Ushauri jamani: Nanyanyasika ukweni, eti nimemchezea muda mrefu

Eti ulikuwa unaogopa mkiachana mtagawana mali wakati yeye ni mama wa nyumbani. SELFISHNESS inakukula. Mtu mmezaa, tena unampenda halfu ujifanya kuishi mguu ndani mguu nje. ukomeee
Walikuwa wanamdanganya kwao, kuna wazazi anamwambia kabisa mwanaye oa mwanamke mwenye kazi ili mwanamke awe anajisaidia mwenyewe hata kama ni kwao,. PhD ya ubinafsi, utazani hao watoto waliwabeba wote tumboni, sasa aoe mwenye kazi yake ili wasaidiane kulea watoto.
 
#KATIKA WANAUME WASIOJITAMBUA WW UTAKUA KIONGOZI WAO_MIAKA 39 HUNA HATA AKILI ZAKUJIONGEZA
 
Wewe jamaa sijui nikutakane,

Anyway si ameshaondoka.......nenda kachukue mahari yako uile na watoto

Tafuta mfanyakazi wa ndani ambaye alishawahi kufanya kazi za ndani na anajua kulea watoto muajiri mlipe 200k kwa mwezi

Mnunulie na mashine ya kufuria afu usiwe mnoko mnoko mlipie king'amuzi ili asiwe mzururaji mjari kama mdogo wako mlozaliwa Mama na Baba mmoja

Miaka 39 bado kijana kabisa, jipende, nenda Barbershop fanya scrub ya mvuke utoe mwonekano wa kizee zee, kula matunda kwa wingi kunywa na maji mengi ili kuboresha afya yako

Kwa sasa huhitaji mwanamke wa kukuumiza kichwa kwa sasa unahitaji kutafuta pesa hakikisha wanao wanainjoi, wewe kula goodtime maisha yaendelee

Lea wanao vizuri hakikisha afya yao ina imarika maradufu wakatie na Bima ya Afya kabisa kama hawana

Huyo shukuru kaondoka kuliko angekuwepo angekuua kabisa na wala usimng'ang'anie achana nae

Mimi nna miaka 38 mpaka mwisho wa mwaka natimiza 39, nna mke na watoto wanne watatu nilizaa na mtalaka wangu, mwaka juzi nikaoa mtoto mbichi tena bikra kabisa nilioa akiwa na miaka 24 huku mimi nikiwa na 37

Na mpaka sasa nimezaa naye mtoto mmoja, na mwenyewe anajua kabisa sitaki ubabaishaji akichoka ndoa aseme kila mtu aishi kivyake
 
Naunga mkono hoja.

Sister hood , mother hood, bongo hood and all of the hoods are proud of this woman.
 
Ukishatoa mahari na wazazi wakapokea ni ndoa hiyo, wanasemaje umemchezea na mahar umetoa?

Kama ameondoka muache, mbona amekutengenezea faida na mtaji wako umerudishiwa, yaani amekupa watoto na mahari umerudishiwa kubali yaishe hilo amelichuma na wazazi wake atalinywa. Kuwa mpole lea watoto wako
 
Ulitaka wazazi wake waendelee kumlea mkeo na wanao?
Kweli hauna akili.
Hauni aibu kuuliza ujinga kama huo mbele za wanaume?
Halafu unajisifia ujinga. Kaa na wanao uwatafutie mama wa kambo .
 
Naunga mkono hoja.

Sister hood , mother hood, bongo hood and all of the hoods are proud of this woman.
Sema tatizo mwanadada kaondoka Ila bado moyo upo kwa jamaa maana kama angetaka kuondoka, asingesubiria kufukuzwa. Kwa hiyo hii move ni aidha kadhamiria au kafanya kumkomoa ambavyo vyote vitaamua kama atapats furaha anayoitafuta au la

Ila kwa sasa jamaa asihangaike. Mwanamke kashadhamiria
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jinga kabisa, unacholilia ni nin ? Wanao si amekuachia ? Tafuta mtoto mdogo wa elfu 2, muoe mzalishe mtoto mmoja tu , ule nae uzee
 
Sio chaguo lako we lea mabao yako hayo maisha yaendelee. Watoto watatu si haba jombaa
 
kwa uchoyo wa mali ulionao ni wakati sasa ulee watoto wako kwa kushirikiana na jamaa zako ili mlinde ulichochuma.
 
Sasa wewe ulitaka umchezee mpka lini?Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…