Nomba ushauri gari yangu TOYOTA VOLTZ ugonjwa wake gari ni nzito nikapeleka garage za mtaani wakafungua gear box na kubadilisha hydrolic cha ajabu imekuwa ata afadhali na awali imekuwa nzito zaidi. Nomba mwenye kujua au mwenye kunishauri anisaidie ili niweze kujua namna ya kuweza kupata wataalamu wa uhakika ili nimalize hili tatizo. Mi nipo Chalinze Pwani.
Pole sana mkuu,nami nina toyota voltz nilishawahi kutana na tatizo kama hili nilihangaika sana mwisho wa siku tukagunfua kwamba kuna kitu kipo pale chini inapoanzia exozi kama kimtungi hivi kilikuwa kimeziba hope hata ww itakuwa tatizo ni hili.Huyu fundi alitafuta kile kifaaa tukakata na kuchomelea hicho kingine.wataalam wataongezea kinaitwaje.Pia kwa huko chalinze sizani kama hao mafundi wanautalaam huo mie nilibadilishia kwa azizi ali temeke kuna fundi anaitwa kikole ni mzoefu sana huyu jamaa