Ushauri bure kwa Kesi yoyote ya Madai au Jinai

Ushauri bure kwa Kesi yoyote ya Madai au Jinai

Sawa kaka ni kesi yenye makosa mawili kula njama na kutenda wizi sasa na hli LA kutenda wizi je adhabu yake ipoje kisheria

Sent using Jamii Forums mobile app

adhabu za makosa ya wizi zimeorodheshwa ndani ya sura ya xxvii ya sheria hizo za kanuni za adhabu namba 16 adhabu yake inaweza kua miaka 10, 15, 14, 7 tokana na kosa lenyewe.
 
Kwanini tunapoteza mda na resources kuendesha kesi katika mahakama za chini kisha hakimu anasema hautakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hii haina nguvu kisheria kusikiliza kesi yako,swali langu kama mahakama haina nguvu kisheria kwanini imefunguliwa pale huku wakijua mshitakiwa hatakiwi kujibu chochote kwanini wasingeifungua moja kwa moja kwenye mahakama husika?
Good question, hii kitu nami inanishangaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ntajaribu mkuu, but hivi vitu vinakatisha tamaa, mfano nimejitolea tu hapa kushauri watu bure lakini wameibuka watu wengine hao na kuanza kuaribu uzi utadhani hapa mim labda nalipwa.
Hata mm nimeshangaa badala ya kukusaidia wao wanakupinga, tena kwa kebehi
Wengine hatujui sheria hivyo kupitia hapa tunajifunza, wao walipaswa washauri pale ulipokosea au waanzishe maada wadau tutakuja na maswali yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je hati za kiwanja cha Makazi au shamba zinazotolewa na serikali za mitaa zinakua valid mahakamani?

Sent using Jamii Forums mobile app
hakuna hati inayotolewa na serikali za mitaa, haziwi valid, na hakuna sheria inayowaruhusu hao watu wa mitaani kutoa hati, hati zote halali ni zile zinazotolewa na wizara ya ardhi moja kwa moja au kutumia ofisi za almashauri ambao hao wizara ya ardhi wameelekeza maombi ya hati za umiliki viwanja vinatolewa, sheria inatambua baraza la ardhi la kijiji ndio angalau litatoa hati miliki ya kiasili (Customary Right of Occupancy) kwa ardhi ya kijiji.
 
Uko vzr
well, mkuu swali zuri sanaa, kisheria hiko hivi, kuna makosa ambayo yanapelekwa mahakama kuu tu kama mauaji, uhaini, ufisadi wa pesa kubwa na madawa ya kiasi kikubwa lakini pia nyara za serikali, sasa makosa haya yote ni jinai, na kwa mujibu wa sheria za jinai hakuna kesi yoyote itakayopelekwa mahakama kuu moja kwa moja pasipo kupitia mahakama ya wilaya au hakimu mkazi, lengo na maudhui ni kukamilisha ushahidi na utaratibu wote utakao tumika mahakama kuu.

kwaio utaona mshtakiwa anaambiwa na hakimu kua "mshitakiwa mahakama hii haina uwezo wa kusikiliza kesi hii, hapa imekuja kwa maulizo na hautopaswa kusema chochote",,, sasa akishaambiwa hivi upande wa mashtaka/jamhuri utamsomea orodha ya mashahidi watakao toa ushahidi wao mahakama kuu, utamsomea vile vile vizibiti vitakavyotumika kama ushahidi, hatua hii kisheria huitwa PI-Preliminary Inquiries, then wakimaliza utaritibu huu, file linachukuliwa kama lilivyo linapelekwa mahakama kuu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa rasmi.

sasa kisheria ktk masikilizo ya kesi yoyote ya jinai ni lazima kuwe na masikilizano ya awali ambayo huitwa Preliminary Hearing ambapo hii ina dhima ya kusave muda ambapo kuna vitu mshitakiwa ata vikubali na havitazungumziwa tena kwenye kesi na kuna document hapa inaitwa Memorundum of agreed facts itasainiwa na mshitakiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hakuna hati inayotolewa na serikali za mitaa, haziwi valid, na hakuna sheria inayowaruhusu hao watu wa mitaani kutoa hati, hati zote halali ni zile zinazotolewa na wizara ya ardhi moja kwa moja au kutumia ofisi za almashauri ambao hao wizara ya ardhi wameelekeza maombi ya hati za umiliki viwanja vinatolewa, sheria inatambua baraza la ardhi la kijiji ndio angalau litatoa hati miliki ya kiasili (Customary Right of Occupancy) kwa ardhi ya kijiji.
Shukran sana mkuu, nitakuja na maswali mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaonekana kasoma law, ila kashindwa kuwa Wakili kwa sababu aidha kafeli Law School au kafaulu ila akanyimwa uwakili kwa sababu ya misconduct, au hajaenda law school kabisa kwa kuwa n masikini na hana hela. Kati ya hayo ni majibu.


