Ushauri: EAC ipitiwe upya - Kenya aondolewe uwanachama kwa vurugu au Tanzania ibaki na SADC tu iachane na EAC

Ushauri: EAC ipitiwe upya - Kenya aondolewe uwanachama kwa vurugu au Tanzania ibaki na SADC tu iachane na EAC

Kimbesa11

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2015
Posts
4,648
Reaction score
2,706
Mwaka 1977 jumuia ya Africa mashariki ilikufa lakini msababishi alikuwa ni huyuhyu anayeleta vurugu Leo,
Sioni haya ya kuwa na regional integration ambayo Haina Tija ambayo inaendesha harakati za vurugu ndani ya jumuia.

Ni vema juumu Kama Taifa tuangalie hili swala huku tukikumbukua kuwa Tanzania yetu ni kubwa kuliko jumuia ya Africa mashariki
 
Hili ni wazo.... Ni kama Kenya inatumika kuivuruga Tanzania na washajua ushamba wa vijana wa Tz ni kuyaburuza tu kupitia mitandao yatafuata. Siku yakija kuamka nchi iko hovyo than ever wakidhani yupo mwanasiasa ataathirika

Vikao vyote na mipango ya pioners ilifanyikia huko....
 
Wakenya ndio marafiki wakweli wa Tanganyika ila ni maadui wa mafisadi,ccm na wauwaji.

Kenya ndio nchi pekee afrika mashariki yenye uhusiano wa damu na Tanzania kwasababu inamakabila mengi yaliyopo pande 2

Wananchi wakitanganyika wanawapenda sana wakenya ila haya majambazi yanayoibia nchi ndio wanaleta hizi propaganda mbaya dhidi ya Kenya.

Wakenya ni marafiki na ndugu wazuri wa watanganyika kuliko wanzazibar,bora tuungane na kenya kuliko kuungana na Zanzibar

Wakenya wamepaza sauti kubwa Dunia huko wakati ndugu zao watanganyika wamezimiwa mitandao na kuuwawa..tunawapenda wakenya
 
Mbona zamani Kenya HAKUa mchonganishi Hadi aje Leo? Moto mnaopuliziwa matakoni si wakitoto hashahahaaaa dadeki
 
Adui wa Tanzania ni Wizi wa kura,Ufisadi na matumizi ya fedha yasiyo na tija (Ripoti ya CAG),Ajira au Nafasi/Teuzi za Upendeleo, Undugunization na Ufamilia,Uchawa,nk hawa ndiyo adui wa Taifa letu SIYO Kenya!🙌🙌
Vipi Report ya Waangalizi kutoka SADC kuhusiana na Uchaguzi huu ambao "The horse ran on its own and Won"! ilisemaje?
Tumeambiwa Uchaguzi ulirahisishwa!
 
Kenya ndio rafiki na ndugu wa kweli wa Tanganyika.

Wakati watanganyika wanapigwa risasi na maiti kutupwa barabarani takribani siku 3 wakenya hawakuchoka kuripoti yote yaliyokua yakiendelea huku vyombo vya unafiki[ sio habari] vya Tanganyika vilikua busy kusoma matokeo feki ya kura feki na uchaguzi feki.

Kenya ndio ndugu wa mtanganyika wa kweli, Kenya kuna wajaluo, wakurya[wakuria] , wamaasai kama ilivyo Tanganyika ila Zanzibar hakuna kabila hata moja linaloshahabiana na mtanganyika.

Propaganda hii imefeli.
 
Back
Top Bottom