Ushauri: Kaambiwa na mwanamke wanayeishi ili atambulike rasmi lazima amrudishie mahari ng'ombe 15 mumewe wa ndoa waliyetengana naye miaka kadhaa

Ushauri: Kaambiwa na mwanamke wanayeishi ili atambulike rasmi lazima amrudishie mahari ng'ombe 15 mumewe wa ndoa waliyetengana naye miaka kadhaa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Hiyo siyo hadithi ni jambo la kweli kabisa limemtokea Jirani yangu hapa nyakato mwanza

Kaishi na mwanamke wa jamii ya wakulya mwaka wa nane huu wakizaa watoto wawili

" Mkewe" majuzi tu ndo kamjuza ili atambulike rasmi na awe na haki zote ikiwamo Watoto walozaa yafaa akamuone mumewe wa ndoa yule ambaye alitoa mahari ya ng'ombe 15 kwa wazazi wakati wa ndoa yao

Kwamba akishamuona mumewe huyo waliyetengana naye miaka kadhaa amuombe kumrudishia mahari yake ya ng'ombe 15 aliyotoa wakati wa ndoa

Kwamba mumewe huyo ambaye kikazi ni mjeda akikubali tu upokea ng'ombe hao basi kuanzia hapo huyo jamaa atahesabika kuwa MUME halali wa ndoa wa mwanamke huyo!

Jamaa huyo kaniomba ushauri nikasema siyo mbaya nikiwashirikisha ndugu zangu wa jamii forum

Niwatakie siku njema
 
Kwetu sisi ili ndoa ivunjike ni hadi urudishiwe mahari uliyotoa
sasa huyo ambaye umemchukua unaweza kurudisha hiyo mahari na siyo kurudisha, wewe unatoa mahari
na wazazi ndo warudishe kule kwa mwanzo.
na asibaki hata ng'ombe mmoja katika hiyo mahari. akibaki hata mmoja bado ni mke wake halali
na huyo jamaa akitoa mahari na watoto anaachiwa ni wa kwake
so mwambie hajaokota dodo
 
Hukuti mjadala kama huu kwa mwanamke ambae umepiga show hadi pakawaka moto!
Mpe jamaa Yako mkongo mwambie apake kidoooogo sana asafishe oblangata ya huyo ambae bado anamuwaza mjeda.
 
Huo ndiyo utaratibu rudisha mahari wewe unataka uendelee kula tunda bure tu. Halafu kwa nini umsingizie jirani yako si ungesema tu ni wewe mkuu wala tusingekucheka!
 
Kwetu sisi ili ndoa ivunjike ni hadi urudishiwe mahari uliyotoa
sasa huyo ambaye umemchukua unaweza kurudisha hiyo mahari na siyo kurudisha, wewe unatoa mahari
na wazazi ndo warudishe kule kwa mwanzo.
na asibaki hata ng'ombe mmoja katika hiyo mahari. akibaki hata mmoja bado ni mke wake halali
na huyo jamaa akitoa mahari na watoto anaachiwa ni wa kwake
so mwambie hajaokota dodo
Sasa watoto wa nini wakati siyo damu yake!!?
 
Back
Top Bottom