Kama elii alivyosema ukizoea sauna huwezi kuacha. Mimi nimekuwa addicted na sauna sana. Naingia pale mara mbili kwa wiki na gharama yangu kwa wiki ni kama Tshs.14,000. Lakini hiyo naona siyo kitu. Nimepata nafuu sana. Kitu kama malaria, gauti na magonjwa mengine ni kama historia. Unapotoka pale unakuwa sana mwepesi. Ngozi inakuwa sana laini na ukilala unalala usingizi wa pono. Wazazi wetu huko nyuma walikuwa na sauna yao. Mfano kama mtu alikuwa naumwa kila mara waliweza kuchemsha maji kwenye chungu kikubwa na lile chungu linafunikwa na blanketi kubwa na wewe pia unafunikwa na lile blanketi kwa hiyo ule mvuke unaotaoka kwenye chungu unakufikia na mhusika kuanza kutoa jasho jingi. Wazungu wameiboresha lakini na sisi waafrika tulikuwa na sauna yetu. Sauna ni tiba hasa ukitumia chapa shoka.