Ushauri Gari yangu aichanganyi speed mwisho 60 tu!


Pole sana mkuu,nami nina toyota voltz nilishawahi kutana na tatizo kama hili nilihangaika sana mwisho wa siku tukagunfua kwamba kuna kitu kipo pale chini inapoanzia exozi kama kimtungi hivi kilikuwa kimeziba hope hata ww itakuwa tatizo ni hili.Huyu fundi alitafuta kile kifaaa tukakata na kuchomelea hicho kingine.wataalam wataongezea kinaitwaje.Pia kwa huko chalinze sizani kama hao mafundi wanautalaam huo mie nilibadilishia kwa azizi ali temeke kuna fundi anaitwa kikole ni mzoefu sana huyu jamaa
 
Mafundi bongo wanayengeneza gar kama wanapiga ramli
 
OK nashukuru mkuu ngoja nikusanye nguvu nije nayo Dar
 
hope utakuwa unazungumzia catalytic converter
 
Mkuu hilo tatizo lako lina tiba lkn maelezo yako bado hayajakamilika na kujitosheleza kwa mm kusema neno ambalo kwa upande wangu ninaloona ni sahihi..utengenezaji wa gearbox za automatic ni mrahisi sana na nimgum sana cha kwanza na cha mhim nikujua au tambua kuwa shida iko sehem gani..

Kwanza uzito wa gari una mambo mawili shida kwenye engine au kwenye gearbox yenyewe.
Unaweza vimba kichwa na kutunisha misuli unagangamala kutengeneza gearbox kumbe shida ipo kwenye engine..

Kama parformance ya engine ni kimeo usitegemee gari itaweza badili gia vizuri coz vitu vinakwenda kwa mahesabu..

Kwa ishu ya gearbox yenyewe nayo pia imegawanyika mara 2..kuna ishu ya umeme na ishu na mechanical ya gearbox yenyewe sasa hapo ndio kuna utamu..kutambua upande upi ndio wenye shida lkn kama ni fundi ni ishu ndogo sana..na ujinga wa gari karibia zote 99% za toyota unapima na mashine lkna no fault code lkn gari inashida tena kwenye mfumo wa umeme..

Kwanza ili kutambua kama ishu ni umeme au laa fanya hivi..endesha gari yako ki manually anzia gear river kwenye L unaendesha mpaka speed 20 au kabla haijafika 20 ipeleke kwenye 2 then iendeshe mpaka kwenye speed 35 au 40 then ipeleke gear river kwenye D angalia ubadilishaji wake upoje na ukiweka D moja kwa moja??. Kama ukifanya hivyo gari ikawa tofauti basi ikaleta mabadiliko basi shida ni upande wa umeme..maelezo mengine ni yakifundi zaidi nitakuchanganya sana nikikwambia mambo ya SLT sijui SL1 na SL2 hotoelewa .

Mara nyingi gearbox za automatic huwa zinasumbua kwenye gear namba 1 huwa zinaunguza clutch za D gear namba 1.kuondoka inakuwa nzito .lkn kwa gear za kumalizia mfano upo speed juu ya 50 au 60 harafu gari inakuwa kama inajivua gear au weka free mara nyingi huwa seal za diaphram zinakuwa zimechoka zinapitisba pressure ya hydrolic..
 
Hahahahaha wanayaita MAKINIKIA mkuu hayo ni dili sana mafundi wengi wanaharibu magari ya watu kwa kuyanyofoa hayo makitu na kwenda kuyauza na wanapata bei nzuri sana mfano ya brevis akitoa na kwenda kuuza ni laki3 hahaha..magari ya europe ndio mpaka laki8 milion hukoo..
 
Nilichangia bila ya kusoma kichwa cha habari kwa shida hiyo hapo kama gari inachimba vizuri basi kuna mambo kama mawili hivi kama walifungua na kusafisha filter/strainer basi yawezekana ikawa valve chasi hapo walipofungua mwanzo waliikuta kwenye hali gani?? Au wafungue chasi wasafishe ..au kagua performance ya engine kuna mdau kashauri juu ya catalic converter pia nayo ni sababu yaweza pelekea janga hilo..

KARIBU JO AUTO TECH kwa msaada ushauri na matengenezo ya gari yako.ni wabobezi na mabingwa wa auto electrical na electronics..
 
Ofisi yenu iko wapi mkuu?
 
Mtaalam LEGE ofisi yako iko wap!?
 
Mafundi bongo wanayengeneza gar kama wanapiga ramli
Na wanatia watu hasara sana...mi niliambiwa gearbox imekufa kumbe ni matatizo ya sensor...
Mafundi washenzi sana...
 
Na wanatia watu hasara sana...mi niliambiwa gearbox imekufa kumbe ni matatizo ya sensor...
Mafundi washenzi sana...
Hahahahahahahaha mkuu siku hizi kuna mashine chungu mzima muwe mnaenda kwa fundi mwenye mashine awe anawapimia kabla ya kuanza kukolokochoa..

Ingekuwa vizuri kama gari yako inasumbua unaipima then kwa uhakika zaidi unaomba hapa ushauri wako ukiambatanisha na hiyo fault code yako ndio tungekuwa tunashauriana vizuri sana na kwauhakika na kujua je shida ya gari yako na hiyo fault nn kifanyike au badilishwe
 
Namba A haiweze kufika 100 chukua D uone moto wake
Mzee mimi nina Voltz namba A-inaenda mwendo wa ndege.DAR ARUSHA nakula wastani wa 7 hours tena nasimama njiani kusalimia watu na kununua machunga
 
Comrade
Nina gar yangu TOYOTA CAMI

Imekuwa nzito balaa kuchanganya moto
Halafu ina miss balaa

Na ukiwasha inatoa moshi mwingi unakata baada ya gari kuchanganya

Wiki iliyopita fund alibadili zile FUSE

Lakini naona shida imepungua kidogo
But, bado ipo
 
Mzee mimi nina Voltz namba A-inaenda mwendo wa ndege.DAR ARUSHA nakula wastani wa 7 hours tena nasimama njiani kusalimia watu na kununua machunga
Pole sana mkuu umejisumbua kweli kumjibu huyo?? Speed ya gari na namba ya gari kuna uhusiano gani
 
Pole sana mkuu umejisumbua kweli kumjibu huyo?? Speed ya gari na namba ya gari kuna uhusiano gani
Hawa ndo wale ambao wanauziwa gari ya mjapan namba D kwa bei mara nne ya gari kali ambayo injini inatoa ute kabisa wakinunua namba badala ya Gari
 
Hawa ndo wale ambao wanauziwa gari ya mjapan namba D kwa bei mara nne ya gari kali ambayo injini inatoa ute kabisa wakinunua namba badala ya Gari
Au kwakuangalia milage/kilomita za gari hahahahahahaha wakati zinashushwa hata mm pia kazi hiyo naifanya sana tuuu
 
Weak fuel pump..... Badili fuel pump halafu utaniambia. Local way ya kupima

Fungua kwenye kiti cha nyuma juu ya tank la mafuta waambie wachomoe running pipe na sio return pipe. Kisha ziba kwa mkono weka switch on. Pump mujarabu huwezi zuia kwa kidole.

Kama tatizo litaendelea angali throtal censor i mara chache plug ziwe na tatizo kama gari haina misi.
 
Mzee mimi nina Voltz namba A-inaenda mwendo wa ndege.DAR ARUSHA nakula wastani wa 7 hours tena nasimama njiani kusalimia watu na kununua machunga
Voltz number A uliingiza hapa Bongo mwaka gani mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…