Ushauri: Familia ya Sativa ikatae Msaada wa Matibabu uliotolewa na Rais Samia, msaada huo ni kejeli

Ushauri: Familia ya Sativa ikatae Msaada wa Matibabu uliotolewa na Rais Samia, msaada huo ni kejeli

Ni kweli kwamba Watanzania kutokana na hali zao duni za kipato wanahitaji msaada wa hali na mali, lakini uduni huo usiwapelekee kudhalilishwa

Naishauri familia ya Sativa kukataa kabisa msaada wa matibabu ya kijana wao uliotolewa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Hii ni kwa sababu serikali anayoiongoza ndiyo inayotuhumiwa kutaka kumuua huyu kijana huku polisi wakihusika moja kwa moja (Hawajawahi kukanusha)

Hakuna kauli yoyote ya serikali kwenye jambo hili, hii maana yake ni kwamba SERIKALI NDIYE MHUSIKA MKUU WA JAMBO HILI la kinyama, na kiongozi wa serikali hiyo ni Samia Suluhu, Kupokea msaada wake itakuwa sawa na kumkufuru Mungu aliyemponya kijana huyo kuliwa na fisi kama watekaji wa serikali ya Samia walivyotaka

Nashauri wanaharakati waendelee kutengeneza mpango wa kuchangia matibabu kama walivyoanza tangu mwanzo.
Ila kwa Tundu Lissu na Prof. Jay kupewa msaada na Mama na wakaupokea ilikuwa sawa. Wahenga walisema "Ukiwa kijana ukawa mnafiki, ukizeeka utakuwa mchawi"!.
 
Siku zote ukweli ndiyo humpa ujasiri msemaji.

Ni uhayawani, ushetani na unyama wa hali ya juu. Watu wako waamue kitaka kumeua mtu, halafu baada ya Munhu kimnusuru, wewe badala ya kuwaadhibu waliohusika (kama wewe huhusiki na hukuwatuma), unasema eti itamtibu aliyenusurika.l!
First, chase the fox away then you..........!
Tatizo huyajui mambo kutokana na umri wako mdogo.
 
Hii issue ipo complicated sana, upande mmoja kuna suala la matibabu ya mgonjwa apone hili ndio la muhimu zaidi kwa sasa.

Upande wa pili tuwafahamu watekaji, au hata kama wakiendelea kuwaficha basi Rais ajitokeze hadharani kukemea utekaji unaofanywa, kwa Sativa ndio iwe mwisho, inatosha sasa.

Haya yote yatafanikiwa endapo patakuwa na maelewano ya pande zote husika, mazungumzo yafanyike kwa amani na upendo baina yao, ili mwisho wa siku uhuru wa mtanganyika urejee.

Lakini mihemko ya aina yoyote ikiwemo ya kisiasa kwenye hili suala ndio itazidi kuharibu kila kitu, na mojawapo ya mihemko hiyo ni kurudisha pesa alizotoa Rais kwa matibabu, kwanza kwanini zirudishwe ikiwa ni pesa zetu walipakodi? sio za Samia zile?

Lakini kama zikirudi, basi naamini kabisa hicho kitendo itakuwa ni sawa na kumwagia moto petrol, utazidi kuwaka, na tutakaoungua ni sisi tusio na silaha za kujitetea.

Nashauri familia ya Sativa sasa iachwe iamue masuala ya matibabu ya kijana wao, hata kama tuliwasaidia michango, isiwe sababu ya kuingilia maamuzi yao wachwe huru wale sio wanasiasa.
 
Kama Lissu na wengine wengi wamekuwa wakipokea msaada wa matibabu kama huo, Sativa ni nani hadi akatae?? Punguza wivu mwache mtoto akatibiwe au unataka afe?
Lissu alishawahi kupewa msaada wa matibabu na huyo mama yako?
 
Huko x wamepaniki hawataki msaada.

But it's better waache Mheshimiwa amtibie, she's a President
 
Achen siasa kwenye matibabu ya menzenu Mkuu. Pamoja na yote serikali pia ikiamua kuwadindia sijui itakuaje. Kwasababu inaenda kwenye matibabu acheni atibiwe apone, huku mukiendelea kuishinikiza serikali iwatafute hao watekaji na kama ni wao wajisahihishe.

kwenye matatizo ni vyema kusahau tofauti zetu zote na kushirikiana wakati tukiendelea kumtafuta Mchawi
Umeandika kinafiki sana
 
Ushauri ni kwamba familia ikubali misaada toka kwa kila mtu ilimradi hali ya kijana iimarike..ikiwezekana wawapige marufuku watu wote wanaojihusisha na siasa kumtembelea mgonjwa .. tena waanze na Chadema
 
