USHAURI: Je, ananipenda au ndiyo jinsi alivyo?

USHAURI: Je, ananipenda au ndiyo jinsi alivyo?

Quan Lup

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2016
Posts
683
Reaction score
946
Habari zenu wadau,

kuna dada mmoja tunafanya nae kazi ofisi X. Huyu dada ni mshikaji wangu since day one maana tulianza kazi siku moja na siku ya interview tulikua wote sema tulikua hatujazingatiana sana.

Sasa kipindi naanza kazi siku ya kwanza Paa hyu hapa tukatambulishwa pale maana ndo tulikua wageni kwa hyo sisi ndo tukawa marafiki.

Sasa tukawa marafiki tumeshazoena sana na aakajua nguo ninazopenda na vitu ninavyopenda mwaka jana mwezi wa 6 ilikua ni happy birthday yangu daah hauwezi amini akanipigia akaniambi i have suprise for you nikamuambia really? akasema yeah nikawamua ok naisubiri akaniambia poa.

Daah kesho kaja kazini mida ya kama saa 4 hivi nikaletewa cake ofisini daaah akaniapa na mfuko akaniambi huu utaufungua bade aisee nilifrahi saana tukakata cake tukawa tunawalisha wafanyakazi wenzetu wa ofisini.

Nikatoka job nina kimuhe muhe cha kufungua zawadi ile nimefika tuu home daaah huwezi amini huyu dada alikua amenununulia samsung galax note 8 jezi ya chelsea na yanga daaah niliishiwa pozi nikamshukuru sana.

Mwisho wa mwaka huu walivunja vikoba akanitumia laki moja akaniambia my friend ya kwako hyo, sasa kapata kazi mpya na mshahara umenonan zaidi akaniambia nichague zawadi ninayoitaka aninunulie ili akiondoka nisiweze kumsahau hapa ndo nawaza zawadi gani? sijawahi kumtongoza sijawahi mwambia habari za mapenzi yaani nashindwa tuu kuelewa naogopa nikimtongoza urafiki wetu utavunjika.

Ila niliishi naye vizuri saana.
 
Kuchagua zawadi kazi ngumu sana ila omba mfanye matembezi ya kawaida tu mfano kama mko karibu na mbuga au bustani za wanyaama(zoo) yoyote mnaeza kwenda huko masaa machache tu yanatosha jioni kila mtu anaendelea na harakati zake.

Kama hupendelei matembezi ya aina io chagua unachoona unakipenda zaidi ila kiwe rahisi tu na gharama ya kawaida.
 
Waswahili daima husema bure ni ghali. Sasa akili mukichwa, kama ni story ya kweli japo ina ukakasi kuiamini basi juwa unaandaliwa kisaikolojia. Utapigwa kizinga kimoja cha haja unaweza jikuta unawekea rehani mpaka nyumba ya urithi.

Ila bado siamini kuwa hiki ni kisa cha kweli. Wabongo wanavyopenda dezo, ingekuwa kweli ungeogopa hata kuomba ushauri kwa hofu msesereko wako utaibiwa.
 
Aisee unabahati sana we mwambie unatamani ukamtambulishe kwenu kama mchumba ili baadae mfunge ndoa, halafu kaa kimya subiria jibu
 
Back
Top Bottom