Ushauri: Jitahidi kutembelea ndugu/jamaa na marafiki wenye uwezo wa Duni na wachini kabisa(masikini)

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Wana jamvi ni kwema? huku leo kuna baridi sana na kwa sababu hii kilimo cha watoto hakina mbadala.

Leo hii watu tumekuwa wabaguzi sana tofauti na kipindi cha nyuma utu ulikuwa sehemu ya maisha ya kila binadamu.

Na kwa sababu hatuna utu basi kuna msemo usemao ndenge wanao fanana huruka pamoja.Sipingi kwa maana hao ni denge na sisi ni binadamu utu wetu kwanza mengine badae.

Ukikaa na kujiuliza umeenda kutembelea watu wa chini wenye maisha duni umewatembelea lini? jibu linaweza kuwa hukumbuki. Lakini tukikuuliza swali hilihilo ila liwe kinyume chake utakumbuka na kukumbuka tena!!

Hatupangiani maisha ila tunakumbushana na kushauriana. Ijapokuwa humu vitabu vyetu vya dini vinabezwa na vitabu vya wakina kabendera na yeriko nyerere vinatukuzwa lakini ukweli biblia nje na imani ina mafundisho mazuri sana ya kuishi vizuri kwenye jamii zetu popote pale duniani!

Hili andiko linatuambia wazi maana ya dini ya kweli.......

Yakobo1:26Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe.
27Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.

Ebu siku moja mwambie ndg yako yoyote mwenye maisha duni kuwa sikukuu hii nakuja kwako au siku fulani nakuja kwako uone mwitikio wake na maandilizi yake yatakavyo kuwa ni zaidi ya ujio wa rais.Mtu huyu atajiona kumbe nami na thamani kiasi hiki?

Wewe ambae huwa unaona hata pa kulala huwa hupaoni nakuambia siku hiyo utalala pazuri sana na uta shangaa watu wa hivyo huwa wana umoja sana kijijini na wanaheshimiana si kwa sababu ya vitu ama mali la hasha bali utu na nidhamu waliyo jijengea.

Utalala pabaya tu iwapo umewasitukiza tena usiku wa manane, Nakwambia hata hicho kikombe utakachonywea chai ni maalumu kwa ajiri ya wageni kama wewe!! godoro hata mashuka huwa wanaenda kuazima kwa majrani na atapewa vilevile istoshe yule mama hata awe na maisha magumu kiasi gani hawezi koswa khanga na vitenge vya wageni.

Kule utakula kuku na mapishi natural adhimu kabisa........

Nakumbuka mimi na wife tukiwa na mtoto wetu first born nilimpa taarifa ndg mmoja upande wa mama kuwa sikukuu hii ya nanenane nakuja kuwasalimia ndg zangu mimi,mke wangu na rafiki yangu (dereva wa gari)

Niliamua kwenda na gari tena ya kuazima ili kumpa heshima tu ndg yangu yule pale kijijni kuwa kumbe naye ana ndg matajiri!! sio mbaya ni show off tu japo yeye hakujua kama nitaenda na gari pale...

Siku ilifika rafiki yangu yule dereva nilikuwa nimemwambia A-Z kuwa mazingira siyo kama alivyozoea hapa town naye akajibu wala nisiwaze kakulia maisha hayohayo na nilkuwa nimemkodi kwa 70k.Basi safari ikaanza njia haikuwa nzuri sana hatimae tukafika pale majira ya saa5 asbh.

Tulikuta Watoto wameoga na wamepakwa mafuta kwa fujo wana nga'aa ile mbaya na nguo mpya wamevaa!!
Basi gari ilizingilwa kwa mapokezi kama putin kadhuru iran.Baada ya kuona tu mazingira nikajiongeza hii familia ilikuwa imejiandaa sana na laiti kama ningekwama ningewakwaza sana.

Basi sio watoto wa pale tu walijaa bali na wale wa majirani na majirani wenyewe walikuja kutulaki mtoto wetu akawa wa kubebwa juu juu tu kama mwenge. Nilikuwa na furaha sana mimi na wife kwa muda huo.

