USHAURI: House girl wangu anatoa harufu ya Jasho

Obel

Member
Joined
Jun 11, 2023
Posts
86
Reaction score
106
Hello dears!

Nmepata msaidizi wa nyumbani, kiukweli nampenda na anajitahidi na kazi zake sifikirii kumuondoa kwani pia huwa napata wadada wazuri tunaishi mda mrefu.

Huyu anashida ya harufu ya jasho lake ni kali sana. Akipita sehemu anaacha harufu. Najitahidi kuhimiza kuoga angalau mara mbili kwa siku haijasaidia!

Naombeni ushauri nimtafutie dawa gani au kitu gani kitachoweza kumsaidia aondokane na hiyo hali!? Sitaki kumpoteza
 
Aoge na atumie deodorant ambazo ni Anti-perspirant, kampuni haijalishi ni Vaseline, Dove, Axe au yoyote tu.
Hizi zinazuia perspiration - kutokwa na jasho. Atumie akiwa ameoga na kwenye ngozi safi!
 
Hicho ni kikwapa au ana chronic STDS Mpeleke hospital
 
Huwa ni kawaida Kwa vibinti vidogo ila akitumia deodorant atakuwa sawa.
 
Mwambie akioga ajisugue mwili wake.wengine kuoga ni kujimwagia maji na kujipaka sabuni Kwa mkono tu Kisha anajimwagia maji Tena kamaliza
Mnunulie Yale mavrashi ya kuogea yapo kama gloves za kuvaa mkononi.hata buku unapata
Mnunulie shavers,mwambie kufuga nywele makwapani na Kwa bibi ni uchafu
Mnunulie hata kale ka pafyumu ka kiss of love zile zinauzwa elfu nane 8_10 mwambie Kila akishavaa nguo safi ajipulizie
Asirudie kuvaa nguo iliyolowa majashi.kama ana uhaba wa nguo za kushindia wewe mpeleke hata sagulasagula za buku buku akachague.
Ukitaka hiyo harufu yake imtoke basi aachane na nguo za zamani Hadi za ndani.hope itasaidia
 
Hamjui harufu ya kijasho nyie, atamaliza vitu madukani ila ngoma itabakia pale pale. Kuna mdada kijijini alikuwa kaipita hata njian u ajua kapita fulani,walitumia marashi hadi yakawa mchanganyiko na kijasho kinatoka new mixture smell. Dawa ikaja kuwa ukoko wa sufuria la ugali, kwa sasa yule mdada ana familia yake na huwez jua alikuwaga kageuka beberu la mbuzi lililoloana na mvua hahaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…