Ushauri: Harmonize acha kuandika Kiingereza

Ushauri: Harmonize acha kuandika Kiingereza

kukosea kitu kisichokuwa cha kwako hakuna shida.angekosea kuandika kiswahili au kimakonde hapo tungemkosoa. alafu hao wenye lugha yao wazungu tukikosea wala hawatushangai wala kutucheka shida ni sisi wazungu wa tandale na buza kwa lulenge
 
Hivi kwa nini anapenda kuandika kwa miherufi mikubwa? Huwa anahisi kila mtu ana matatizo ya macho?
 
Harmonize wewe ni msanii Mkubwa Tanzania lakini unafeli sana anapolazimisha kuandika English lhali bado hujakijua vizuri.

Harmonize unaonekana haupo Serious kwenye post zako kwa kuandika Ngeli Mbovu na zisizo na maana kwa wanaojua English pekee.

View attachment 2956342

BADILIKA MKUU.
Mkuu huwa unakisoma kiinglishi cha wanaijeria?

Hichi anachoa andika Harmo au Rayvan au shilole ndio kiingereza chetu halisi ambacho kimeathiriwa na matamshi yetu ya kiswahili
Tukianza kuongea nankuandika bila kuoneana aibu wala kukosoana itakua ni lugha inayoeleweka kama wenzetu wanaijeria au wajamika
 
Utakuwa unamwonea. Kwa background ya Harmonize hapo kajitahidi sana. Tuwanyooshee vidole watu waliosoma kama Nikki wa 2 ambaye akiandika hata kiswahili kunakuwa na kasoro kibao.
 
Kwahiyo unataka aandike kingereza Cha kimarekani wakati kazaliwa chitohole mkuu?We mwenyewe ukute kiswahili umekijua vyema ulivyoenda dar,na ungebaki usukumani sahizi kule ungekuwa unasema "kuree"
 
Msomi wa std 7 huyo kaandika hivyo, vizuri tu, kaweza!

Tafuta maandiko ya graduates ambao wanafanyiwa kila kitu, wanatengenezewa mpaka CVs, kisha uone kama Harmo atakuwa tofauti nao!

Kiswahili tu ni mtihani mkubwa, sio kwenye kuongea wala kuandika...ndio ije kuwa hiyo ya mkoloni!
 
Back
Top Bottom