FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Anayepewa ushauri akausikiliza bila kuufanyia kazi, huyo ni nusu mtu.
Anayepewa ushauri akausikiliza na akaufanyia kazi huyo ni mtu kamili.
Anayepewa ushauri asiusikilize kabisa, huyo ni mtu sifuri, hakuna mtu hapo.
Dhana ya ushauri kwa viongozi haikuanza leo kwenye tawala na utawala. Tukisoma historia tunakuta watawala hawajawahi kuwacha kuwa na washauri na wananchi hawajawahi kuwacha kutowa ushauri.
Katika kisa cha mtawala maarufu sana kuwahi kutokea na kutajwa sana ni Harun Al-Rashid wa Baghdad. Sitaki hapa kutaja sifa zote za uongozi wa Harun Rashid bali naitaja sifa moija tu, ya kushauriwa akasikia na akafanyia kazi yote aliyoshauriwa. Hata ushauri mbaya aliufanyia kazi na kuugeuza uwe mzuri.
Moja katika sifa za Harun Al Rashid ni kuwa hajawahi kukataa kusikiliza ushauri na hajawahi kuwacha kuufanyia kazi ushauri.
Nimeanza kwa utangulizi huo kwa kuwa naziona wazi athari za utawala wa kusikiliza na kufanyia kazi ushauri za utawala wa Harun Rashid kwa mama Samia. Mama Samia, kama jina lake lilivyo. Niliwahi kuandika maana ya jina la mama Samia hapa:
www.jamiiforums.com
Leo nawashauri Mawaziri; Kwanza kuweni wasikivu kisha muyafanyie kazi mnayoshauriwa hata kama kwa mtazamo wenu hayaingii akilini.
Ushauri wangu wa msingi ni kuwa Mawaziri badilikeni katika undeshaji wenu wa kazi wa kila siku. Msiendelee kufanya kazi kimazowea. Uwaziri wa kuwa msaidizi wa kupaza sauti za kisiasa za utawala umepitwa na wakati. IUwaziri wa kuwa ni cheo cha kisiasa umepitwa na wakati. Uwaziri wa leo unahitaji waziri muelewa na mchapa kazi kwa vitendo zaidi ya Katibu Mkuu wake.
Waziri umeshapewaa "outline guidance" uende vipi kwenye kazi zako. Guidance yako ni R 4 za mama Samia.
Jifikirie kwenye wizara yako ya kwanza ya Reconciliation umefanya nini kinachoingia kwenye falsafa hiyo?
Hali kadhalika kwa R zote zilizobakia. Kama ukiona hufanyi kazi zako kwa misingi hiyo basi elewa kuwa uwaziri haukufai kabisa.
Kwa ufupi, kama hauna amani, utulifu na kufata ushauri hutoweza kutimiza malengo ya falsafa ya R 4 za mama Samia.
Harun Al Rashid utawala wake wote, uliokuwa na mafanikio makubwa sana, ukiusoma utazikuta hizo R 4 bila kusemwa hizi ni R 4.
Mawaziri ambao mnashindwa kuzifata R 4 za mama Samia mjielewe kabisa, kuwa safari yenu itaishia 2025, kama mtafika huko. Kwani nahisi hapa kati kutakuwa na mabadiliko madogo madogo mawili matatu, kama si moja kubwa.
Nahitimisha kwa kuwataka mzisome maana ya hizo R 4 kwa undani wake.
Wakati uzi huu unaendelea, unaweza kuwataja mawaziri unaoona wanahitaji wabadilike kwa namna zao za utendaji kazi.

Maana ya Jina la Rais wa Tanzania, Samia Suluhu
Jina la Rais wetu Bi Samia Suluhu limeundwa kutokana na maneno ya Kiarabu. 1) Samia: Maana yake ni msikivu. Neno hili hupatikana hata katika salat za kila siku kwa Waislaam, pale Muislam anaposali, akinyanyuka kwenye rukuu husema "Samia Llahu liman Hamida". maana yake, Ni "Allah humsikia mwenye...