Ushauri: Kafaulu lakini anataka kuolewa

Ushauri: Kafaulu lakini anataka kuolewa

USHAUR wangu,
Angalia na mtu mwnyw anaetaka kumuoa bint yako.

Kama anaeleweka na umemwelewa kuweza kumtunza na kumhakikishia usalama binti yako.

Mruhusu aolewe TU.
 
Ashatimiza miaka 18, na elimu ya msingi ameshamaliza. Hilo la kuendelea au kutoendelea ni juu yake.

Kama kaamua kuolewa, mwache aolewe.
Kama ningekua ni mimi, kwakua huyo ni mwanangu na nna maamuzi nae basi ningemwambia yafuatayo.

Mimi kama baba yako nataka uendelee na shule, kwani ndio ufunguo wako wa maisha na mimi kama mzazi nitajiona natizmiza wajibu wangu kwa wewe kusoma. Lakini kwakua umetaka ndoa, na mimi nimetimiza jukumu langu la kukusomesha mpaka hapo ulipofikia basi nakuruhusu uolewe.
Ila kumbuka, ukiwa hapa kwangu kila kitu kukuhusu wewe ni juu yangu ila unapoenda kuolewa jua kila kitu kukuhusu ni kwa mumeo na sio mimi tenaa. Kwaheri.
 
Kw wakati nasoma (sio zamani sana) ni nadra sana kuona binti mwenye uwezo wa kupata division I afu hataki kuendelea naa shule...Napata ukakasi na story yako mkuu
 
Wewe, na Muoaji nyote mtakumbwa na mkono wa Sheria
 
Mwanaume ana 28, na anajihusisha na biashara. Kuhusu kumtunza sina shaka naye hilo ataliweza vyema..! Ila wasi wasi ni serikali hawawezi kuleta shida kwa kuruhusu binti aliyefaulu kuolewa?
Unakaa visiwani au tanzania bara ?
 
Hapo kuwa na roho mbaya we ni mbongo acha kulea kizungu, achague kwenda shule au msijuane
 
Wakuu habari za wakati.....!

Unaambiwa kwa mwenzako sikia ila omba yasikukute, Mimi yamenikuta na ni kitu ambacho sikuwaza.....! Iko hivi

Nina mwanangu wa kike kamaliza kidato cha nne mwaka huu kafaulu vizuri kwa div 1 kali tu...! Lakini cha ajabu amegoma kata kata kwenda shule akidai anataka kuolewa, na amemleta huyo mchumba hadi nyumbani ili taratibu zingine zifuate.

Sasa wakuu nimeshauri na kumsihi sana aachane na mawazo hayo azingatie masomo lakini imeshindikana....!

Na hasa ukizingatia ni mtoto wa kike, nimeona haina haja ya kumlazimisha sana kitu ambacho hataki..! Maana hata nikimzuia ipo Siku ataolewa tu....! Ngoja nimuache aende kupambana kwa alichokiamua...!

Ila wasi wasi wangu kama nikiamua kukubali kumuoza vipi siwezi kuchukuliwa hatua kwa kuruhusu aolewe akiwa amefaulu? Na ndo kwanza ana miaka 18, namuona bado mdogo kuingia kwenye ndoa...! Nashangaa ujasiri wa kulazimisha kuolewa kautoa wapiii....!

Sheria inasemaje kuhusu msichana aliyemaliza kidato cha nne akaamua kwa hiari asiendelee na shule, na kuamua kuolewa? Ushauri wenu muhimu sana wakuuu
Kwa nini usiongee na huyo mtu wake? Ukamshawishi avute muda, binti hatakuwa na jinsi. Ila itabidi aende chuo, apate ujuzi wowote na baada ya miaka 2 au 3 aingie ndoani.
Huyo bwana akikataa, hutaweza kumshawishi binti lolote.
Kuhusu Sheria, unaweza kumshitaki huyo bwana Kwa kuanzisha mahusiano na mwanafunzi, ila uwe mwangalifu, binti anaweza kujidhuru. Hivyo shirikisha watu wa serikali, wanasheria na ndugu wa pande zote ili mfikie muafaka wa lolote Kati ya kusoma au ndoa.
 
Ototo Wewe na Ototo yule kijana mwenye miaka 27 ni watu wawili tofauti au ni mmoja???

Baba kuambiwa maneno ya hvo na mwanao jua tatizo ni wewe wala hata sio mwanao...

