Binafsi, Nakushauri awekeze UTT especilly Bond Fund au Liquid fund, kwa 100 ambayo anayo atakuwa anapata walau 1,000,000 kila mwezi (Ambayo anauwezo wa kuitoa ndani ya siku kumi tu tofauti na fixed deposit za bank ukitoa unakuwa umevunja mkataba while UTT unaweza kuitoa hela yote wakati wowote ndani ya siku kumu.....actualy ni siku mbili hivi ..mimi huwa napata fedha yangu ndani ya siku mbili tokea nifanye repurchase),Pili Bank ile riba unapata wanakata witholding tax ya 10% wakati UTT au Bond ya BOT hawakati kodi ya Zuio.
Baada ya kuwekeza UTT-Bond fund, kama yupo interested na vibiashara vidogovidogo ama kujenga nyumba anaweza kwenda bank akakopa akaweka vipande vyake vya UTT kama bond/Collateral na zile coupon /faida anazopata zikatumika kulipa mkopo wake, say,rejesho la kila mwezi 700,000 anakuwa anabakiwa na 300,000. Hii 300,000 akichanganya ka pension zake za kila mwezi ataishi vizuri tu, Mungu akimjalia vibiashara navyo vikafanya vema atapata faida.
Kwa mpangilio huo niliokushauri,pesa yake yote itabakia 100M, muda wote bila kupungua na life likaenda vema.
For more Advise ,kwenye eneo la Personal finance PM with consultation fees