Ushauri Balozi HP: Ukiongoka, Kujitenga na Uovu na Kusema Ukweli, Sema Ukweli Wote Sio Ukweli Nusu Nusu!. Jitenge Jumla Sio Mguu Ndani, Mguu Nje!

Ndiyo maana nimesema nimeandika nikafuta maana mleta mada anataka kumlengesha mzee .

Ila kikubwa nilitaka kuuliza kwanini kamuita mdogo wake alafu anataka kutuingiza matatizoni wengine zaidi
Watanzania wengi hawajui kufocus kwenye message gani wanataka kusema.

Yule Polepole ka ramble all over the place yeye mtakatifu sanaa, anataka kuiona mbinguuu, hivii, vileee, yeye kashashika nafasi kubwa sanaaa, mpaka ana distract message yake muhimu kuhusu ombwe la uongozi.

Huyu naye maneno meengi Polepole shujaa, Polepole mdogo wakee, mambo kibao irrelevant mpaka unapata tabu kuelewa point inayotaka kusemwa ni ipi hapa.

Na huyo ndiye mtu kashakuwa muandishi wa habari na kasoma sheria.

Yani kitu kinachoweza kuelezwa kwa maneno 100 kitaandikwa kwa maneno 3,000.

Na kila mtu anavyozidi kuandika zaidi au kusema zaidi ndivyo anavyozidi kuji contradict.

We can't be precise and succinct (you see what I did there?)
 
Bora umeleta uzi, asiishie kujitenga na serikali tu, aondoke na kwenye chama.

Serikali nivya chama cha mapinduzi na havitenganishwi, mwenyekiti ndiye rais.

Na wakuu wa serikali na vitengo vyake vyote ni wana ccm, hivyo hakupaswa kuishia njiani.

Alipaswa aendelee kujitia mpaka chamani.
 
Nikianza na paragraph yako ya tatu na nne.

HP alijikita zaidi kupambana na chama chake na sio Serikali, amemzungumzia Rais kama mwenyekiti wa chama na mgombea Urais wa CCM na sio RAIS. ( Ndio maana kwenye Katiba mpya tulitaka Mwenyekiti wa Chama asiwe RAIS wa nchi) - ili akishambuliwa mwenyekiti wa CCM issue isiwe RAIS wa nchi, lakini pia ingeweza kuepusha rasimali za nchi kutumika kwenye shughuli za chama.

HP alijua kabisa matatizo yaliyopo hayawezi kutatuliwa ndani ya siku moja maana yamejengwa na kuwepo zaidi ya miaka kumi, kuyaondoa lazima mfumo mzima uliopo utoke.
Kwa kujua pia bosi wa mamlaka yake ya uteuzi naye ni sehemu ya mfumo anaoupigia kelele, isingeweza kusaidia kwa yeye kusubiri majibu au kuresign kimyakimya zaidi ya dhamira yake kujulikana na yeye kuwahiwa.

Kwa HP kutoka public na kutoa sababu alizotoa, inatupa picha lengo lake ni jamii ijuye nini kilichopo ndani na yeye sio sehemu yakilichopo na upande wake ni upande wa Watanzania na sio watesi, hii itamfanya kuwin nguvu ya umma na kuwa na ulinzi wa umma, maana malalamiko yake ndio malalamiko ya umma.

Ndani ya viunga vya Damascus - Syria.
 
Wanabodi,
Huu ni ushauri wa Bure kwa Balozi Humprey Polepole.

Tukubali tukatae, kitendo alichokifanya Balozi Humprey Polepole, kujiuzulu nyadhifa yenye hadhi kubwa kama ya ubalozi, ni kitendo cha kishujaa, hivyo Balozi Polepole ni shujaa mzalendo wa kweli kama Mwalimu Nyerere. Sii wengi wanajua kuwa mara baada ya Tanganyika kupata uhuru kutoka kwa Wakoloni Waingereza, na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika, kuna jambo lilitokea, Mwalimu Nyerere akajiuzulu wadhifa huo ndani ya miezi yake mine tuu, nchi ikawa chini ya Rashidi Kawawa. Hata ule mwaka 1985 alipomuachia Ali Hassan Mwinyi Urais wa Tanzania, yeye alipaswa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, lakini aliamua kung'atuka, hivyo Polepole ni shujaa kama Nyerere!.