Muda kama dka 40 hivi tukapita ndani kwenda kula vyombo vipya vilivyo tunzwa kwa ajiri yetu. Jioni ya saa11 tuliwabeba wenyeji wetu kwenye gari tukaenda kwenye senta yao nikanunulia vinywaji watu wa pale walio fahamiana na wenyeji wetu.

Huku gari yetu imezingilwa na watoto muda wote.By saa3 usiku tulirudi na kufikia kula tena msosi wa hatali.Wakati tunaenda tulibeba net kama tahadhari hasa mtoto na kweli ilitumika maana hapakuwa na net kule

Kesho yake tuliaga wakagoma kabisa tuliendelea kula kuku huku mwenyeji wetu akinitembeza kwa wanazengo wenzake nyumba kwa nyumba na kila tunapofika walikuwa wanatulazimisha watupikie tule kwanza ndo tuondoke siku hiyo ya trh 9 kidogo tulale kwingine maana hadi saa4 usiku tupo kwa jamaa mwingine tu tunapiga story

Ilibidi sasa trh 10 ndo tushinde kwenye mji tulipofikia Cha kushangaza tukiwa pale tukawa tunaona wamama wanaleta mizigo kwenye viroba kumbe ulikuwa mpunga!

kesho yake tuliagaa japo hawakutaka kabisa turudi siku hiyo.Sisi kipindi tunaenda tulikuwa tumebeba zawadi kidogo tu kwa mahesabu ya jumla haikufika hata 200k Lakini sisi kipindi tunarudi tulipewa vitu vingi sana kama kuku na nafaka ukikadiria na vile tulivyokula lazima izidi 200k.

Hii huwa na fanya hivi na kwanini leo nimeandika hapa? Ileile familia walijikongoja wakafuga mbuzi hatimae ng'ombe wapo kama saba kwa sasa na mbuzi kadhaa Leo nikiwa nimelala nikasikia sauti ya mbuzi ikipiga kelele huku wife akiwaambia mfungeni pale.

Ikabidi niamke ili nijue na kuona huyu mbuzi anayefungwa kwangu ametoka wapi? Ile natoka nikaona kijana aliye maliza form mwaka jana na kufaulu dv2 kaniletea zawadi nichinje nile namimi ni mpale si chinji nafuga!

Huyu dogo aliniomba hela ya kuwezesha mahafari yake. Nilikuwa na pair ya viatu ambavyo nilikuwa nimevivaa na baadhi ya nguo basi nikampa na hela 50k tu na nikasahau wala sikuulizia habari za matokeo yake leo ndo kaja nikaangalia kapata Dv2 shule kayumba. Nimemuahidi nitamsadia kadiri nitakavyoweza kwenye masomo yake!!

Mwisho tusipende kwenda kwenye misiba yao tu hata kwenye furaha yatupasa kujumuika nao vilevile.
 
Mwisho tusipende kwenda kwenye misiba yao tu hata kwenye furaha yatupasa kujumuika nao vilevile
Amkaaa usingizini mkuu 😂😂😂😂 ,Dunia ya Leo usipokuwa na kitu jua una thamani yyt ,,haka km n ndugu zako wa damu Wana pesa kipindi Cha ckuku wanatafuta wenye pesa wenzao wanaunga kikundi wanaenda zao Dubai,Serengeti,ngororo kula maishà,,ww maskin km una smart phone na namba zao unaishiaa tu kuonaa status mapicha picha 😂😂😂😂

Mchawi pesa pesa pesa pesa
 
Uko sawa ni mtazamo wako.Ndio maana nimetoa kama ushauri.Kwanini siku ya msiba huwa mnaenda na magari yenu?
 
Una mfano wa familia iliyojaa fadhila, ila wengi hukutana na majanga ya watu waliojaa roho mbaya na visasi vya ugumu wa maisha, kwa hiyo badala ya kufurahia hujikuta wameingia kwenye wingi wa kulaumiwa na mwisho kujilaumu, roho za kwanini wewe,wivu na kukomoa zinarudisha hata jitihada ndogo za kujaribu ulichosuggest.
 
