Ushauri: Ili kulinda heshima yako Mataragio usikubali huo uteuzi wako, kataa waachie cheo chao

Ushauri: Ili kulinda heshima yako Mataragio usikubali huo uteuzi wako, kataa waachie cheo chao

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ni kwa sababu Mamlaka ya Uteuzi haikuamini tena na ndio maana nafasi yako akapewa mtu mwingine , Kilichotokea ni kwamba huyo aliyepewa nafasi yako ameonekana kituko , duni na hatoshi na ndio maana ametenguliwa ukarudishwa tena , hii haimaanishi wewe unafaa , jiongeze mwenyewe ndugu.

Wewe umekuwa kama mbuzi wa Shughuli , awamu iliyopita uling'olewa na kuswekwa Rumande kwa muda kutokana na tuhuma za Uhujumu uchumi , kabla ya kutolewa Jela na Rais aliyepita na kurejeshewa cheo chako , Magufuli alisema hauhusiki na tuhuma ulizopewa.

Hivi hujiulizi nani anayekuhujumu kiasi hicho na anakutakia kitu gani ? kwanini usijiokoe mwenyewe kwa kuwaachia cheo chao ? mbona kuna maisha mengine baada ya hivyo vyeo vya kidunia ambavyo ni vya kupita tu !
............

ANGALIA VIELELEZO HIVI HAPA.

2733542_EyMYDN8XAAEFCFU.jpeg

2733540_EyMYDN8WgAEhKZz.jpeg
 
Yule jamaa muungwana sana hata jiwe alivyojifanya kumtengua na akamridisha wala hakusema neno , baada ya kuzinguliwa alirudi zake USA akaendelea na kazi zake mishahara kama kawaida sasa hili la yohana univasiti ni kubwa kuliko, nchi ina wakati mgumu sana
 
Hahahaaaa!! eti nchi ina wakati mgumu!

Building & Finance vs Yohana University

Kweli tuna wakati mgumu bwashee......... hahahaaaa!
 
Ushauri mzuri , Ila kama anaweza aombe kuonana na Raisi Kwanza wayajenge kuhusu stuation anayopitia ..... Raisi akimhakikishia basi aendelee la sivyo apige chini , ni fedheha
Inasikitisha sana , huyu jamaa ana familia yake lakini anadhalilishwa kizembe namna hii jamani !
 
Hii ni kwa sababu Mamlaka ya Uteuzi haikuamini tena na ndio maana nafasi yako akapewa mtu mwingine , Kilichotokea ni kwamba huyo aliyepewa nafasi yako ameonekana kituko , duni na hatoshi na ndio maana ametenguliwa ukarudishwa tena , hii haimaanishi wewe unafaa , jiongeze mwenyewe ndugu....
Hivi unajua njaa wewe?unajua manono yaliyopo kwenye cheo hicho?
 
Yule jamaa muungwana sana hata jiwe alivyojifanya kumtengua na akamridisha wala hakusema neno , baada ya kuzinguliwa alirudi zake USA akaendelea na kazi zake mishahara kama kawaida sasa hili la yohana univasiti ni kubwa kuliko, nchi ina wakati mgumu sana
Hivi Chuo hicho kimekuwa accredited na TCU kweli?
 
Hii ni kwa sababu Mamlaka ya Uteuzi haikuamini tena na ndio maana nafasi yako akapewa mtu mwingine , Kilichotokea ni kwamba huyo aliyepewa nafasi yako ameonekana kituko , duni na hatoshi na ndio maana ametenguliwa ukarudishwa tena , hii haimaanishi wewe unafaa , jiongeze mwenyewe ndugu...
Wabongo inabidi kuwa nao makini sana. Huyu anamshauri DG asude ili wakawe wanabet pamoja
 
Back
Top Bottom