USHAURI DOCTORS:Huyu mama kashika ujauzito akiwa na mshono miezi 11(alijifungua kwa operation c-section)

Job Richard

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
3,876
Reaction score
2,190
Doctors au aliyewahi ku experience hii kitu msaada wa ushauri kabeba ujauzito mtoto aliyepo ana umri wa miezi 11 je tumbo litaweza kuhimili ujauzito mwingine? Binafsi nikashauri labda zile njia nyingine LAKINI KAGOMA KABISA NAMI NIKIJIULIZA KUHUSU MSHONO ALIOFANYIWA OPERATION NAONA BADO MIEZI 11 TOKA KUJIFUNGUA NI MICHACHE SANA naomba ushauri kwake kwa afya ya mtoto huyu mwenye miezi 11 hana shida labda je aendelee kunyonya au ni kumwachisha kadai anakula vizuri tu
 
Nenda moja kwa moja kamuone dakitari hiyo itakusaidia kuliko kumsuburi humu.. wakati watu wako chitchat MMU
 
hata wewe kama una lolote liweke mkuu
Aende hospital akaonane na daktari ndio anaweza msaidia zaidi coz atamuona mhusika moja kwa moja lakini sisi humu tutakufariji kwa maneno hatumuoni mhitaji msaada kwa karibu.
Asante.
 
Asanteee mkuu
 
Usimwachishe mtoto hadi atakapokaribia kujifungua ndo amwachishe yaani mwezi 1 kabla, pia asihofu atajifungua Salama tu kikubwa asifanye kazi ngumu na awahi hospital
 
Mungu ni mwema atajifungua salama na asimuachishe mtoto mpaka mimba itapotimiza miezi 6.

Kwa ushauri zaidi ungeenda kumuona Gyno.

Next time muwe makini jamani msifanye mchezo na afya
 
Doctors au aliyewahi ku experience hii kitu msaada wa ushauri kabeba ujauzito mtoto aliyepo ana umri wa miezi 11 je tumbo litaweza kuhimili ujauzito mwingine? Binafsi nikashauri labda zile njia nyingine LAKINI KAGOMA KABISA NAMI NIKIJIULIZA KUHUSU MSHONO ALIOFANYIWA OPERATION NAONA BADO MIEZI 11 TOKA KUJIFUNGUA NI MICHACHE SANA naomba ushauri kwake kwa afya ya mtoto huyu mwenye miezi 11 hana shida labda je aendelee kunyonya au ni kumwachisha kadai anakula vizuri tu
Mkuu, kuwa na amani, ushauri wangu
1. Hiyo mimba ya ya sasa itakua vizuri tu, azingatie taratibu zote za mama mjamzito, i.e kwenda kliniki, kutumia dawa za folic acid, madini chuma, dawa za kinga ya malari (muda ukifika), kula vizuri na kupumzika.

2. Mtoto wa sasa asiachishwe kunyonya, anyonyeshwe na kupewa vyakula vingine kama kawaida. Pia baba na mama onesheni mapenzi na ujirani kwa huyu mtoto.

3. Wakati wa kujifungua ukifika, daktari apewe historia kamili, sababu kitaalam huyo mama hashauriwi kujaribu kusukuma, hivyo ni salama zaidi akifanyiwa C section tena hata kama sababu za Csection za mtoto wa kwanza hazipo kwenye hii mimba ya sasa.
 
Pole sana. Jibu sahihi ni hili: NENDA HOSPITALI, ONANA NA DAKTARI WA AKINA MAMA, ATAKACHOKUSHAURI TEKELEZA BILA KULETA UBISHI!

Wanandoa hasa akina baba, tuwe makini jamani, tuwe wavumilivu ktk kufanya tendo la ndoa, Mishono inawaumiza sana akina mama!

Poleni!
 
Awahi kliniki amweleze dr.hali halisi,ujauzito wake utakua vizuri tu Wakati wa kujifungua ni vizuri achague oparetion ndio njia salama zaidi,kuhusu mtoto anaweza kuendelea kunyonyesha lkn mama ni sharti ale msosi wa maana na baba uonyeshe support ya nguvu
 
Asante sana nashukuru sana hata daktari kashauri hivyo hivyo blessed much
 
Awahi kliniki amweleze dr.hali halisi,ujauzito wake utakua vizuri tu Wakati wa kujifungua ni vizuri achague oparetion ndio njia salama zaidi,kuhusu mtoto anaweza kuendelea kunyonyesha lkn mama ni sharti ale msosi wa maana na baba uonyeshe support ya nguvu
Asante sana mkuu
 
Pole sana. Jibu sahihi ni hili: NENDA HOSPITALI, ONANA NA DAKTARI WA AKINA MAMA, ATAKACHOKUSHAURI TEKELEZA BILA KULETA UBISHI!

Wanandoa hasa akina baba, tuwe makini jamani, tuwe wavumilivu ktk kufanya tendo la ndoa, Mishono inawaumiza sana akina mama!

Poleni!
asante sana mkuu kaweza kuwaona kashauriwa vizuri sana kama wadau humu baadhi
 
Mungu ni mwema atajifungua salama na asimuachishe mtoto mpaka mimba itapotimiza miezi 6.

Kwa ushauri zaidi ungeenda kumuona Gyno.

Next time muwe makini jamani msifanye mchezo na afya
Asante sana mkuu nashukuru kaweza kuwaona wameshauri vizuri sana
 
Heri wewe ana miezi 11, kuna mmoja alipata baada ya miezi 3 na still akazaa vizuri kwa operation ya pili ndani ya miezi 12.
 
Atajifungua tu mkuu! Kwa sasa aendelee kunyonyesha mpk anapokaribia kujifungua ila akae karibu na hosp na awe anamwona daktari mara kwa mara. Hiyo ilishawahi kunikuta
 
Mleta mada next time mtumie uzazi wa mpango uwe na huruma kwa mkeo, though atazaa salama ila kwa operation na inabidi awe karibu na Dr ili awahishwe operation. Namhuhurumia huyo mama operation inauma balaa maana kidonda kwa ndani kinachukua two years had kupona tena kwa wafanya mazoezi. Nyie kuwe karibu na ma gyno had atakapojifungua
 
Back
Top Bottom