Ushauri Balozi HP: Ukiongoka, Kujitenga na Uovu na Kusema Ukweli, Sema Ukweli Wote Sio Ukweli Nusu Nusu!. Jitenge Jumla Sio Mguu Ndani, Mguu Nje!

Ushauri Balozi HP: Ukiongoka, Kujitenga na Uovu na Kusema Ukweli, Sema Ukweli Wote Sio Ukweli Nusu Nusu!. Jitenge Jumla Sio Mguu Ndani, Mguu Nje!

Wanabodi,
Huu ni ushauri wa Bure kwa Balozi Humprey Polepole.

Tukubali tukatae, kitendo alichokifanya Balozi Humprey Polepole, kujiuzulu nyadhifa yenye hadhi kubwa kama ya ubalozi, ni kitendo cha kishujaa, hivyo Balozi Polepole ni shujaa mzalendo wa kweli kama Mwalimu Nyerere. Sii wengi wanajua kuwa mara baada ya Tanganyika kupata uhuru kutoka kwa Wakoloni Waingereza, na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika, kuna jambo lilitokea, Mwalimu Nyerere akajiuzulu wadhifa huo ndani ya miezi yake mine tuu, nchi ikawa chini ya Rashidi Kawawa. Hata ule mwaka 1985 alipomuachia Ali Hassan Mwinyi Urais wa Tanzania, yeye alipaswa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, lakini aliamua kung'atuka, hivyo Polepole ni shujaa kama Nyerere!.

Balozi Polepole ameandika barua ya kujiuzulu na kumpelekea Rais, kwenye barua hiyo ametoa sababu kumi za kujiuzulu. Barua hiyo imeonyesha utovu mkubwa wa nidhamu kwa mamlaka yake ya uteuzi!. Kwa kawaida barua za kujiuzulu nafasi nyeti, huwa zinafanywa siri, mpaka baada ya mamlaka yake ya uteuzi kukubali kujiuzulu kwake, ndipo zinatangazwa hadharani, kwa sababu kuna viongozi wanaweza kuamua kujiuzulu kwa hasira za kijinga tuu, lakini mamlaka ya uteuzi ikagoma, hivyo alichokifanya Balozi Polepole, kuandika barua ya kujiuzulu, na hata kabla hajajibiwa amekubaliwa au amekataliwa, yeye akaitundika kwenye mitandao ya jamii. Huu ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa mamlaka yake ya uteuzi, Nyerere alipojiuzulu, ilikuwa siri, na sababu pia alizifanya siri.

Tukija kwenye sababu za kujiuzulu Balozi Polepole alizotoa, sisi wa jicho la tatu, tunajua amesema ukweli nusu!, ndio maana bado yuko mguu ndani, mguu nje!. Mguu mmoja, bado ni mwanachama wa kawaida wa CCM, na mguu mwingine nje, ameamua kujilipua na kujitoa muhanga kuisema vibaya serikali na chama chake, japo ukweli anaousema ni ukweli mchungu kwa mwaka wa uchaguzi na utakijeruhi chama, lakini ni ukweli ambao viongozi wasiopenda kuambiwa ukweli, hawapendi kuusikia. Sisi wa jicho la tatu, tunajua Polepole ameusema ukweli nusu tuu. Je atoe miguu yote nje asimame pembeni na kuusema ukweli wote uliobakia, apewe maua yake?, au huu huu ukweli nusu na ukweli kiduchu alioutoa unatosha kumpa maua, huku ameufukia ukweli mkubwa na mchungu zaidi wa awamu ya 5, kwasababu alikuwa anakula meza kuu?. Je nini kimemtokea kumfanya aseme sasa wakati siku zote alikuwepo na yanayofanyika, yote yamefanyika yeye yupo? . Jee Polepole ana malengo gani na ukweli huu mwaka wa uchaguzi?, Kiingereza wanaita (what is his
motives behind) kufanya hiki alichokifanya, na amefanya haya ili iweje?, na mwisho nitamalizia na matokeo ya alicho kifanya, yaani (the consequences) ya kujiuzulu kwake kwa serikali, kwa CCM na kwake binafsi.

