USHAURI: Je, naweza kupata gari kwa shilingi milioni 6?

USHAURI: Je, naweza kupata gari kwa shilingi milioni 6?

Ndugu zangu nawasalimu humu,

Kama mada inavyojieleza hapo juu, ni kweli kiasi cha hiyo pesa naweza pata ka ndiga ka kuzugia au nijazie kidogo? Aina ya gari ni Toyota Run x, Allex, IST, Raum au Spacio.

Asanteni ndugu zangu, kikubwa naomba msaada wa mawazo na uzoefu wenu.
Nafikiri zile Brevis utazipata
 
Zina tatizo gani, maana zinauzwa sana
Kweli Brevis zimeshuka hadi milioni 6.5
naona tatizo ni ubwiyaji wa mafuta kwani zina cc kubwa hadi 3000cc
halafu kwa spidi ni kubwa sana 120 km/h mpaka 180 km/h kwa barabara za lami na huku kwetu mwisho ni 50 km/h
2001 Toyota Brevis in Dar Es Salaam
1eab16b816ab56c9d8a678206bdf7cb59e9bc52d.png

2001 Toyota Brevis
TSh 5,000,000
Brevis hii ni 5,000,000/ (milioni 5 tu)
Location
Kinondoni, Kimara Dar Es Salaam
Description
Transmiss. Automatic
Engine Size 2,990cc
Engine kubwa
Haina tatizo
Nzuri haijawai pata ajari
 
Zina tatizo gani, maana zinauzwa sana

Nilipata kuona uzi hapa kwamba zipo na bei nafuu mpaka 9M ila ukinunua haiuziki tena, nadhani kwasababu ya fuel consumption kuwa juu ...nadhani ina cc 2400+
 
unapata economic cars kama IST na magari mengine ila gari yenye Cc kubwa kama brevis sio nzuri kununua kwa sababu ya sharia ya barabara zetu za rami huku zinazosukuma 50km/h afu inatafuna mafuta mnoo,
 
Acha kumdanganya mwenzako. yeye kakwambia ana 6m
wewe unamshawishi akaongeze atazipata wapi kwa usawa huu?
muokotamatunda wewe ingia www.zoomtanzania.com huko kuna gari kibao na za bei yako uitakayo
hata za 5m km wasemavyo Member wengine
na uzuri wa huko unaongea na mwenye gari kabisa, hata km kuna Dalali hapo kati mwambie namtaka mwenye mali
Poa mkuu.
 
Mkuu ukitulia utapata nzuri tu, tazama matangazo kila sehemu, kuanzia zoomtanzania.com mpaka jumia.com..
Ulizia watu wa karibu, tembea tembea mjini kwa wadosi, hakika utafanikiwa...
 
Back
Top Bottom