Ushauri juu ya matumizi ya sauna

Hii ya kuchanganya miarobaini na baadhi ya majani nilishawahi fanyiwa na bimkubwa nakumbuka nilikamatwa na Malaria kali sana nikapigwa hii kitu asee jasho jingi lilitoka baada siku mbili Malaria kwisha habari haya madawa ya hospital mda mwingine yanajaza sumu mwilini asee.
 
agreed; KUFUKIZWA TUNAITA HUKO TZ

 
Chapa shoka ndio nini wakuu?
 
Yes, sisi tuliita 'kufukiza' na kule kwetu walikuwa wanachemsha madawa ya mitishamba kwenye chungu kikubwa kilichofunikwa vizuri na jani la mgomba, madawa yakishachemka chungu kinaepuliwa mtu anakaa kwenye kigoda anafunikwa na mablanketi na chungu kinawekwa ndani ya blanketi. Mfukizwagi anakuwa anafunua lile jani la mgomba taratibu mvuke unatoka unamzingira mule ndani ya blanketi. Unafanya hilo zoezi dk 45 mpaka lisaa unatoka jasho kweli kweli, Kisha unatoka kwenda kuoga kabla jasho halijakukaukia. Bibi yetu alitufanyia sana wajukuu wake. Kwa sasa hakuna tena naona watu wako busy na mahospitali
 
Hahaha nyungu ya mawe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…