaka sasa hivi nimesita kwanza kujenga hicho kiwanja, ninahofia siku tukikosana au kuachana na mtoto wake itakuwaje na nishajenga nyumba pale?

Wakuu naombeni mnishauri, nijenge au niache kiwanja? Maana kipo katikakati ya mji na amesema tukijenge.

Kuhusu maisha ya baba mkwe yeye yupo vizuri kwani ni msitaafu, hana shida kabisa. Watoto wake karibu wote wapo serikalini.

Ushauri wenu wa muhimu sana, karbuni.
Usijenge hapo, utaingia mtegoni.
Mwezi wa tatu Kuna kikao cha Wanaume wote, usikose.

Ukijenga tu, ipo siku,
Utaumia,
Utajuta,
Utalia,
Utakimbia.
 
Back
Top Bottom