Laki ni ndogo lakini inaweza kukufanya ufike mahali yaani ukuze mtaji kama ifuatavyo..
Chukua 20,000 shona barakoa 150-200 nenda masokoni,kwenye taasisi au wape vijana wakauze kwa shilingi 500 moja.
wapitishie bodaboda,daladala(abiria na madereva) tena kwenye daladala fanya kama wale wajasiriamali wa sabuni uwe muongeaji na uwaelimishe kisha wauzie barakoa ila usipotoshe kuhusu huu ugonjwa. Jikite kuwaeleza faida ya bidhaa yao.
80,000 tafuta mabinti wawili nunua chupa za chai koroga uji wakauze vijiwe mbalimbali asubuhi sana na jioni kwasababu njombe kuna baridi.
Au
Pesa yote kanunue kuku vijiji kwa 7,000 hadi 10,000 kawauzie wenye majiko bar au hotelini ila usiwe na tamaa upate faida kubwa zitakudodea ila ukifocus kwenye kutengeneza wateja wa uhakika hatakama faida ndogo mzigo utakuwa unauza mara kwa mara tena watakusumbua.
vile vile ukiweza ongeza thamani kuku zako sio uwachinje no uza kuku wape wateja ofa ya pilipili au malimao.
e.t.t