Hapa nakuletea hoja 10 za kujiuzulu alizozitoa kwenye barua yake ya kujiuzulu ambazo zina mambo makubwa na ya msingi sana!, unaweza kumbeza Polepole, ni binadamu tuu lakini huwezi kubeza hoja zake!

Hoja 10 za Polepole kujiuzulu, kuna mambo ameyataja kijuu tuu, yaani ametuwekea ukweli nusu, na kuna mambo makubwa mabaya ya kutisha na kusikitisha, anayajua, lakini hakuyasema, kwa sababu na yeye alikuwa ni sehemu ya kwayo hayo mambo!. Sisi watu wa jicho la tatu kwa kumsoma, utajua amezungumzia ukweli nusu tuu, kuna ukweli mkubwa anaujua ameuhifadhi. Hata kwa ndugu zetu Waislamu, kula Nguruwe ni haramu!, lakini wanashauriwa, ukiamua kula nguruwe, chagua aliyenona!, hivyo kama Balozi Polepole, ameamua kujizima data na kujilipua, ajilipue jumla mazima, auseme ukweli wote ukiwemo ule ukweli wa biashara ya siasa na kununua watu, na kuwaumbua wahuni wenzake wote na mambo aliyokuwa akiyafanya wakati akiwa ni Saulo, kabla ya kuongoka na kugeuka Paulo!. Ukiamua kumkataa shetani, mkatae na mambo yake yote uyakatae!.

Hizi ni hoja zake kumi, nakuchambualia anajua nini, amesema nini na nini hakusema!

1. Mwelekeo wa uongozi usiojielekeza ipasavyo katika kusimamia Haki za watu, Amani na kuheshimu watu,” -hapa anazungumzia watu kupotezwa, na hata hizi kesi za mchongo!, Balozi Polepole anawajua wasiojulikana, anawaita wahuni!, lakini hawezi kuwataja kwasababu na yeye alikuwa sehemu yao!. Maadamu sasa ameongoka, aseme kweli, awataje na Watanzania tuwajue!.

2. Kufifia kwa dhamira ya kweli na uwajibikaji wa dhati wa kushughulikia kero na changamoto za wananchi- hapa anazungumzia uwajibikaji, unazijua fika sababu za kufifia uwajibikaji wa dhati na kushughulikia kero za wananchi. Mhe. Jerry Slaa alipoteuliwa Waziri wa Ardhi, alishughulikia kero za wananchi kwa dhati na mara akaondolewa!. Paul Makonda alipoteuliwa Mwenezi, alishughulikia uwajibikaji wa serikali ya CCM kwa wananchi, ghafla akaondolewa!. Polepole anazijua sababu lakini hazisemi!.

3. Kudidimia kwa maadili ya uongozi katika ngazi mbalimbali- hapa anazungumzia rushwa na ufisadi, Polepole anajua vizuri kabisa wala rushwa na mafisadi!, anajua hata fedha za Kagoda zilichotwaje na zilifanya nini, anaujua kabisa mzizi wa rushwa na ufisadi wa nchi hii, lakini hausemi kwa sababu fulani ambayo hata mimi naijua na pia siisemi!.

4. Kudhoofika kwa utekelezaji wa majukumu ya msingi ya serikali kwa ajili ya ustawi wa wananchi - hapa anazungumzia udhaifu wa serikali awamu ya 6, Polepole anajua fika udhaifu umelalia wapi lakini ameamua kuutata tuu, na sio tuu anaujua udhaifu pia anayajua madhaifu na anawajua wadhaifu lakini hawataji!.

5. Mambo haya yanateteresha maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - hapa anazungumzia maslahi ya taifa, hili la maslahi ya taifa, nakiri Polepole ni mzalendo, ila lazima asimame pepembeni ndipo alipigie kelele!.

6. Haya yote yamezidi kunifanya nikose amani ya moyo na imani katika uongozi niliopo ndani yake sasa- hapa anazungumzia kukosa amani na imani na serikali ya awamu ya 6, na hapa ndipo Polepole alipoongoka, kama ni amejiongokea yeye mwenyewe kwa kuamua kuongoka, ni haki yake kuchagua ukweli gani auseme na ukweli gani asiuseme, ila kama ameongolewa na YEYE, inampasa aseme tuu ukweli wote na yule YEYE, atasimama na yeye!.