Balozi Polepole ameandika barua ya kujiuzulu na kumpelekea Rais, kwenye barua hiyo ametoa sababu kumi za kujiuzulu. Barua hiyo imeonyesha utovu mkubwa wa nidhamu kwa mamlaka yake ya uteuzi!. Kwa kawaida barua za kujiuzulu nafasi nyeti, huwa zinafanywa siri, mpaka baada ya mamlaka yake ya uteuzi kukubali kujiuzulu kwake, ndipo zinatangazwa hadharani, kwa sababu kuna viongozi wanaweza kuamua kujiuzulu kwa hasira za kijinga tuu, lakini mamlaka ya uteuzi ikagoma, hivyo alichokifanya Balozi Polepole, kuandika barua ya kujiuzulu, na hata kabla hajajibiwa amekubaliwa au amekataliwa, yeye akaitundika kwenye mitandao ya jamii. Huu ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa mamlaka yake ya uteuzi, Nyerere alipojiuzulu, ilikuwa siri, na sababu pia alizifanya siri.

Tukija kwenye sababu za kujiuzulu Balozi Polepole alizotoa, sisi wa jicho la tatu, tunajua amesema ukweli nusu!, ndio maana bado yuko mguu ndani, mguu nje!. Mguu mmoja, bado ni mwanachama wa kawaida wa CCM, na mguu mwingine nje, ameamua kujilipua na kujitoa muhanga kuisema vibaya serikali na chama chake, japo ukweli anaousema ni ukweli mchungu kwa mwaka wa uchaguzi na utakijeruhi chama, lakini ni ukweli ambao viongozi wasiopenda kuambiwa ukweli, hawapendi kuusikia. Sisi wa jicho la tatu, tunajua Polepole ameusema ukweli nusu tuu. Je atoe miguu yote nje asimame pembeni na kuusema ukweli wote uliobakia, apewe maua yake?, au huu huu ukweli nusu na ukweli kiduchu alioutoa unatosha kumpa maua, huku ameufukia ukweli mkubwa na mchungu zaidi wa awamu ya 5, kwasababu alikuwa anakula meza kuu?. Je nini kimemtokea kumfanya aseme sasa wakati siku zote alikuwepo na yanayofanyika, yote yamefanyika yeye yupo? . Jee Polepole ana malengo gani na ukweli huu mwaka wa uchaguzi?, Kiingereza wanaita (what is his
motives behind) kufanya hiki alichokifanya, na amefanya haya ili iweje?, na mwisho nitamalizia na matokeo ya alicho kifanya, yaani (the consequences) ya kujiuzulu kwake kwa serikali, kwa CCM na kwake binafsi.

Hapa nakuletea hoja 10 za kujiuzulu alizozitoa kwenye barua yake ya kujiuzulu ambazo zina mambo makubwa na ya msingi sana!, unaweza kumbeza Polepole, ni binadamu tuu lakini huwezi kubeza hoja zake!

Hoja 10 za Polepole kujiuzulu, kuna mambo ameyataja kijuu tuu, yaani ametuwekea ukweli nusu, na kuna mambo makubwa mabaya ya kutisha na kusikitisha, anayajua, lakini hakuyasema, kwa sababu na yeye alikuwa ni sehemu ya kwayo hayo mambo!. Sisi watu wa jicho la tatu kwa kumsoma, utajua amezungumzia ukweli nusu tuu, kuna ukweli mkubwa anaujua ameuhifadhi. Hata kwa ndugu zetu Waislamu, kula Nguruwe ni haramu!, lakini wanashauriwa, ukiamua kula nguruwe, chagua aliyenona!.

Hizi ni hoja zake kumi, nakuchambualia anajua nini, amesema nini na nini hakusema!

