Hellow!
Katika Taasisi mbalimbali zitoazo huduma za kibenki na Taasisi zingine za Serikali na binafsi, watumishi huvaa vitambulisho shingoni vyenye Majina Yao Ili kumpa nafasi mteja Kutoa malalamiko au kudai HAKI yake ambayo anaona imepokwa au kudhulumiwa na mtoa huduma.
Tukirudi kwenye sekta nyeti ya Afya, baada ya kuona ajira kwenye sekta ya Afya pana ajira za uhakika, wahuni nao wameingia wengine Kwa RUSHWA wengine Kwa uwezo darasani ila hawana wito, Wala HOFU ya Mungu Wala huruma Kwa binadamu wenzao, wanatoa huduma viwango vya chini sana. Yaani daktari yumo chumba Cha stroke unit na wagonjwa serious apasao kuwaangalia, Yeye anachat na kuvinjari mitandao ya kijamii muda wa KAZI, wengine hawafanyi KAZI zao Hadi wabembelezwe!
Sasa nimepokea malalamiko tokea vyanzo vyangu kuhusu hospitali nyingi za Serikali yetu hawana vitambulisho, sasa kuanza kumuuliza Jina mhudumu au daktari aliyempora nduguyo HAKI ya uhai Si Rahisi, ingekuwa Rahisi kama wangekuwa na vitambulisho vya kuvaliwa shingoni.
Namaanisha hospitali zote za Serikali ngazi zote kuanzia kata ,wilaya, mikoa ,majiji, Kanda Hadi rufaa, wote wavae ID.
Hii itasaidia sana ikiwa mwananchi ambaye ndiye mwajiri wa mtoa huduma, akitaka kumfuata KAZI mhudumu muhuni, katili asiye na utu kujali wagonjwa iwe Rahisi kufutwa KAZI.
Yaani kupoteza KAZI Kwa nurse au daktari mzembe, katili iwe Rahisi kama kumfuata KAZI polisi asiye na maadili.
Uhai ni zawadi aliyotupa muumba wetu tuutunze na kuuthamini.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Nawasilisha.