7. Matukio ya hivi karibuni ya wazi ya kukiuka misingi, utamaduni na desturi za Chama cha Mapinduzi (CCM) hususan katika mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya Chama- Hapa anazungumzia kile kilichofanyika Dodoma kwenye uteuzi wa wagombea urais wa JMT na Zanzibar. Hapa Polepole anajua kila kitu, na sababu ya kufanyika kilicho fanyika, lakini ameamua kujifanya ana shangaa!. Mungu asingemuita kwake yule Kaka yetu, ni Polepole huyu huyu angekuwa mstari wa mbele kuhakikisha ile "atake asitake" kwa Kaka inapita!, lakini kwa sababu sasa ni Dada, ndio anajifanya kushangaa!.

8. Kila awamu huwa msingi wa kukihuisha Chama na fursa ya kufanya Mageuzi hukipa chama sura ng’aavu mbele ya umma kabla ya uchaguzi desturi hii ya kufanya mageuzi ndani ya chama imekuwa nguzo muhimu ya ukubalifu na ushindi wa CCM mbele ya umma- Hapa anazungumzia ukubalifu wa CCM kumaanisha CCM haikubaliki sana kivile. Hili hakuna mtu anayelijua vizuri kama Polepole!, anakijua kila kinachofanyika kwenye chaguzi na CCM kuibuka kidedea!, kwa vile sasa ameongoka, bado yuko mguu ndani mguu nje, akisimama nje mazima, ukweli huu wa kinachofanyikaga, atakisema kama alivyosema Nape, alipoteleza ulimu kule Bokoba!.

9. Imekuwepo kauli maarufu ya CCM isemayo “Chama kwanza mtu baadaye”, kauli hii inafanyika vinginevyo, nimejiuliza mara kadhaa ni maslahi ya nani yanapiganiwa wakati huu, mtu, kikundi au Chama Taasisi?- Hapa anazungumzia uzalendo kwa CCM badala ya uzalendo kwa nchi!. Hili pia Polepole analijua sana na anakijua fika kile kinachowafika wazalendo wa kweli!.

10. Siwezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba ya nchi na chama, haki, maadili, utu na uwajibikaji kwa wananchi - hapa anazungumzia yale mambo mengine yote ya ajabu ajabu yanayofanywa na serikali, Bunge na Mahakama, ikiwemo kututungia sheria batili, kuunda INEC kiubatili, na vitu kama hivyo. Hapa sasa ndipo Balozi Polepole anapotakiwa kusimama kuhesabiwa ili Watanzania tumpe maua yake.

Hitimisho.

Watu kama hawa wa type hii ya Polepole , humo ndimo Gwajima yumo, humo ndimo Luhanga Mpina yumo!, japo hawana nidhamu, ila ni wasema ukweli ndio watamsaidia Rais Samia kwa kumwambia ukweli, Watalisaidia Taifa na kuwasaidia Wananchi, ila ili Polepole ajitendee haki na kuitendea haki nchi hii, alikuwa na option ya kujiuzulu na kujikalia kimya bila kutoa sababu, kwa vile kaamua kuwa mkweli kwa kusema ukweli na kusimama na ukweli, namshauri, akae pembeni auseme ukweli wote uliobakia, japo atapopolewa sana mawe, atayakuta maua yake tumemtayarishia!.

Paskali
Kaka yake Polepole!.
🙋✍️👏👍🤝🙏
 
Wanabodi,

Hitimisho.

Watu kama hawa wa type hii ya Polepole , humo ndimo Gwajima yumo, humo ndimo Luhanga Mpina yumo!, japo hawana nidhamu, ila ni wasema ukweli ndio watamsaidia Rais Samia kwa kumwambia ukweli, Watalisaidia Taifa na kuwasaidia Wananchi, ila ili Polepole ajitendee haki na kuitendea haki nchi hii, alikuwa na option ya kujiuzulu na kujikalia kimya bila kutoa sababu, kwa vile kaamua kuwa mkweli kwa kusema ukweli na kusimama na ukweli, namshauri, akae pembeni auseme ukweli wote uliobakia, japo atapopolewa sana mawe, atayakuta maua yake tumemtayarishia!.