Una mfano wa familia iliyojaa fadhila, ila wengi hukutana na majanga ya watu waliojaa roho mbaya na visasi vya ugumu wa maisha, kwa hiyo badala ya kufurahia hujikuta wameingia kwenye wingi wa kulaumiwa na mwisho kujilaumu, roho za kwanini wewe,wivu na kukomoa zinarudishaa hata jitihada ndogo za kujaribu ulichosuggest.
Mifano ni mingi mtu sitaweza kuandika yote.Kwa kifupi mtu mwenye roho mbaya awe tajiri ama maskini anafahamika tu kwenye ukoo.Muepuke
 
Wana jamvi ni kwema? huku leo kuna baridi sana na kwa sababu hii kilimo cha watoto hakina mbadala.

Leo hii watu tumekuwa wabaguzi sana tofauti na kipindi cha nyuma utu ulikuwa sehemu ya maisha ya kila binadamu.

Na kwa sababu hatuna utu basi kuna msemo usemao ndenge wanao fanana huruka pamoja.Sipingi kwa maana hao ni denge na sisi ni binadamu utu wetu kwanza mengine badae.

Ukikaa na kujiuliza umeenda kutembelea watu wa chini wenye maisha duni umewatembelea lini? jibu linaweza kuwa hukumbuki. Lakini tukikuuliza swali hilihilo ila liwe kinyume chake utakumbuka na kukumbuka tena!!

Hatupangiani maisha ila tunakumbushana na kushauriana. Ijapokuwa humu vitabu vyetu vya dini vinabezwa na vitabu vya wakina kabendera na yeriko nyerere vinatukuzwa lakini ukweli biblia nje na imani ina mafundisho mazuri sana ya kuishi vizuri kwenye jamii zetu popote pale duniani!

Hili andiko linatuambia wazi maana ya dini ya kweli.......

Yakobo1:26Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe.
27Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.

Ebu siku moja mwambie ndg yako yoyote mwenye maisha duni kuwa sikukuu hii nakuja kwako au siku fulani nakuja kwako uone mwitikio wake na maandilizi yake yatakavyo kuwa ni zaidi ya ujio wa rais.Mtu huyu atajiona kumbe nami na thamani kiasi hiki?

Wewe ambae huwa unaona hata pa kulala huwa hupaoni nakuambia siku hiyo utalala pazuri sana na uta shangaa watu wa hivyo huwa wana umoja sana kijijini na wanaheshimiana si kwa sababu ya vitu ama mali la hasha bali utu na nidhamu waliyo jijengea.

Utalala pabaya tu iwapo umewasitukiza tena usiku wa manane, Nakwambia hata hicho kikombe utakachonywea chai ni maalumu kwa ajiri ya wageni kama wewe!! godoro hata mashuka huwa wanaenda kuazima kwa majrani na atapewa vilevile istoshe yule mama hata awe na maisha magumu kiasi gani hawezi koswa khanga na vitenge vya wageni.

Kule utakula kuku na mapishi natural adhimu kabisa........

Nakumbuka mimi na wife tukiwa na mtoto wetu first born nilimpa taarifa ndg mmoja upande wa mama kuwa sikukuu hii ya nanenane nakuja kuwasalimia ndg zangu mimi,mke wangu na rafiki yangu (dereva wa gari)

Niliamua kwenda na gari tena ya kuazima ili kumpa heshima tu ndg yangu yule pale kijijni kuwa kumbe naye ana ndg matajiri!! sio mbaya ni show off tu japo yeye hakujua kama nitaenda na gari pale...

Siku ilifika rafiki yangu yule dereva nilikuwa nimemwambia A-Z kuwa mazingira siyo kama alivyozoea hapa town naye akajibu wala nisiwaze kakulia maisha hayohayo na nilkuwa nimemkodi kwa 70k.Basi safari ikaanza njia haikuwa nzuri sana hatimae tukafika pale majira ya saa5 asbh.

