Ushauri juu kesi hii je nitaishinda.

Ushauri juu kesi hii je nitaishinda.

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
457
Reaction score
328
Kuna jirani angu tarehe 22.03.katika maelezo yake alidai mnamo mda wa saa saba usiku alikuwa ameweka simu 2 na computer juu ya meza karibu na dirisha.
Kipindi amelala aliskia watu wanagusa kitasa cha mlango wake.
Mara akaskia kama upepo unapuliza na dirisha kufunguka (dirisha ni la nyavu na nondo linafungiwa ndani) basi ndipo alipoona watu wakichukua simu na baadae wakibeba na computer mezani.

Katika maelezo yake hayo anadai alivyokuja kuchungulia kwenye tundu la dirisha akanitambua mimi kwa mbali tukiwa tunakimbia na mali yake. Akarudi kulala na kuamka saa 1:30 asubuhi huku akidai amemuona aliyemuibia na kwenda kuripoti chuo na baadae polisi
Juzi kanipeleka polisi na kuniweka maabusu.

Kwa upande wangu sikufanya tukio hilo na wala sina tabia ya wizi ila nilichokigundua ni kuwa kwa kuwa mimi najiweza kifedha angalau kidogo ninaweza kumlipa kirahisi.
Kesho tunapanda mahakamani kujibu mashitaka nami kama ushindi nauona njenje.

Ushauri wenu juu ya maswali ntakayomuuliza ashindwe kuyajibu maana yeye mwenyewe hajiamini na ukweli anajua sio mimi ila tu anataka alipwe.
 
Kama alikuona na kukujua kwa nini hakupiga yowe kuita jina lako, na nini kinamdhibitishia kuwa wewe ni mwizi? Je alishawahi kusikia kuwa umeiba sehemu na je anaweza kuthibisha?
 
Kama alikuona na kukujua kwa nini hakupiga yowe kuita jina lako, na nini kinamdhibitishia kuwa wewe ni mwizi? Je alishawahi kusikia kuwa umeiba sehemu na je anaweza kuthibisha?
Hapo sasa nami ndo nataka nkazie hapo
 
ili utiwe hatiani ni lazima mahakama ijiridhishe beyond any reasonable doubt, sasa kwahiyo tuhuma huwezi kutiwa hatiani!
 
Hapo hakuna kesi!
Utakuwa cjuh mwanfunxi!
But mbane kwenye ushahid na vielelezo!!
 
Binafsi wakat nasoma chuo ishawah Nikuta
Niliambiwa nimeiba
Cm na laptop
Nikapelekwa polisi pale ud
But niliwabana kwa evidence na nikala ma fidia juu!!!
 
Unaeza kumchomekea kuwa aache wivu, wanawake wako wengi,
 
Maelezo yako ndio yatakayokufunga.
Kwanza umejuaje yeye amekuchagua wewe kwa kuwa unajiweza ili umlipe? Hapo kuna mashaka maana yaelekea unamjua na kisa kizima unakijua.
Pili maelezo yako yanaonesha unajua unachokitetea.
 
Back
Top Bottom