USHAURI: House girl wangu anatoa harufu ya Jasho

USHAURI: House girl wangu anatoa harufu ya Jasho

Hicho ni kikwapa au ana chronic STDS Mpeleke hospital
Inawezekana kabisa kaka maana hata alivyokuja nilimuona km mtu aliedhoofu japo sijawahi kumuona kabla na nikamuuliza unaumwa akasema hapana! Maana ni mgeni ana miezi mwili Tu.
Na juzi kuna Jirani yangu ameniambia "huyu msichana wako mbona km anaumwa hivi km ametoa Mimba! Nikamwambia hata mm nilihisi anaumwa!
Namuhimiza Sana kuoga na Kula sana mtoto mdogo!
 
Ni kazuri MashaaAllah
Simple sana, ukishapika sufuria la ugali aloweke maji kisha aache yalale humo, asubuhi aogee huo ukoko ajisugue nao kwenye hizo kwapa. Then ukipata matokeo nipe mdogo wako nioe. Ni hilo tu
 
Mwambie akioga ajisugue mwili wake.wengine kuoga ni kujimwagia maji na kujipaka sabuni Kwa mkono tu Kisha anajimwagia maji Tena kamaliza
Mnunulie Yale mavrashi ya kuogea yapo kama gloves za kuvaa mkononi.hata buku unapata
Mnunulie shavers,mwambie kufuga nywele makwapani na Kwa bibi ni uchafu
Mnunulie hata kale ka pafyumu ka kiss of love zile zinauzwa elfu nane 8_10 mwambie Kila akishavaa nguo safi ajipulizie
Asirudie kuvaa nguo iliyolowa majashi.kama ana uhaba wa nguo za kushindia wewe mpeleke hata sagulasagula za buku buku akachague.
Ukitaka hiyo harufu yake imtoke basi aachane na nguo za zamani Hadi za ndani.hope itasaidia
Sawasawa!
 
Hello dears!

Nmepata msaidizi wa nyumbani, kiukweli nampenda na anajitahidi na kazi zake sifikirii kumuondoa kwani pia huwa napata wadada wazuri tunaishi mda mrefu.

Huyu anashida ya harufu ya jasho lake ni kali sana. Akipita sehemu anaacha harufu. Najitahidi kuhimiza kuoga angalau mara mbili kwa siku haijasaidia!

Naombeni ushauri nimtafutie dawa gani au kitu gani kitachoweza kumsaidia aondokane na hiyo hali!? Sitaki kumpoteza
Mimi wa kwangu nilifanya hivi.

Nilikaa nae kama dada, nikaanza kumpiga uongo na kweli kwamba yeye ni mrembo na ameshakuja mjini kuna vitu inabidi vibadilike ili awe na uonekano wa mjini.

Nikamueleza nitamletea baadhi ya vitu atatumia ili awe msafi, nikamnunulia deodorant (my main target), lotion, perfume na mafuta ya nywele. Nikamfundisha jinsi yaekutumia msisitizo ni kila anapooga apake deodorant kukata jasho na kupaka lotion na mafuta ya nywele.

Kwa kweli ilinisaidia sana nyumba haikuwa tena na harufu nzito. Na yeye akuipokea kama vile namnyanyapaa ila alichukulia kama nam-upgrade.
 
Ngoja amu-upgrade lije tatizo jingine la kunguru hafugiki...

Mimi wa kwangu nilifanya hivi.

Nilikaa nae kama dada, nikaanza kumpiga uongo na kweli kwamba yeye ni mrembo na ameshakuja mjini kuna vitu inabidi vibadilike ili awe na uonekano wa mjini.

Nikamueleza nitamletea baadhi ya vitu atatumia ili awe msafi, nikamnunulia deodorant (my main target), lotion, perfume na mafuta ya nywele. Nikamfundisha jinsi yaekutumia msisitizo ni kila anapooga apake deodorant kukata jasho na kupaka lotion na mafuta ya nywele.

Kwa kweli ilinisaidia sana nyumba haikuwa tena na harufu nzito. Na yeye akuipokea kama vile namnyanyapaa ila alichukulia kama nam-upgrade.
 
Simple sana, ukishapika sufuria la ugali aloweke maji kisha aache yalale humo, asubuhi aogee huo ukoko ajisugue nao kwenye hizo kwapa. Then ukipata matokeo nipe mdogo wako nioe. Ni hilo tu
Dah hivi hii tiba ya Aina hii ni kweli inasaidia??
 
Usafi tu,
Anyoe nyoe.
mwekeeni deto kwenye maji ya kuogea
atakua sawa tu
 
Mi wangu alikua anavaa shanga kiuononi nikaenda kumwambia mke wangu sahivi ananidai talaka
 
Inawezekana kabisa kaka maana hata alivyokuja nilimuona km mtu aliedhoofu japo sijawahi kumuona kabla na nikamuuliza unaumwa akasema hapana! Maana ni mgeni ana miezi mwili Tu.
Na juzi kuna Jirani yangu ameniambia "huyu msichana wako mbona km anaumwa hivi km ametoa Mimba! Nikamwambia hata mm nilihisi anaumwa!
Namuhimiza Sana kuoga na Kula sana mtoto mdogo!
Muwege mnawapima afya mabinti wa kazi, hasa HIV japo anaweza kuwa haumwi ni issue tu ya maisha ya dhiki akishazoea maisha ya kula vizuri atapendeza afya yake.
Kikwapa anaza na kumwambia akishaoga anapaka limao asubuhi na jioni kama sio ugonjwa kikwapa kitarudi utotoni hautakereka tena nlikuwa na binti ananuka kwapa ila alivotumia limao hata husikii hatufu na kumhimiza zaidi kuoga maana kuna jamii zingine kuoga ni issue ambayo haina maana ukinyamaza hata week anakata bila kujimwagia maji akiingia bafuni anamwaga mwaga maji anatoka we unahisi ameoga kumbe hakuna, nliwahi kuwa na binti wa hivo ikabidi niwe nasimama anajimwagia maji akianza kujisugua ndo natoka😀
 
Ahahaha ni kweli kuna jamii kuoga ni mtihani! Asante sana kwa ushauri! Juzi nilimunulia deodorant kiukweli harufu imepungua kwa kiasi kikubwa! Nitamuhimiza kutumia ndimu au limao kujisugulia makwapani
 
Anyoe nywele. Akiwa anaoga asugulie limao mixer baking powder kwapani aache dakika mbili kisha anawe kwa siku saba hivi. Harufu na jasho havitamsumbua
 
Back
Top Bottom