Pili wewe ototo mwenye miaka 27 achana na mapenzi,,hayatakusaidia lolote
 
Mwanaume ana 28, na anajihusisha na biashara. Kuhusu kumtunza sina shaka naye hilo ataliweza vyema..! Ila wasi wasi ni serikali hawawezi kuleta shida kwa kuruhusu binti aliyefaulu kuolewa?
Kumbe wewe unataka mwanao aolewe..na ukute kajamaa kana hela..mbona unashabikia serikali serikali..wewe km.kweli ni baba huna maamuzi km.mzazi..yn usomeshe hlf aishie kuolewa udogoni...
Sio bure huyo mkwe ana walisha hapo kwako

Mtt nizae mwenyewe anishinde maamuzi[emoji849]

Au hii ni chai...
 
Usikubali aolewe saiv aende shule. Hajala ujana hata kidogo atakuja kujuta baadae. Na huyo mwanaume hana haya.
 
Kumbe wewe unataka mwanao aolewe..na ukute kajamaa kana hela..mbona unashabikia serikali serikali..wewe km.kweli ni baba huna maamuzi km.mzazi..yn usomeshe hlf aishie kuolewa udogoni...
Sio bure huyo mkwe ana walisha hapo kwako

Mtt nizae mwenyewe anishinde maamuzi[emoji849]

Au hii ni chai...
Hata mimi hapo amenishangaza jaman mmmh
 
Wakuu habari za wakati.....!

Unaambiwa kwa mwenzako sikia ila omba yasikukute, Mimi yamenikuta na ni kitu ambacho sikuwaza.....! Iko hivi

Nina mwanangu wa kike kamaliza kidato cha nne mwaka huu kafaulu vizuri kwa div 1 kali tu...! Lakini cha ajabu amegoma kata kata kwenda shule akidai anataka kuolewa, na amemleta huyo mchumba hadi nyumbani ili taratibu zingine zifuate.

Sasa wakuu nimeshauri na kumsihi sana aachane na mawazo hayo azingatie masomo lakini imeshindikana....!

Na hasa ukizingatia ni mtoto wa kike, nimeona haina haja ya kumlazimisha sana kitu ambacho hataki..! Maana hata nikimzuia ipo Siku ataolewa tu....! Ngoja nimuache aende kupambana kwa alichokiamua...!

Ila wasi wasi wangu kama nikiamua kukubali kumuoza vipi siwezi kuchukuliwa hatua kwa kuruhusu aolewe akiwa amefaulu? Na ndo kwanza ana miaka 18, namuona bado mdogo kuingia kwenye ndoa...! Nashangaa ujasiri wa kulazimisha kuolewa kautoa wapiii....!

Sheria inasemaje kuhusu msichana aliyemaliza kidato cha nne akaamua kwa hiari asiendelee na shule, na kuamua kuolewa? Ushauri wenu muhimu sana wakuuu
Duuh, Mungu atupe hekima sana, huyo mtoto anapaswa kusaidiwa ili aendelew na masomo, msiue ndoto zake kwa kumruhusu kuolewa, akigoma sana peleka hata jeshini akili ikomae
 
Simama kama baba utoto tu unamsumbua baadae atakuja kukupa lawama ww mwenyewe akishazalishwa watoto watatu na kuachika ndo atakuja kukuona ww hufai.
 
Kumbe wewe unataka mwanao aolewe..na ukute kajamaa kana hela..mbona unashabikia serikali serikali..wewe km.kweli ni baba huna maamuzi km.mzazi..yn usomeshe hlf aishie kuolewa udogoni...
Sio bure huyo mkwe ana walisha hapo kwako

Mtt nizae mwenyewe anishinde maamuzi[emoji849]

Au hii ni chai...
Ukija kuzinduka unakuja kushtuka kumbe mleta mada ndio huyo kijana anaetaka kuoa binti wa form 4 ila kaileta hii story kwa style ya kupindua meza ili ajithibitishie kama anachofanya ni kosa kisheria au la?
Huyu kijana ni akili mingi, amefanikiwa kuchezea akili ya muhitimu sasa hivi anachezea akili za wanajamii [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Chai kama chai [emoji57][emoji57]kujaza saver tu [emoji867][emoji867][emoji867]
 
Anahitaji ushauri nasaha. Ndio kazi zetu hizo mkuu. Karibu DM
 
Back
Top Bottom