Ushauri juu ya biashara ya kitimoto

Ushauri juu ya biashara ya kitimoto

Soko lake si haba maana ni mnyama anaeongoza kwa utamu huku akifuatiwa na kuku..so fuga tu mkuu washabiki wa hiyo kitu tuko wengi sana
 
Jamani mie nina plan ya kufuga kitimoto kwa wingi.
nmesha fuatilia kwa karibu gharama infmashen nyingi ila
kabla sijaanza ufugaji wenyewe naomba nijue kuhusu soko.
nia yangu ni kufuga na kuuza wakiwa wazima (sio kuuza nyama)
kwa hivyo naomba ajuaye anifahamishe wapi lilipo soko zuri la hii nyama nzuri.
soko hilo lipoje(kama kwa kilo ni bei gani)?
kwa uwezo wangu na plan yangu naweza kutoa kitimoto sio chini ya 50 kila awamu.

Mimi nipo mwanza.

Nnaomba kufahamishwa please.

Uko Mza sehemu gani Mkuu nikuelekeze kwa wafugaji wazoefu wa hiyo mifugo?
 
Usiogope Mkuu sheria ipo itawafunga ndani. Kuna wa2 walifanya hivyo wakalipa fidia ya ukweli...

Nguruwe anafaida sana mkuu. Na wala hana Gharama kubwa kama Wanyama wengine kwenye Vyakula.
Ukisema hawana gharama kubwa labda unalinganisha na kuku wa kisasa. Vinginevyo nguruwe ni kati ya mifugo yenye gharama kubwa za ulishaji. Hadi waingereza wana msemo huu: "A pig is a sack of grain by another name". Wanamaanisha kulisha nguruwe ni sawa na kujaza nafaka kwenye gunia.
Kwa mfano huwezi kufananisha nguruwe na ng'ombe kwa sababu chakula kikuu cha ng'ombe ni nyasi vingine ni vya ziada ili kuboresha lishe.
 
Mi nishawafuga Najua Kwahiyo siongei tu... Mi sifuatu Misemo Ya Mitandao...

Kuna Waty humu wanaweza kukupa gharama wakakukatisha Tamaa Za Kufuga ...
 
Hali ya uchumi imeyumbisha biashara ya kitimoto ukilinganisha na zamani. Mauzo yake makubwa ni kwenye baa, ambazo sasa zimeamuriwa kufunguliwa saa 10 ili watu wafanye kazi, kana yenyewe si kazi. Pia pumba, chakula kikuu cha ktm, bei iko juu. Faida ya hiyo biashara si kubwa kama wasemavyo, na hasa ukitunza kumbukumbu za shughuli yote. Mtaji mkubwa wa biashara hiyo ni ujenzi wa mabanda.
 
Umenena vema Mkuu, pumba iko juu kwa sasa gharama za chakula kwa ufugaji wa pig ni wa juu kila kukicha. Hapa Jf watu wengi si wakweli. Sisi wafugaji wakongwe tunajua A-Z.
 
Umenena vema Mkuu, pumba iko juu kwa sasa gharama za chakula kwa ufugaji wa pig ni wa juu kila kukicha. Hapa Jf watu wengi si wakweli. Sisi wafugaji wakongwe tunajua A-Z.
ukitaka kufuga nguruwe andaa kabisa shamba la mahindi kama hekari 6 hivi la kulisha nguruwe pamoja na alizet kidogo.nakuakikishia hautokuja kujuta kamwe
 
Wakuu,

Nampango wa kufungua sehemu kwa ajili ya kuchoma/kuroast kitimoto. Kwa ambaye anauzoefu wa biashara hii naomba ushauri tafadhali hususani kwenye vitu vya muhimu kuzingatia kabla ya kuanza na baada ya kuanza hii biashara.

Binafsi ninampango wa kufungua sehemu ambayo siyo bar ila ni karibu na taasisi ya elimu yenye wanafunzi wengi. Ugali, Ndizi, Kitimoto, vinywaji baridi ndivyo natagemea kuviuza (Pombe haitakuwepo).

Natanguliza shukrani.

10502143_952141531466932_3650862621506676574_n.jpeg
 
Kwanza usiwategemee wanafunzi kwenye hiyo biashara kwa 7bu kipindi hiki wengi wanasoma kwa shida.

Fanya hivi
Angalia kwanza kama kuna waislam wengi maeneo hayo??

Hafu angalia je walaji wapo?
Kiukweli hiyo biashara kiustaarabu bila kuwa karibu na bar uuzwaji wake hua shida
 
Hiyo biashara sio ya kuuliza, ni wewe tu na pesa zako uanze kupiga hela. Cha msingi ni kuwepo kwenye pilika pilika za watu,ila hapo pa kutokuwepo kwa vinywaji vikali ndipo utakapokosea,maana mdudu mwenzie "ngumu kumeza"
 
Kwanza usiwategemee wanafunzi kwenye hiyo biashara kwa 7bu kipindi hiki wengi wanasoma kwa shida.

Fanya hivi
Angalia kwanza kama kuna waislam wengi maeneo hayo??

Hafu angalia je walaji wapo?
Kiukweli hiyo biashara kiustaarabu bila kuwa karibu na bar uuzwaji wake hua shida

Mkuu, eneo hili wanafunzi ndiyo wengi na ndiyo wateja wakubwa wanaotegemewa, labda ni kubadili namna ya kuuza hiyo kitimoto, kwamba kama wanaishi kwa shida basi iwepo kitimoto wanayoweza kuimudu. Hapo je?
 
Back
Top Bottom