Ushauri jamani: Nanyanyasika ukweni, eti nimemchezea muda mrefu

Ushauri jamani: Nanyanyasika ukweni, eti nimemchezea muda mrefu

Hii ndio ile ‘One man’s trash is another man’s treasure’

Dada popote ulipo kama kuna duka la mangi hapo nje pata fanta nyeusi ya baridiiiii (na hili joto) nitailipia. Umejua kumnyoosha huyu nyau
 
Situation kama hii iliwahi kumtokea mwanangu mmoja Kila akija kijiweni "utasikia tu Yani wanangu yule mwanamke mimi nime vumilia tu na alivo na pua kubwa kama pumbu za mtoto mdogo 🥶🤣watu kijiweni hoi kwa mbavu

Pole likuepukalo linashari"
 
Tafuta single mama kafunge nae ndoa watoto wake na WA kwako familia imetosha
 
Watanzania wengi hawajui sheria zinazohusu ndoa

Kitendo cha kulipa mahari na kujulikana na wazazi wake hiyo ni ndoa ya kimila

Kilichokuwa kimebaki hapo ni kwenda kuisajili ndoa mpewe cheti cha ndoa

Mwanamke alikuwa anataka harusi sio ndoa

By the way shukuru Mungu lijambazi limeondoka ulikuwa unaishi na tapeli
Subili binti yako akue
 
Oya hili nalo ni lakuleta kwenyebalaza pijadiliwe. Nilitegemea unaleta hoja kwamba umefanya maamuzi ya kutafuta manzi nyingine mmekubaliana mnalea watoto maisha yanasonga, alafu ukija hapa sisi tunakiongezea abc za kutokaa kifala.
 
mimi ni mbabaz wa miaka 39, sijaoa lakini naishi na mwanamke ambaye naweza kusema kuwa ni kama mke wangu kwani nilishamtolea mahari, tumeishi pamoja kwa miaka kumi bila ndoa, sikuona umuhimu wa kufunga naye ndoa kwani yeye ni mama wa nyumbani, nilijua kama nikifunga naye ndoa ikatokea tunatengana basi tunaweza kugawana mali hivyo nikawa nafanya mambo yangu kimya kimya.

Kila mara alikua akilalamika kufunga ndoa mimi nampiga chenga, lakini siku za karibuni amekua haulizii tena mambo ya ndoa, alikaa kimya kwa meizi sita mpaka na mimi nikaanza kuwa na wasiwasi. Nilianza kuchunguza kwani nilihisi kuwa ana mwanaume mwingine, huwezi amini nimegundua kuwa mke wangu ana mwanaume mwingine, tena mtu mzima ambaye alishaoa na kufiwa na mke wake pamoja na mtoto mmoja, alikua hajaoa muda mrefu baada ya kufiwa na mke wake.

Baada ya kuona hivyo niliongea na mke wangu akaniambia kuwa hakuna kitu kama hicho, nilimuambia suala la kuoana nikamuambia kuwa sasa hivi mimi niko tayari lakini yeye ndiyo akawa mtu wakunipiga chenga mara nyumbani hawajajiandaa, nymbani hivi na nyumbani vile. Mimi niliamua tu kwenda mwenyewe lakini cha ajabu nimefika huko wakwe zangu wamekataa mimi nisimuoe binti yao, eti wanaseam nimemchezea muda mrefu hivyo wamenirudishia mahari yangu ingawa mimi nimekataa kuzipoke.

Nimemuuliza mke wangu anajifanya hajui kitu,a naniambia lakini kama wazazi wameamua yeye si wakuwapinga. Nimefuatilia kumbe kashampeleka yule mwanaume kwao na kajitambulisha na kutoa mahari. Nilipombana na kumpiga kidogo aliondoka, niliamua kumtishia na kumuambia kama anaondoka na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine basi anaichie wanangu akanijibu hakuja kwangu na mtoto hivyo ni sawa tu nikibaki nao kwani ni wakwangu hata kama nikiamua kuwanyanyasa ni mimi, ananitumia meseji ananiambia tena ni afadhali kwani ingemuwia shida kuanza ndoa mpya na watoto. Tuna watoto watatu na mke wangu kaondoka na kuniachia nao, sijui hata nifanyeje
Huyo sio mkeo pimbi wewe
 
Subili binti yako akue
Kwa hiyo unamaanisha nile mahari ya kijana wa watu, aishi na binti yangu miaka 10 na wazae watoto 3 halafu nije kukubali aolewe na mwanaume mwingine!

Sijawa baba mpumbavu kiasi hicho
 
Sema wote tu mnamatatzo, wew uliokosea kuwa mbinafs.
Yey naye alikua hana uaminifu..
UKWEN kwako nao hawajitambui..

Tukiachana na hayo kisheria ukiish na mwanamke/mwanamme kuanzia miez mitatu 3+ hyo atajurikana ni mke/mme wa mtu.
Pia kitendo cha kutoa mahari na ikakubariwa na kuridhiwa pande mbil kwa waoaj/waolewaj huyo tayar ni mali yako tena ni mke harari kijadi.
Wew kijad na kisheria yule ni mkeo unaweza mshka ugoni.

Usukuman hiz ndoa nying sana, hutoa mahar na kubeba mzigo hapo hadi uzeen harus had wapende sasa.

Ila Mwisho...
Ucjisumbue kumludisha hyo mwanamke hana uaminifu tena ata akirud kwako.
Pili ameshakutoa moyon mwake, na hii ni hatar zaid.
Peleka watoto kwa bib yao au oa uckae single koz umli umeenda mno, ila uskurupuke kuoa.
Na usiwe mbinafs tena.

Mda si mref mkeo ataachika kule koz jamaa hawez kuwa na mwanamke aliesalit kwa kuhs atamsalit yey pia
 
Unaposema ulikuwa hujaoa una maana gani,kitendo cha kutoa mahali ni kuoa huko.
Kuna ndoa za aina tatu,kimila,kidini na kiserikali.

Huyo mwanamke kama ambavyo ulidhania mwanzo,alikuwa after mali zako.Na kweli ndicho kilichotokea.
Mie nakushauri huyo mwanamke anaonekana kabisa sio mwaminifu,hao watoto kawapime DNA.
 
Back
Top Bottom