Ushauri: Gari zote ziondolewe vioo vya tinted Ili kuwabaini watekaji wasiojulikana

Twende hatua Kwa hatua,

Mambo yawe hadharani, pasiwepo na yeyote wa kujificha Kwa vioo tinted.

Tuzuie utekaji tu ila kama mtu akitaka kukuteka hata akiwa hana TINT anasepa na wewe mazima na unaweza kukalishwa kwenye kiti fresh halafu chuma imewekwa tumboni hakuna kutikisika.
 
Haitasaidia sana wat chini ama kukuvisha kinyago ama kukudunga sindano ya kaput
 
Jitahidi kupunguza ujinga

USSR
Mwalimu Nyerere alitumia gari isiyo na tinted.

Hilo Si jambo geni kufanyika Leo.

By the way ikiwa ninyi ni watu WEMA, kwanini mjifiche msionekane?
 
Hata gari za viongozi wakuu ziondolewe tinted.

Mwalimu Nyerere alitumia gari isiyo na tinted.

Mimi sioni sababu ya kiongozi wa umma gari yake kutiwa Giza la tinted Ili tusimwone ilhali analindwa.
 
Ni Rahisi kuchukua video au kupiga picha watu utakaowatilia mashaka.

Ikiwa jeshi la polisi limeshindwa kulinda raia, umma uingize haraka kazini kulinda HAKI ya kuishi ya JAMII ya Watanzania.
Haisadii kivile, jiulize ni kwa nini ni mara chache watu huweza kuwsona watekaji hata kama ni mchana.
 
Naunga mkono hoja,hasa kwenye vioo vya milango ya mbele na kioo cha mbele...
 
Tinted zote ziondolewe kwenye magari, ukaguzi kwenye check point ndipo ufuate.

Tunelekea kubaya,

Nawashauri raia WEMA wenye gari tinted kuzitoa mara Moja, maana hasira za umma nazifahamu.
Kumbuka siyo gari zote huchekiwa kwenye check point, zingine zinapita kama stuff!!
 
Kumbuka siyo gari zote huchekiwa kwenye check point, zingine zinapita kama stuff!!
HOJA ni kuturahisishia umma wa Watanzania tutakapoanza kufanya check up wenyewe kuwatafuta ndugu zetu.

Ikiwa u raia Mwema, ni muhimu kuondoa tinted Ili kujitofautisha na watekaji.
 
Nguvu ya Umma ndiyo suluhisho la hizi hofu tunazojengewa na dola.

Gari ya umma kuwa na tinted ni kuvunja sheria ya usalama kwa umma kutokana na mazingira ya sasa
 
Nguvu ya Umma ndiyo suluhisho la hizi hofu tunazojengewa na dola.

Gari ya umma kuwa na tinted ni kuvunja sheria ya usalama kwa umma kutokana na mazingira ya sasa
Mimi nilikuwepo Mzee Nyerere alipokuwa Rais, hakutumia gari zenye tinted, tulimuona live.

Sahizi tinted inawekwa Hadi kwenye kioo Cha mbele,halafu viongozi wanavyoendeshwa Kwa spidi unaweza Dhani wametekwa tayari!!
 
Ikulu imejengewa ukuta mzito na endapo ukatembea kwa nje yake na ukaugusa, kama hawwtakuua basi utashtakiwa kwa kutishia usalama wa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…