Ushauri: BBC, CNN, VOA au Aljazeera, mumuhoji Erick Kabendera juu ya madai yake kuwa Magufuli alimpiga risasi Ben Saanane

Ushauri: BBC, CNN, VOA au Aljazeera, mumuhoji Erick Kabendera juu ya madai yake kuwa Magufuli alimpiga risasi Ben Saanane

Huu ndio ushauri wangu kwani naamini kupitia mahojiano ya aina hiyo, Kabendera ataweza kufunguka zaidi na maelezo yake yatasaidia watu kupata picha halisi juu ya tuhuma hizi.

Sitegemei ataweka hadharani kila kitu kwasababu inaweza kusababisha ushahidi ukaharibika /kuharibiwa hasa ikiwa walioompa taarifa wako hai na mambo menginyo.

Lakini naamini itasaidia sana kutoa mwanga wa hili tukio. Hivyo, nashauri vyombo hivi vikubwa na huru vya habari vya kimataifa, vimuhoji na mahojiana hayo yawe live.

Ingekuwa ni katika nchi za wenzetu, hata media za ndani zingeweza kumuhoji. Lakiini katika nchi zetu hizi za bara la giza, unaweza kumuhoji leo, halafu kesho ukaokutwa "unonino" ukiwa umeuawawa au ukiwa hoi taabani na hujitambui.
Sio rahisi kwa taasisi hizo kumhoji, kwani wana taratibu zao. Kwanza, hata wao wanafanya utafiti wao kujiridhisha kuhusu hoja husika. Pili, wanachukua tahadhari ya kuhoji jambo hadharani wasije wakaingia kwenye mgogoro na nchi husika na kulipa fidia kubwa kubwa!
 
Back
Top Bottom