scientificall
JF-Expert Member
- Jun 4, 2015
- 457
- 328
Kuna jirani angu tarehe 22.03.katika maelezo yake alidai mnamo mda wa saa saba usiku alikuwa ameweka simu 2 na computer juu ya meza karibu na dirisha.
Kipindi amelala aliskia watu wanagusa kitasa cha mlango wake.
Mara akaskia kama upepo unapuliza na dirisha kufunguka (dirisha ni la nyavu na nondo linafungiwa ndani) basi ndipo alipoona watu wakichukua simu na baadae wakibeba na computer mezani.
Katika maelezo yake hayo anadai alivyokuja kuchungulia kwenye tundu la dirisha akanitambua mimi kwa mbali tukiwa tunakimbia na mali yake. Akarudi kulala na kuamka saa 1:30 asubuhi huku akidai amemuona aliyemuibia na kwenda kuripoti chuo na baadae polisi
Juzi kanipeleka polisi na kuniweka maabusu.
Kwa upande wangu sikufanya tukio hilo na wala sina tabia ya wizi ila nilichokigundua ni kuwa kwa kuwa mimi najiweza kifedha angalau kidogo ninaweza kumlipa kirahisi.
Kesho tunapanda mahakamani kujibu mashitaka nami kama ushindi nauona njenje.
Ushauri wenu juu ya maswali ntakayomuuliza ashindwe kuyajibu maana yeye mwenyewe hajiamini na ukweli anajua sio mimi ila tu anataka alipwe.