1. Mwelekeo wa uongozi usiojielekeza ipasavyo katika kusimamia Haki za watu, Amani na kuheshimu watu,” -hapa anazungumzia watu kupotezwa, na hata hizi kesi za mchongo!, Balozi Polepole anawajua wasiojulikana, anawaita wahuni!, lakini hawezi kuwataja kwasababu na yeye alikuwa sehemu yao!. Maadamu sasa ameongoka, aseme kweli, awataje na Watanzania tuwajue!.

2. Kufifia kwa dhamira ya kweli na uwajibikaji wa dhati wa kushughulikia kero na changamoto za wananchi- hapa anazungumzia uwajibikaji, unazijua fika sababu za kufifia uwajibikaji wa dhati na kushughulikia kero za wananchi. Mhe. Jerry Slaa alipoteuliwa Waziri wa Ardhi, alishughulikia kero za wananchi kwa dhati na mara akaondolewa!. Paul Makonda alipoteuliwa Mwenezi, alishughulikia uwajibikaji wa serikali ya CCM kwa wananchi, ghafla akaondolewa!. Polepole anazijua sababu lakini hazisemi!.

3. Kudidimia kwa maadili ya uongozi katika ngazi mbalimbali- hapa anazungumzia rushwa na ufisadi, Polepole anajua vizuri kabisa wala rushwa na mafisadi!, anajua hata fedha za Kagoda zilichotwaje na zilifanya nini, anaujua kabisa mzizi wa rushwa na ufisadi wa nchi hii, lakini hausemi kwa sababu fulani ambayo hata mimi naijua na pia siisemi!.

4. Kudhoofika kwa utekelezaji wa majukumu ya msingi ya serikali kwa ajili ya ustawi wa wananchi - hapa anazungumzia udhaifu wa serikali awamu ya 6, Polepole anajua fika udhaifu umelalia wapi lakini ameamua kuutata tuu, na sio tuu anaujua udhaifu pia anayajua madhaifu na anawajua wadhaifu lakini hawataji!.

5. Mambo haya yanateteresha maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - hapa anazungumzia maslahi ya taifa, hili la maslahi ya taifa, nakiri Polepole ni mzalendo, ila lazima asimame pepembeni ndipo alipigie kelele!.

6. Haya yote yamezidi kunifanya nikose amani ya moyo na imani katika uongozi niliopo ndani yake sasa- hapa anazungumzia kukosa amani na imani na serikali ya awamu ya 6, na hapa ndipo Polepole alipoongoka, kama ni amejiongokea yeye mwenyewe kwa kuamua kuongoka, ni haki yake kuchagua ukweli gani auseme na ukweli gani asiuseme, ila kama ameongolewa na YEYE, inampasa aseme tuu ukweli wote na yule YEYE, atasimama na yeye!.

7. Matukio ya hivi karibuni ya wazi ya kukiuka misingi, utamaduni na desturi za Chama cha Mapinduzi (CCM) hususan katika mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya Chama- Hapa anazungumzia kile kilichofanyika Dodoma kwenye uteuzi wa wagombea urais wa JMT na Zanzibar. Hapa Polepole anajua kila kitu, na sababu ya kufanyika kilicho fanyika, lakini ameamua kujifanya ana shangaa!. Mungu asingemuita kwake yule Kaka yetu, ni Polepole huyu huyu angekuwa mstari wa mbele kuhakikisha ile "atake asitake" kwa Kaka inapita!, lakini kwa sababu sasa ni Dada, ndio anajifanya kushangaa!.

8. Kila awamu huwa msingi wa kukihuisha Chama na fursa ya kufanya Mageuzi hukipa chama sura ng’aavu mbele ya umma kabla ya uchaguzi desturi hii ya kufanya mageuzi ndani ya chama imekuwa nguzo muhimu ya ukubalifu na ushindi wa CCM mbele ya umma- Hapa anazungumzia ukubalifu wa CCM kumaanisha CCM haikubaliki sana kivile. Hili hakuna mtu anayelijua vizuri kama Polepole!, anakijua kila kinachofanyika kwenye chaguzi na CCM kuibuka kidedea!, kwa vile sasa ameongoka, bado yuko mguu ndani mguu nje, akisimama nje mazima, ukweli huu wa kinachofanyikaga, atakisema kama alivyosema Nape, alipoteleza ulimu kule Bokoba!.