Kimaadili, Wakili hawezi Ku behave kama huyu na kimsingi, kuna kupingana kwa hoja ila kuna namna bora sana ya kupinga na siyo kama anavyofanya Hutu.

Ana stress fulani
nikweli usemacho kaka angu
 
Habari Mkuu. Kama mtu anakudai, let say shilingi 100, na umeshalipa asilimia 60 ya deni. Jee akifungua kesi mahakamani , kuna uwezekano wa kufungwa? Au mahahakama inakuwa na uamuzi wa aina gani? Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unacho takiwa ni kulipa kama umeptliza muda mahakama inaweza kumuaward mdai wako kwa ww kutoa fyn kufungwa haiwzkan unless ukatae kulpa kwa maksudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndivyo walivyo wanadamu.
Mkuu sheria inasemaje pale inapotokea polisi wanataka kupekua nyumba ya mtu, na baada ya kumaliza Kupekuwa wanawajibika kufanyaje ?

Na unapokamatwa n'a polisi inatakiwa kisheria ndani ya muda gani wawe wamekuchukua maelezo ? na inapotokea ktk maelezo uliyoyatoa polisi ukagundua siku yanaposomwa mahakamani kuna kitu kimeongezwa, Je inatakiwa ufanyaje ili mahakama ijue kuwa kuna uchakachuaji ktk maelezo yk uliyotoa police,

KWA FAIDA YA WOTE,
 
Mkuu nilijaribu kumwelewesha bila kunielewa.
Majibu yake yakutaka kujua utimamu wa akili zangu ndiyo ulionipa doubts ya sheria alizosoma achilia mbali mapungufu ya ushauri anaotoa.

By the way sikufanya hivyo kwa nia ya kuharibu uzi wake na kumshambulia mtoa mada personally bali kwa lengo la kumsahihisha kidogo na atoe ushauri mzuri kwa walengwa wake .
Katika ethics za kisheria ww pter ndo unakosea, unakuwa na hisia za hasira kisa tu kupingwa na kusema amesoma za Libya. Law is about argument.

Jaribu kusoma RULING za HC pale ambapo kuna dissenting opinion or conflict decision of the same Court horizontally.

Plz use Legal language to challenge ur fellow learned member of the bar.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hii ndiyo tafsiri sahihi ya kanuni ya 31(1)
Sivyo alivyokuwa analazimisha nakuanza kuleta kejeli za kitoto.
Mkuu, 666 chata "HAPO HAKUNA UKOMO"

Wakati wa kuomba Mirathi hutegemea na marehemu alikufa kwa kuacha wosia (testacy) ama bila wosia (intestacy). Sasa wakt wa kufungua MIRATHI huwa kuna nyaraka zinaambatanishwa, ambazo pamoja na mambo mengine ni:-

1. Mhutasari wa wanaukoo au wosia
2. Cheti cha kifo kutoka RITA
3. fomu za mirathi ikiwa imejazwa sahihi
4. Ada ya mahakama n.k

Vitu hv vinatakiwa ndani ya miezi 3. Sasa kanuni ya 31 inaweka mazingira kuwa endapo mtu hataleta hv vitu ndan ya miaka 3 basi aongezee (i.e 5. hapo juu) maelezo ya kwa nn amechelewa zaidi ya miaka 3. Akiambatanisha tu maelezo basi kesi inafunguliwa. Na maelezo hayo sio extension of time kama ilivyo kwny torts (3yrs), contract (6yrs) , land (12yrs), Fatal accident 6 months) n.k

So naungana na PTER kuwa hakuna ukomo ili kuna kuongeza nyaraka baada ya miaka 3 kupita.