Tulikuta Watoto wameoga na wamepakwa mafuta kwa fujo wana nga'aa ile mbaya na nguo mpya wamevaa!!
Basi gari ilizingilwa kwa mapokezi kama putin kadhuru iran.Baada ya kuona tu mazingira nikajiongeza hii familia ilikuwa imejiandaa sana na laiti kama ningekwama ningewakwaza sana.

Basi sio watoto wa pale tu walijaa bali na wale wa majirani na majirani wenyewe walikuja kutulaki mtoto wetu akawa wa kubebwa juu juu tu kama mwenge. Nilikuwa na furaha sana mimi na wife kwa muda huo.

Muda kama dka 40 hivi tukapita ndani kwenda kula vyombo vipya vilivyo tunzwa kwa ajiri yetu. Jioni ya saa11 tuliwabeba wenyeji wetu kwenye gari tukaenda kwenye senta yao nikanunulia vinywaji watu wa pale walio fahamiana na wenyeji wetu.

Huku gari yetu imezingilwa na watoto muda wote.By saa3 usiku tulirudi na kufikia kula tena msosi wa hatali.Wakati tunaenda tulibeba net kama tahadhari hasa mtoto na kweli ilitumika maana hapakuwa na net kule

Kesho yake tuliaga wakagoma kabisa tuliendelea kula kuku huku mwenyeji wetu akinitembeza kwa wanazengo wenzake nyumba kwa nyumba na kila tunapofika walikuwa wanatulazimisha watupikie tule kwanza ndo tuondoke siku hiyo ya trh 9 kidogo tulale kwingine maana hadi saa4 usiku tupo kwa jamaa mwingine tu tunapiga story

Ilibidi sasa trh 10 ndo tushinde kwenye mji tulipofikia Cha kushangaza tukiwa pale tukawa tunaona wamama wanaleta mizigo kwenye viroba kumbe ulikuwa mpunga!

kesho yake tuliagaa japo hawakutaka kabisa turudi siku hiyo.Sisi kipindi tunaenda tulikuwa tumebeba zawadi kidogo tu kwa mahesabu ya jumla haikufika hata 200k Lakini sisi kipindi tunarudi tulipewa vitu vingi sana kama kuku na nafaka ukikadiria na vile tulivyokula lazima izidi 200k.

Hii huwa na fanya hivi na kwanini leo nimeandika hapa? Ileile familia walijikongoja wakafuga mbuzi hatimae ng'ombe wapo kama saba kwa sasa na mbuzi kadhaa Leo nikiwa nimelala nikasikia sauti ya mbuzi ikipiga kelele huku wife akiwaambia mfungeni pale.

Ikabidi niamke ili nijue na kuona huyu mbuzi anayefungwa kwangu ametoka wapi? Ile natoka nikaona kijana aliye maliza form mwaka jana na kufaulu dv2 kaniletea zawadi nichinje nile namimi ni mpale si chinji nafuga!

Huyu dogo aliniomba hela ya kuwezesha mahafari yake. Nilikuwa na pair ya viatu ambavyo nilikuwa nimevivaa na baadhi ya nguo basi nikampa na hela 50k tu na nikasahau wala sikuulizia habari za matokeo yake leo ndo kaja nikaangalia kapata Dv2 shule kayumba. Nimemuahidi nitamsadia kadiri nitakavyoweza kwenye masomo yake!!

Mwisho tusipende kwenda kwenye misiba yao tu hata kwenye furaha yatupasa kujumuika nao vilevile.
Unajua kinachofanyika sasa hv yatima na wajane wanasaidiwa na watu ambao wameamua kutumika na shetani ili shetani apate utukufu ljn bado watu waMungu wasijisahau hili ni jukumu letu ila hali ya maisha inatusonga sna mwenyez Mungu atukumbuke
 
Hakika mkuu
 
Watu wanapenda kwenda kwa matajiri tu
 
Back
Top Bottom