Ushauri: Je, ajenge nyumba au aweke pesa fixed deposit CRDB kwa riba ya 7%?

Mkuu kwa mfano umeweka Milioni 1 huko UTT, mwisho wa mwezi wanaweza kukupatia mgao kiasi gani?
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please
Inaonekana alikuwa mtu mkubwa sana mama yako, kwa kikokotoo cha wizi hiki kupata 100m ujue alistahili 300m kwa kikokotoo cha nyuma kabla ya huu ujambazi wa siku hizi
 
Halafu zina zaaje ukishanunua!!?mfano tafadhali!!
Hapa ni somo refu, ila unaweza kupata kwa namna mbili, moja ni kama ulinunua kwa bei pungufu(at discount, mfano umenunua bond kwa sh.70 yenye face value/par value 100, faida yako ni 30 kwenye kila kipande), namna ya pili ni ile coupon rate (Riba) kwa Bond za muda mrefu BOT wanatoa riba mara mbili kwa mwaka
 
Maisha ya ajira kwel ni utumwa na unyonyaji unafanyaa kazi miaka 40 ufike miaka 60 ndipo upate milion 100.
Wakati watoto wa Kikinga anamiaka 20 anapita airport ana cash milioni 300 anaenda jumua t shirt na jeans China akauze njombe
Huyo mkinga muulize na hasara anayoipata mzigo ukidoda au kuungua ni kiasi gani? Biashara sio kila mtu anaweza and the same applies to things like soccer and music. Kila mmoja afanye kipaji chake kilipo kama Samatta na Ali Kiba.
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please
Nyumba ni hasara
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please
Hiyo nyumba itampa hizo laki saba kila mwezi ? Nadhani jibu lipo hapo.., sio kila kitu ni kizuri kwa kila mtu mwingine hata kama atapata 2m kila mwezi ila kero za kusumbuana na watu na kuwadai kama vile unawaomba wakati ni haki yako its not worth it.... Unajua maana ya kustaafu ni ku-relax na ku-enjoy mafao yake sio kuingia kwenye Utumishi Na. 2 - (ili astaafu lini ? siku anazikwa?)
 
Hivi akijenga
sebule chumba 3m x3m na sebule 4m x 3m , choo ndani 1.3m x 2.3m na jiko lake dogo 1.3m x 3.5m

Budget yake kamoja ni bei gani kwa haraka ili avijenge kama 20 hivi
Tofali 1000 zinaweza kukatika kulingana na foundation. 1000*1100
Mifuko ya cement zaidi ya 40 inaweza kukata 40*17,000
Bati zaidi ya 20*28,000
Mbao za kenchi zaidi ya 30za4*6000
Bado hajaskimm, bado fundi, bado mchanga, bado kokoto, bado nondo, bado maji, bado blundering, bado madirisha, bado umeme na bado fundi hajakutapeli. 😆 7m kima cha chini lazima ikate.
N.B tofali za kuchoma akakazia na tope alafu baadae aje apige plasta inaweza punguza gharama.
 
Tenure20 Years
Coupon Rate(%)
12.1​
Weighted Average Price(WAP)
92.9342​
Amount at Maturity(Face Value)
107,603,013.75​
Investment Amount(Cost Value)
100,000,000​
Capital Gain (Face Value - Cost Value)
7,603,013.75​
Yearly Coupon
13,019,964.66​
Total Coupon Amount
260,399,293.26​
Total Coupon Amount After Withholding Tax
260,399,293.26​
Total Gain (Tal Coupon + Capital Gain)
268,002,307.01​
 
Hatifungani za BOT, na hasa za muda mrefu zenye riba nzuri zaidi,
Hii ni nzuri kama unawawekea watoto na wajukuu, yaani unachukua riba wewe hata ikitokea umekufa, basi hao niliowataja wanaendelea kula mema ya nchi.
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please
Ajenge nyumba kama anataka kuwapea urithi usiohamishika...
 
Mkuu hii comments Nahisi umeijibu kutoka kwenye mvungu wa moyo yani deeeeeep kabisa [emoji1]
Umejuaje? Ni kweli, haya makosa tulifanya enzi hizo ila tungerudi nyuma, siamini kama tungepoteza pesa ati kuinvest kwa kujenga nyumba za kupangisha. Kumbuka ukijenga nyumba ya kupangisha huwezi kamwe kurudisha hela yako uliyotumia kujenga. Niishie hapa
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please
Nyumba ya biashara ni no no maana mpaka hela irudi ni miaka 15. Baada ya miaka 15 ndo anaanza kula faida!

Aweke hela kwenye fixed account au UTT bonds anaanza kula faida immediately huku hakimbizani na kudai Kodi wala sijui choo kimeharibika.

Uzuri principal amount aliyoweka Bado anaweza kuichukua anytime akitaka. Lakini nyumba akiamua kupata hela kuuza sio rahisi.

Ps. Why CRDB? Kuna benki ya serikali inaitwa TCB zamani benki ya posta wana riba nzuri.....
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please

Aamue mwenyewe, yani kweli unakuja mwombwa Maza ushauri wa kutumia hela zake?
 
Hivi mburula nao wanadai consultation fee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…