NB: Sheria hupendeza sana kutoa hoja na supporting authority (section of law or precedence)View attachment 1029965

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii rule wakili inakuchenga jaribu kuisoma kwa utulivu uielewe.
Kwenye petition for probate or letters of administration hatuna time limitation.
Kumbuka time limitation is a bar to jurisdiction lakini kifungu hicho kinatoa mwongozo tu wa nini kifanyike ikiwa muda wa miaka mitatu umepita.
Unless hiyo sheria unayoitumia wewe siyo tunayoijua sisi
mkuu nimeona hata na wewe hapa nisikuache hivi hivi, naomba nikueleweshe kuhusu hio kanuni uliyo i quite na hayo maelezo yako, hahahaha, ni kwamba kanuni ya 31 inatumika kwenye kufanya application upya kabisa endapo mtu atakua kachelewa kufanya application baada ya miaka mitatu, na sio et akichelewa kuleta izo barua sijui vyeti rita hahaha, soma ata marginal note hapo, alaf rule hio iko ndani ya sehemu ya sita ambayo ina husu taratibu za mtu kua granted letter/probate, lakini sijui ata unaitafsiri vipi rule 31(1) mbona iko very clear, ivi ukiisoma hii rule inaendana na iki ulichokiandika hapa? really?.... anyway its hard to point a finger to a lawyer if your one among of them,,, lakini interpretation of law hua ni tatizo kubwa sanaa kwa wanasheria wengi. hivi mkuu ni petition gani itapokelewa mahakamani endapo ikiwa haina ivyo vitu vinne ulivyovitaja? so unataka kuniambia wewe mwanasheria unaweza kufanya application ya probate ikiwa na will na zile forms tu labda alaf mahakama ikapokea ikawa inakusubiri wewe ndani ya miaka mitatu uvilete ivyo vitu then ndio iendelee? really? mahakama gani hio?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu naombeni msaada wenu...niliianzishia Uzi hii ishu ila naona INA views zaidi na mia ila replies ni zero. Naombeni msaada wakuu

Mimi ni mgeni kabisa katika hili jukwaa la sheria na limefika hapa baada ya kutatizwa na hii kitu inayojulikana kama mgongano wa kimaslahi au conflict of interest kwa kimombo. Naomba niende kwenye mada moja kwa moja.

Kuna makubaliano ya uchimbaji wa Madini ya Dhahabu nataka kuingia na Jamaa Fulani hivi, basi katika mkataba huo wakaweka sehemu ya mgongano wa kimaslahi. Katika vipengele vyake kikawepo kimoja ambacho ndo kinanyima Amani Kabisa. Kinasema "Mbia Namba moja (ambaye ndo Mimi) hataruhusiwa kuchimba Dhahabu katika eneo la masumbe au kuwa na hisa ya uchimbaji na mtu yoyote katika eneo hili, pia hatatakiwa kuchimba wala kuwekeza katika uchimbaji katika Wilaya ya KAHAMA kwa kipindi chote cha mkataba huu". Jambo la kusikitisha sana ni kwamba hawataki niwe Mwanachama katika maduara yao ila nina gawio la 10% katika faida itakayopatikana kutokana na uchimbaji tunaofanya.

Sasa wakuu kitu ninachoomba kujua Kutoka kwa wanasheri, je hii kitu ya conflict of interest inatambuliwa na sheria Zetu? Na je application yake inakuweje? Je hiki hawa Jamaa zangu wanachong'ang'ania kibakubalika kisheria?

Kuna Jamaa yangu lawyer nimeongea Naye akaniambia inatakiwa tu ku-declare kwao kuwa nafanya pia Biashara inayofanana na Biashara tunayotaka Kufanya pamoja na si vinginevyo, Je hii ni kweli wakuu Wangu.

Naomba mnisaidie nguli wa sheria maana naona kama mkataba huu unaenda kunifunga pingu kwenye utafutaji Wangu maana shughuli zangu nyingi zinahusisha uchimbaji wa Dhahabu hasa hasa Kanda ya Ziwa.

Naomba msaada wenu wakuu
 
Nimependa ushauri wako. Sasa na Mimi naomba msaada wa kisheria. Nina mdeni wangu namdai 600,000 tangu novemba 2017. Mpaka sasa nikimdai anasema atanipa. Deni lenyewe ni kuwa tuliuziana mali halali, akanilipa inakabaki hiyo balance ila hatukupeana muda maalumu wa kumaliza malipo. Swali, naweza kumpeleka Mahakamani na akalazimishwa kulipa? Je ni mahakama ipi? Ya mwanzo au ya Wilaya. Je, lazima nifungue kesi katika mahakama ya mahali tulipofanyia mauziano? Au mahakama ya popote ambapo ni convinient kwangu kuhudhuria? Naweza kumdai riba na gharama za kuendesha kesi?
 
Back
Top Bottom