Ushauri huru kwa mawaziri wa Tanzania

Ushauri huru kwa mawaziri wa Tanzania

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Anayepewa ushauri akausikiliza bila kuufanyia kazi, huyo ni nusu mtu.
Anayepewa ushauri akausikiliza na akaufanyia kazi huyo ni mtu kamili.
Anayepewa ushauri asiusikilize kabisa, huyo ni mtu sifuri, hakuna mtu hapo.
Dhana ya ushauri kwa viongozi haikuanza leo kwenye tawala na utawala. Tukisoma historia tunakuta watawala hawajawahi kuwacha kuwa na washauri na wananchi hawajawahi kuwacha kutowa ushauri.

Katika kisa cha mtawala maarufu sana kuwahi kutokea na kutajwa sana ni Harun Al-Rashid wa Baghdad. Sitaki hapa kutaja sifa zote za uongozi wa Harun Rashid bali naitaja sifa moija tu, ya kushauriwa akasikia na akafanyia kazi yote aliyoshauriwa. Hata ushauri mbaya aliufanyia kazi na kuugeuza uwe mzuri.

Moja katika sifa za Harun Al Rashid ni kuwa hajawahi kukataa kusikiliza ushauri na hajawahi kuwacha kuufanyia kazi ushauri.

Nimeanza kwa utangulizi huo kwa kuwa naziona wazi athari za utawala wa kusikiliza na kufanyia kazi ushauri za utawala wa Harun Rashid kwa mama Samia. Mama Samia, kama jina lake lilivyo. Niliwahi kuandika maana ya jina la mama Samia hapa:

Leo nawashauri Mawaziri; Kwanza kuweni wasikivu kisha muyafanyie kazi mnayoshauriwa hata kama kwa mtazamo wenu hayaingii akilini.

Ushauri wangu wa msingi ni kuwa Mawaziri badilikeni katika undeshaji wenu wa kazi wa kila siku. Msiendelee kufanya kazi kimazowea. Uwaziri wa kuwa msaidizi wa kupaza sauti za kisiasa za utawala umepitwa na wakati. IUwaziri wa kuwa ni cheo cha kisiasa umepitwa na wakati. Uwaziri wa leo unahitaji waziri muelewa na mchapa kazi kwa vitendo zaidi ya Katibu Mkuu wake.
Waziri umeshapewaa "outline guidance" uende vipi kwenye kazi zako. Guidance yako ni R 4 za mama Samia.

Jifikirie kwenye wizara yako ya kwanza ya Reconciliation umefanya nini kinachoingia kwenye falsafa hiyo?

Hali kadhalika kwa R zote zilizobakia. Kama ukiona hufanyi kazi zako kwa misingi hiyo basi elewa kuwa uwaziri haukufai kabisa.

Kwa ufupi, kama hauna amani, utulifu na kufata ushauri hutoweza kutimiza malengo ya falsafa ya R 4 za mama Samia.

Harun Al Rashid utawala wake wote, uliokuwa na mafanikio makubwa sana, ukiusoma utazikuta hizo R 4 bila kusemwa hizi ni R 4.

Mawaziri ambao mnashindwa kuzifata R 4 za mama Samia mjielewe kabisa, kuwa safari yenu itaishia 2025, kama mtafika huko. Kwani nahisi hapa kati kutakuwa na mabadiliko madogo madogo mawili matatu, kama si moja kubwa.

Nahitimisha kwa kuwataka mzisome maana ya hizo R 4 kwa undani wake.

Wakati uzi huu unaendelea, unaweza kuwataja mawaziri unaoona wanahitaji wabadilike kwa namna zao za utendaji kazi.
 
Habari za Asubuhi Dada yangu FaizaFoxy. Nakutakia siku njema. Tuendelee kumuunga Mkono Kiongozi wa nchi yetu.

Tusimuwekee makwazo kiongozi wetu. Yeye ana macho makali ana masikio makali kutuzidi...hivyo, tumuache afanye kazi yake bila mashinikizo kisa tu tuna bifu na wateuliwa wake.

Tujikite kwenye issues ambazo yeye tukimpelekea hizo issues atajua, ni mteuliwa wake yupo hajatimiza wajibu kisha atafanya maamuzi sahihi kama afanyavyo muda wote.

Kwa namna ulivyoleta hoja, Dada, utatuhumiwa kuwa na "kijiba cha roho" wakati nadhani si makusudio yako.
 
Habari za Asubuhi Dada yangu FaizaFoxy. Nakutakia siku njema. Tuendelee kumuunga Mkono Kiongozi wa nchi yetu.

Tusimuwekee makwazo kiongozi wetu. Yeye ana macho makali ana masikio makali kutuzidi...hivyo, tumuache afanye kazi yake bila mashinikizo kisa tu tuna bifu na wateuliwa wake.
Umeisoma mada?
 
Nnafahamu kuwa moja ya kazi za mawaziri ni kumshauri Rais.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum)​

MHE. KAPT GEORGE HURUMA MKUCHIKA

MHE. KAPT GEORGE HURUMA MKUCHIKA​

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum)

Kuna anaeweza kunisaidia "Kazi Maalum" huwa ni zipi? Au uzee ni dawa?

Hivi kazi ya uwaziri haihusiani na sheria au kanuni za ustaafu Tanzania? Maana Capt umri wake kwa sasa ni miaka 75.

Binafsi nashindwa kushauri kitu chochote kuhusu waziri Mkuchika, kwa sababu sizielewi kazi na majukumu yake.

Mwenye uelewa, ni jukwaa huru hili.
 