9. Imekuwepo kauli maarufu ya CCM isemayo “Chama kwanza mtu baadaye”, kauli hii inafanyika vinginevyo, nimejiuliza mara kadhaa ni maslahi ya nani yanapiganiwa wakati huu, mtu, kikundi au Chama Taasisi?- Hapa anazungumzia uzalendo kwa CCM badala ya uzalendo kwa nchi!. Hili pia Polepole analijua sana na anakijua fika kile kinachowafika wazalendo wa kweli!.

10. Siwezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba ya nchi na chama, haki, maadili, utu na uwajibikaji kwa wananchi - hapa anazungumzia yale mambo mengine yote ya ajabu ajabu yanayofanywa na serikali, Bunge na Mahakama, ikiwemo kututungia sheria batili, kuunda INEC kiubatili, na vitu kama hivyo. Hapa sasa ndipo Balozi Polepole anapotakiwa kusimama kuhesabiwa ili Watanzania tumpe maua yake.

Hitimisho.

Watu kama hawa wa type hii ya Polepole , humo ndimo Gwajima yumo, humo ndimo Luhanga Mpina yumo!, japo hawana nidhamu, ila ni wasema ukweli ndio watamsaidia Rais Samia kwa kumwambia ukweli, Watalisaidia Taifa na kuwasaidia Wananchi, ila ili Polepole ajitendee haki na kuitendea haki nchi hii, alikuwa na option ya kujiuzulu na kujikalia kimya bila kutoa sababu, kwa vile kaamua kuwa mkweli kwa kusema ukweli na kusimama na ukweli, namshauri, akae pembeni auseme ukweli wote uliobakia, japo atapopolewa sana mawe, atayakuta maua yake tumemtayarishia!.

Paskali
Kaka yake Polepole!.
Polepole ni Mcheza kamali au Gambler.
Kenny Rogers alishatoa wosia kuhusu Gambler kwenye maisha yake anatakiwa aishi au achezeje.....
Labda yeye ndivyo kapanga Karata zake ..

View: https://youtu.be/MdgoQyY33Go?si=FnB4Z-7gUon2PziC
 
Polepole ni mnafiki na sio wa kuaminika. Haya yanayoendelea sasa ni zao la awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ambapo polepole alikuwa kiongozi wa ngazi za juu huko ccm na sometimes walitoa maamuzi yao kama viongozi pasi na kushirikisha wanachama wa ccm.
Haya anayoyasema leo polepole yeye ndiye muasisi.

Tunachokihitaji ni katiba moja iliyosukwa vizuri sana. Hiyo ndio itakuwa salama kwa nchi yetu dhidi ya viongozi walaghai.
 
Motives ni kumtoa SSH asigombee 2025 tu, hilo la genge la wahuni kichaka tu😁
 
Sawa Kaka yake Polepole
 
Hata kwa ndugu zetu Waislamu, kula Nguruwe ni haramu!, lakini wanashauriwa, ukiamua kula nguruwe, chagua aliyenona!.
Dah hapa umeamua tu kunogesha kidgo mada ila uhalisia wa ruhusa iliyotoka ni kunapokuwa na dharura ya njaa ya kufa na hakuna vilivyo vya halali kwa muda huo na yenyewe ni kwa kiasi bila kujishindilia
 
Mkubwa P umeamua kusimama kwenye ukweli endelea mana umeshalipia gharama zake tayari wenye kuelewa wameelewa ushauri wako wa Balozi kumalizia ukweli ni mzuri sana kwa kuiponya nchi mana hakuna namna ma alichokifanya ni disobidience positive ingawa ina madhara ya usaliti na haijalishi mambo yake ya nyuma ila hoja ni za ukweli kwanini aziseme sasa hilo ni jambo na mjadala mwengine ambao hauhusiani na hoja zake za msingi ambazo hazijajibiwa hadi wakati huu zaidi yamayowe ya hapa na pale