Ni kweli kwamba Watanzania kutokana na hali zao duni za kipato wanahitaji msaada wa hali na mali, lakini uduni huo usiwapelekee kudhalilishwa

Naishauri familia ya Sativa kukataa kabisa msaada wa matibabu ya kijana wao uliotolewa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Hii ni kwa sababu serikali anayoiongoza ndiyo inayotuhumiwa kutaka kumuua huyu kijana huku polisi wakihusika moja kwa moja (Hawajawahi kukanusha)

Hakuna kauli yoyote ya serikali kwenye jambo hili, hii maana yake ni kwamba SERIKALI NDIYE MHUSIKA MKUU WA JAMBO HILI la kinyama, na kiongozi wa serikali hiyo ni Samia Suluhu, Kupokea msaada wake itakuwa sawa na kumkufuru Mungu aliyemponya kijana huyo kuliwa na fisi kama watekaji wa serikali ya Samia walivyotaka

Nashauri wanaharakati waendelee kutengeneza mpango wa kuchangia matibabu kama walivyoanza tangu mwanzo.
Huyu dogo akipata washauri wazuri anapata Uraia wa moja kwa moja Katika nchi za ulaya, Marekani au Australia. Kama amesoma degree afuate ushauri huo. Akifika kule anaanza kazi moja kwa moja na kuongezea la masters mdogo mdogo. Ila inawezekana akawa mzito kufikiri.
 
Angekuwa kaka yako ungeshauri ujinga huu?
Mh Rais ametenda jambo lililo jema saana, mistake kujinufaisha kisiasa na huyu Kijana
 
Ni kweli kwamba Watanzania kutokana na hali zao duni za kipato wanahitaji msaada wa hali na mali, lakini uduni huo usiwapelekee kudhalilishwa

Naishauri familia ya Sativa kukataa kabisa msaada wa matibabu ya kijana wao uliotolewa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Hii ni kwa sababu serikali anayoiongoza ndiyo inayotuhumiwa kutaka kumuua huyu kijana huku polisi wakihusika moja kwa moja (Hawajawahi kukanusha)

Hakuna kauli yoyote ya serikali kwenye jambo hili, hii maana yake ni kwamba SERIKALI NDIYE MHUSIKA MKUU WA JAMBO HILI la kinyama, na kiongozi wa serikali hiyo ni Samia Suluhu, Kupokea msaada wake itakuwa sawa na kumkufuru Mungu aliyemponya kijana huyo kuliwa na fisi kama watekaji wa serikali ya Samia walivyotaka

Nashauri wanaharakati waendelee kutengeneza mpango wa kuchangia matibabu kama walivyoanza tangu mwanzo.
hakika
 
Uzi ulitupwa sijui wapi, umerejeshwa ukiwa ushachakachuliwa!
 
Nafikiri umbali wa Dar - Katavi, ilitumika ndege au gari?
* Watu wangekuta maiti kule wangedhani alikuwa muwindaji haramu?

* Watu wangekuta maiti yake wangejua ni jambazi lililopigwa risasi likiwa ktk unyang'anyi?

* Waliomteka huenda walikuwa ktk OP kanda ya Katavi - So, wkt wakienda huko ndo walimbeba kisha wakashauriana kumwacha porini huko?

* Waliomkamata na kumhoji walipata taarifa za konekisheni ya uhalifu wa Sitiva, kwa HIYO kuna genge ambalo anafanya nalo kazi huko sasa alipofika kule aligoma kutoa ushirikiano ndipo wakaamua kumdhuru?

"TUKIO LA SITIVA LINAACHA MASWALI KIBAO - SIDHANI IWAPO YEYE MWENYEWE YUKO TAYARI KUSEMA YANAYOFANYA AFANYIWE HIVYO". ILA UKWELI WANAUJUA WAO
 
Lakini si tumekuwa tukiambiwa kwamba haya mambo ya kutekana tekana hayapo tena, yaliishia kwenye ile awamu iliyoitwa na akina Zitto kwamba ni ya kishamba??
 
Huko x wamepaniki hawataki msaada.

But it's better waache Mheshimiwa amtibie, she's a President
Haya yote yasingetokea kama uzi huu ungeachwa tangu day 1, niliandika karibia yote yanayojadiliwa leo kila mahali, lakini Mtukufu Moderator akauondoa, nadhani ni kwa vile ulijaa ukweli mtupu, sasa kaurejesha ukiwa umenyofolewa minofu yote utadhani umeandikwa na Malasusa wa KKKT au Mufti wa Bakwata
 
Back
Top Bottom