ASANTE SANA FAIZA FOXY,KWANGU MIMI MAWAZIRI AMBAO ATLEAST WANAJITAHID KUFUATA R4 ZA MAMA PRESIDENT NI MCHENGERWA,BASHE,AWESO,BITEKO NA ULEGA...

WATU KAMA JANUARY MAKAMBA NA RIDHIONE KIKWETE WANAZINGUA SANA, NA WAJIANGALIE PLUS MWIGULU NCHEMBA,NI WATU AMBAO SEEMS WANA NDOTO ZAO WANAZOTAKA KUZISAFARIA KUPITIA MAMA
 
Anayepewa ushauri akusikiliza bila kuufanyia kazi, huyo ni nusu mtu
Anayepewa ushauri akausikiliza na akaufanyia kazi huyo ni mtu kamili.
Anayepewa ushauri asiusilize kabisa, huyo ni mtu sifuri, hakuna mtu hapo.
Dhana ya ushauri kwa viongozi haikuanza leo kwenye tawala na utawala. Tukisoma historia tunakuta watawala hawajawahi kuwacha kuwa na washauri na wananchi hawajawahi kuwacha kutowa ushauri.

Katika kisa cha mtawala maarufu sana kuwahi kutokea na kutajwa sana ni Harun Al-Rashid wa Baghdad. Sitaki hapa kutaja sifa zote za uongozi wa Harun Rashid bali naitaja sifa moija tu, ya kushauriwa akasikia na akafanyia kazi yote aliyoshauriwa. Hata ushauri mbaya aliufanyia kazi na kuugeuza uwe mzuri.

Moja katika sifa za Harun Al Rashid ni kuwa hajawahi kukataa kusikiliza ushauri na hajawahi kuwacha kuufanyia kazi ushauri.

Nimeanza kwa utangulizi huo kwa kuwa naziona wazi athari za utawala wa kusikiliza na kufanyia kazi ushauri za utawala wa Harun Rashid kwa mama Samia. Mama DSamia, kama jina lake lilivyo. Niliwahi kuandika maana ya jina la mama Samia hapa:

Leo nawashauri Mawaziri; Kwanza kuweni wasikivu kisha muyafanyie kazi mnayoshauriwa hata kama kwa mtazamo wenu hayaingii akilini.

Ushauri wangu wa msingi ni kuwa Mawaziri badilikeni katika undeshaji wenu wa kazi wa kila siku. Msiendelee kufanya kazi kimazowea. Uwaziri wa kuwa msaidizi wa kupaza sauti za kisiasa za utawala umepitwa na wakati. IUwaziri wa kuwa ni cheo cha kisiasa umepoitwa na wakati. Uwaziri wa leo unahitaji waziri muelewa na mchapa kazi kwa vitendo zaidi ya Katibu Mkuu wake.
Waziri umeshapewaa "outline guidance" uende vipi kwenye kazi zako. Guidance yako ni R 4 za mama Samia.

Jifikiriea kwenye wizara yako ya kwanza ya Reconciliation umefanya nini kinachoingia kwenye falsafa hiyo?

Hali kwadhalika kwa R zote zilizobakia. Kama ukiona hufanyi kazi zako kwa misingi hiyo basi elewew kuwa uwaziri haaukufai kabisa.

Kwa ufupi, kama hauna amani, utulifu na kufata ushauri hutiwezza kuzitimiza maengo ya falsafa ya R $ za mama Samia.

Harun Al Rashid utawala wake wote, uliokuwa na mafanikio makuwa sana, ukiusoma utazikuta hizo R $ bila kusemwa hizi ni R 4.

Mawaziri ambao mnashindwa kuzifata R 4 za mama Samia mjielewe kabisa, kuwa safari yenu itaishia 2025, kama mtafika huko. Kwani nahisi hapa kati kugtakuwa na mabadiliko madogo madogo mawili matatu.

Nahitimisha kwa kuwataka mzisome maana ya hizo R 4 kwa undani wake.

Wakati uzi huu unaendelea, unaweza kuwataja mawaziri unaoona wanahitaji wabadilike kwa namna zao za utendaji kazi.
Chawa wa samia
 
Waziri wa Uchukuzi​

MHE. PROF. MAKAME M. MBARAWA

MHE. PROF. MAKAME M. MBARAWA​

Waziri Mbarawa, kwanza hongera sana kwa juhudi na kazi kubwa ulizozifanya bandarini.

Sasa nakushauri, anza kutolea macho usafiri wa Jamii (public transport), anza na UDART (mwendokasi), ondowa mabasi yote hayo, weka mabasi ya umeme. Na battery zake ziwe ni "tamper proof", matairi yake yawe na marked kwa rangi ya mpira kuaniza kiwandani, labda yake na ufito wa kijani. Kuzuia kuibiwa na kuuzwa.

Au hakikisha wanakutengenezea saizi ya matairi ambayo hayatumiki kwenye malori na mabasi yetu.

Usafiri wa mwendokasi mkifanikisha, hata daladala binafsi ziwe za umeme.

Hii itatupa fursa Watanzania kuanzisha viwanda vya battery zitazotumika. Pia tutautumia vyema umeme unaotugharimu esa nyingi sana wa bwawa la Nyerere.

Naamini hata canter na malori ya kuingia mjini yote inawezekana kabisa ikawa ya umeme.

Tuanze sasa, faida zake ni nyingi sana.
 
Imatisha sana kuonanleo bungeni mawaziri wanapewa ushauri wa kupambana na wiz8 na ubadhirifu kwenye wizara zao, wao hawana habatlri, wapo bize ndani ya ukumbi wa bunge wanachezea simu.
 
Back
Top Bottom