Ushauri Juu ya kuanza Biashara kwa mtaji wa laki moja

Ushauri Juu ya kuanza Biashara kwa mtaji wa laki moja

Laki ni ndogo lakini inaweza kukufanya ufike mahali yaani ukuze mtaji kama ifuatavyo..

Chukua 20,000 shona barakoa 150-200 nenda masokoni,kwenye taasisi au wape vijana wakauze kwa shilingi 500 moja.
wapitishie bodaboda,daladala(abiria na madereva) tena kwenye daladala fanya kama wale wajasiriamali wa sabuni uwe muongeaji na uwaelimishe kisha wauzie barakoa ila usipotoshe kuhusu huu ugonjwa. Jikite kuwaeleza faida ya bidhaa yao.

80,000 tafuta mabinti wawili nunua chupa za chai koroga uji wakauze vijiwe mbalimbali asubuhi sana na jioni kwasababu njombe kuna baridi.

Au

Pesa yote kanunue kuku vijiji kwa 7,000 hadi 10,000 kawauzie wenye majiko bar au hotelini ila usiwe na tamaa upate faida kubwa zitakudodea ila ukifocus kwenye kutengeneza wateja wa uhakika hatakama faida ndogo mzigo utakuwa unauza mara kwa mara tena watakusumbua.

vile vile ukiweza ongeza thamani kuku zako sio uwachinje no uza kuku wape wateja ofa ya pilipili au malimao.

e.t.t
Kuku ni changamoto kwa mtaji huo anaweza poteza wote,
 
kuku naunga mkono idea biashara ya uchuuzi inataka ujanja ni kwenda kwa watu wa bar kuwapanga una mzigo ila itataka research kabla ujue bei ya unakonunua iwe pembeni kidogo ya mji ili isikucost gharama zaidi then ongeza cha juu mfano ukinunua kwa 8000 jogoo kauze 10000 uwe competitive chukua laki utapata jogoo 10 wa kuanza faida iwe 2000 kwa jogoo utakuwa na 20000 per trip kama net profit nauli isiwe zaid ya 5000 kwenda kurudi angalau upate 15000 kwa trip ukipata baiskeli hata ya kukodi itakuwa poa sana Fanya research jenga mahusiano na watu wa mabar managers utapiga hatua I swear be serious ila tembea kwa machale maana kupata Right information hapo katikati unaweza lambwa
 
Fanya research ya phone accessories base kwenye vitu vifuatavyo memory card,earphones pia battery za simu ndogo chagua kimoja tu.mfano battery ndogo zinazoingiliana zinauzwa kuanzia buku na kuendelea zipo pia chini ya buku kwa jumla ila ni fake usijali sana wewe uza 4000/5000 kwa laki chukua mzigo wa tisini elfu utapata betri 90 ukiuza kwa 4000 utapata 360k faida zaidi ya 250k, earphone nako utachukua za buku jero na buku mbili utauza buku 5 kama utachagua earphones, kama memory utachukua zile ndogondogo ile ni lazima uzitembeze anza na washkaji mzigo ni kkoo so tafuta jamaa yako wa dar umpange akakuchukulie na akutumie malipo mtakubaliana usihofu kuanza na tumzigo tudogo angalia faida
Pia angalia bei za mayai pembeni ya mji kama zipo reasonable kusanya ongea na wakaanga chips uwauzie kwa bei reasonable mfano trey 9000 wewe uza kwa 12000 kama itafaa lakini kwa huko njombe so utapata trey 10 faida itakuwa 30000 sio mbaya kuna mzee alikuwa anafanya hii mishe na anaishi changamoto ni nyingi ukiwa hujui kuhifadhi utakula loss ya ajabu pia
 
Back
Top Bottom