Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 796
- 918
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
kwenye mada.....
Hivi karibuni kumeibuka mjadala mkali juu ya kilichotokea jimboni kisesa ilipokuwapo ziara ya Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.
Watu wengi, pengine ni uelewa mdogo, wanauliza kwanini Mhe, Raisi alimjibu vile Mpina. Naomba nitumie jukwaa hili kuandika kwa wino mwingi kwamba alichokipata mpina ni stahiki yake na Raisi hajakosea lolote.
Kwanza amefanya unafki wa kisiasa.
hata mimi nilishangaa mpina alivyopongeza treni letu la nishati ya umeme. Nikajiuliza alikuwa wapi siku zote? ingawaje sio kosa kulisema hilo kwa jana lakini, politicaly inadelay au kuzorotesha popularity ya chama.
Mwenyekiti kamjibu vyema tu, afuate taratibu husika aache kuvunja kanuni na taratibu anazozipigania kila siku.
Mpina ni kama mtoto mdogo, haridhiki na nyumbani, ana kazi ya kulinganisha makochi ya nyumbani kwao na kwa jirani.
Wananchi wa kisesa wanashangilia changamoto lakini pia haohao hawajashangilia mafanikio yalipotajwa na Mpina.
Maana yake ni kwamba watu wa jimbo la Mpina wanapenda kuona spana zikitembea badala ya chochote.
Haya yote yanasababishwa na Mpina mwenyewe kashindwa kumjengea mazingira mazuri ya kisiasa mwenyekiti wake jimboni halafu anajidai kumnadi kwa ajili ya mwezi oktoba.huu ni unafki wa hali ya juu.
Ili chama kishinde uchaguzi bas kinahitaji cooordination na forged unit, Mpina hatambui hili badala yake anamuonea wivu Lissu anavyopashana na Mwenyekiti ama Raisi kimantiki majukwaani, so akiona changamoto kama za sukari basi anachangamkia fursa za kina Lema na Heche ili naye aonekane anaweza kuparurana.
Anaingia kwenye mtego wa Chadema kuwataka wana CCM kukikosoa chama chao kichwakichwa ili kikose ushindi akidhani ataitwa shujaa kumbe anaua juhudi za chama.
Kama Mpina anatamani kuzungumza madhaifu ya chama chetu majukwaani basi, jukwaa stahiki halipo ndani ya CCM.
MY TAKE !.
Mpina ni mtoto wetu ametunyea mkononi.
Ameonesha kuwa na ushawishi mkubwa jimboni kwake, hii maana yake ni kwamba Mpina anatufaa kwa kukamatia kura mwezi oktoba.
Tukifanya kosa la kumkimbiza inawezekana kabisa tukapata wakati mgumu kwa sababu hatuna uhakika na atakaekuja ukizingatia mwaka huu kutakuwa na ushindani mkubwa sana. Tukiweka mtu dhaifu tukamtupa Mpina inawezekana kabisa upinzani wakasimamisha kichwa cha jini ukanda ule, matokeo yake tutapoteza kura za mbunge na za Rais.
Lakini akigombea Mpina mwenyewe, tutapata kura za mbunge. Haiwezekani Mbunge ashinde kwa kishindo halafu Rais akose kura katika jimbo hilohilo. Waacheni wananchi wapige kura kwa Mpina kwani Mpina akipita Ndo Samia atapitia humohumo.
Mwisho, wazee wa busara wamwambie Mpina aombe radhi kwa chama chetu mbele ya waandishi wa habari, awaambie watanzania kuwa hakuwa na nia mbaya katika harakati zake za kuishauri serikali, hivyo taswira iliyojengeka juu yake kukidhoofisha chama ni taswira ambayo hakuitegemea.
Pia ufanyike mkakati Mpina apelekwe kupata chakula cha jioni na Mhe, Raisi ili kuondoa tofauti zitakazotuletea joto ndani ya chama kuelekea uchaguzi hapo Oktoba.
Yusufu R H Sabura
[email protected]