No reform No Election taifa la wote
 
Kusema ukweli sio uadui. Kwamba mke/mume akiwa mchafu inatakiwa ujitenge nae lahasha inabidi umfundishe huku mkibaki kwenye status yenu ile ile zaidi unapunguza au kuongeza umakini kwa baadhi ya mambo.
huo mfano wako haundani kabisa..Polepole anatakiwa atoke huko awe katika kundi la watakatifu kama ambovo anavojiita kwasasa ili watakatifu wenzie wamuunge mkono..kutokufanya hvo ni drama za kisiasa..japo kaongea mambo ambayo serikali ilipaswa iyatolee majibu haraka ili kurejesha imani kwa wananchi.
 
Kusema ukweli sio uadui. Kwamba mke/mume akiwa mchafu inatakiwa ujitenge nae lahasha inabidi umfundishe huku mkibaki kwenye status yenu ile ile zaidi unapunguza au kuongeza umakini kwa baadhi ya mambo.
Ndio uweke wazi huo uchafu wake wote ili aweze kujirekebisha jumla km inawezekana sio unatoa uchafu nusunusu
 
Polepole ni shujaa kwa kusema ukweli ambao watanzania walikuwa wanaona lakini wanashindwa kusema ...Polepole anatakiwa aje na njia mbadala wa kutatua hzo changamoto atuambie ss wtz...Pole pole anatakiwa kuondoka CCM kwani kaonesha kuwa hoja zake anapoziwasilisha ndani ya Chama wanazidharau ndo maana kaamua kuweka hadharani kutokufanya hvo ni drama za kisiasa..Polepole anatakiwa aanzishe chama chake nasio kwenda chama kingine kutokufanya hvo ni drama za kisiasa,, akishindwa aachane na mambo ya Siasa kabisa...Polepole alijivisha mabovu kaamua kujilipua yeye na jopu lake...
 
Kwanza naendelea kumpongeza Polepole, pili sikubaliani nayeye aseme yote. Kwasababu ya Watanzania wengi, hawajielewi wako ili mradi siku inaenda. Kwahiyo, asihatarishe zaidi maisha yake kwa watu wa aina hiyo. Kafanya uzalendo, wa kuyaelezea madudu kaeleweka kazi imebaki kwa Watanzania kuchagua mbivu na mbichi.
Nasisitiza
Kwasababu ya Watanzania wengi, hawajielewi wako ili mradi siku inaenda.
 
Pole pole Gwajima na Mpina sio kwamba Hawana nidhamu /Adabu wanazo sana ila inaoenekana kwamba walipambana sana Kwa ndani wakiwa wanatafuta nafasi ya kubadilisha mambo Kwa kuwashrikisha Wakubwa lakini maoni Yao yakawa Yana tupiliwa mbali , So kawaida ya binaadamu The way ilivyo hauwezi kumzuia kudai haki maana ndoto ya mtu Huwa ni Wito wa ndani yake na wito Huwa una desturi ya kumsukuma mtu ndani yake ili Aweze kutimiza jukumu lililo mleta hapa Duniani, So inapofikia hatua kama hiyo ndio Huwa inatokea mambo kama hayo ,

But all in all Kwa Upande wangu pole pole sio shujaa ila ni kwakuwa siasa jinsi ilivyo nilazima kuwe na power imbalance ili pasiweze kutokea mrafaruku ndani ya chama serikali au Taifa Zima Kwa ujumla so it seems ndani ya chama Chao hakuna power imbalance Kuna upande ambao umeamua kuitafuna keki ya Taifa pasipo kuwapa wenzao nafasi vyema ya kuitafuna hiyo keki na huo upande ya wasio itafuna hiyo keki vyema ndio wapo kina pole pole

That's why unaona pole pole kaamua kumwaga mboga baada ya walio na power kumwaga ugali Ili Tukose wote
Mkuu
I barely see you writing something long such as this. Bless up.
 
Back
Top Bottom