Paskali
Kaka yake Polepole!.
Leo HP ataongea, labda ndio atatekeleza ushauri huu Leo ni leo asemaye kesho muongo!Leo tarehe 21!Ni siku ya siku!The twenty first to remember! Ni saa mbili kamili usiku! Usikose!
P
 
Wanabodi,
Huu ni ushauri wa Bure kwa Balozi Humprey Polepole.
, kwa vile kaamua kuwa mkweli kwa kusema ukweli na kusimama na ukweli, namshauri, akae pembeni auseme ukweli wote uliobakia, japo atapopolewa sana mawe, atayakuta maua yake tumemtayarishia!.

Paskali
Kaka yake Polepole!.
Huu ni ushauri wangu kwa Polepole, akae kwanza pembeni pahala salama, ndipo afunguke mazima!. Nikasema japo atapopolewa sana mawe, ila maua yake atayakuta tumemtayarishia!.

YEYE Atatenda!
P.
 
Mbona hio signature ya 'Kaka Yake Polepole' umetemana nayo....

1759873081665.png
 
Wanabodi,
Huu ni ushauri wa Bure kwa Balozi Humprey Polepole. ili Polepole ajitendee haki na kuitendea haki nchi hii, alikuwa na option ya kujiuzulu na kujikalia kimya bila kutoa sababu, kwa vile kaamua kuwa mkweli kwa kusema ukweli na kusimama na ukweli, namshauri, akae pembeni auseme ukweli wote uliobakia, japo atapopolewa sana mawe, atayakuta maua yake tumemtayarishia!.

Paskali
Kaka yake Polepole!.
Yuko wapi Polepole?
Polepole yupo pale alipohifadhiwa, ila sisi watu wa ushauri tulimshauri kabla!.

P
 
Siku hii nchi ikiwa uwanja wa vita nitafurahi sana.
Kuna Mungu na shetani, Mungu ni mambo ya kheri na shetani ni mambo ya shari, kuna watu wa Mungu na kuna watu wa shetani!. Watu wa Mungu hufanya yaliyo ya Kimungu, na watu wa shetani hufanya ya kishetani!. Ukifurahia mambo ya kheri wewe ni mtu wa Mungu, kufurahia mambo ya shari ni ushetani!, hivyo wewe ni wa shetani!.
P
 
Kuna Mungu na shetani, Mungu ni mambo ya kheri na shetani ni mambo ya shari, kuna watu wa Munghu na kuna watu wa shetani!. Watu wa Mungu hufanya yaliyo ya Kimungu, na watu wa shetani hufanya ya kishetani!. Ukifurahia mambo ya kheri wewe ni mtu wa Mungu, kufurahia mambo ya shari ni ushetani!, hivyo wewe ni wa shetani!.
P
Zaburi 18:34
"Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba."

Hata hivyo unaweza soma sura nzima Zab 18 | Biblia SUV | YouVersion
 
wewe uko upande gani?
Kuna Mungu na shetani, Mungu ni mambo ya kheri na shetani ni mambo ya shari, kuna watu wa Munghu na kuna watu wa shetani!. Watu wa Mungu hufanya yaliyo ya Kimungu, na watu wa shetani hufanya ya kishetani!. Ukifurahia mambo ya kheri wewe ni mtu wa Mungu, kufurahia mambo ya shari ni ushetani!, hivyo wewe ni wa shetani!.
P
 
wewe uko upande gani?
Mkuu Siko, Scott junior, kwa vile wewe ume join jf Mar 24, 2022, utakuwa hunijui mimi, mimi humu ni mmoja wa wana jf very few ombao tuko very truthful, very objective, tuko impartial na tuna balance mambo.

Kiongozi akifanya mazuri, tunamsifu na kumpongeza, siku akiboronga, tuna mbananisha. Hizi ni sifa za watu wa Mungu.

P
 
Back
Top Bottom